12 May 2011

Waliochoma vibanda vya Wabara kortini

Na Mwajuma Juma, Zanzibar

WATU sita wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya kuchoma moto mabanda ya biashara yanayomilikiwa na wafanyabiashara wenye asili ya
Tanzania Bara huko katika Kijiji cha Pwani Mchangani Wilaya ya Kaskazini A, Unguja.

Watu hao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Bw. George Joseph Kazi katika Mahakama ya Mkoa Vuga Mjini Zanzibar.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Bw. Mohammed Khamis aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Haji Ame Idd (45), Talib Faki Ame (60), Mohammed Haji Sheha (21), Mohammed Massoud Afadhali (21), Mwinyi Abdallah Msanif (22), pamoja na Hassan Makame Chande (21), wote wakiwa ni wakazi wa Pwani Mchangani Zanzibar.

Mwendesha Mashtaka huyo alidai kuwa washtakiwa hao wanadaiwa Mei 5, mwaka huu, kati ya saa 10:00 na saa 12:00 jioni huko Pwani Mchangani walichoma moto mabanda ya biashara na kusababisha hasara ya zaidi ya sh. milioni 80.4, Euro 70 na dola 60 za Marekani.

Washtakiwa hao waliofikishwa mahakamani hapo wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), walikana mashtaka yao na kuomba wapatiwe dhamana kupitia wakili wao, Bw. Abdallah Juma.

Wakili alisema kwa mujibu wa ibara ya 12 (6) a ya Katiba ya Zanzibar, washtakiwa hao wana haki ya kupata dhamana kwa makosa kama hayo, kwa vile sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai namba 7 kifungu cha 150 ya mwaka 2004 yametajwa makosa yasiyokuwa na dhamana.

Makosa hayo ni uhaini, mauaji, makosa ya ujambazi wa kutumia silaha na dawa za kulevya.

Hata hivyo, Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Bw. Mohammed Khamis alisema kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kuna watuhumiwa wengine bado wanaendelea kutafutwa na kuachiwa kwao kunaweza kukaathiri upelelezi.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Kazi aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 23, mwaka huu ambapo mahakama itatoa uamuzi kuhusu suala la dhamana kwa washtakiwa hao.

Mapema mamia ya wananchi kutoka kijiji cha Pwani Mchangani walifika mahakamni hapo na kuishia nje ya lango kuu, wakifuatilia kesi hiyo akiwemo mbunge wa Jimbo la Matemwe Bw. Kheri Khatib.

Watu hao baadaye waliondoka na kuagana kwa dua maalumu ambayo ilisomwa na watu hao waliokuwa wamekusanyika nje ya ofisi za Shirika la Bima na walianza kupanda katika mabasi yasiyopungua sita kurejea kijijini baada ya kesi yao kuahirishwa.

7 comments:

  1. Nao hao Wapemba wamezidi kwa kuwabagua Wara, hao waliokamatwa kwa kosa hilo wakanyee ndo kwanza ili waonje joto ya jiwe, hao ni wauwaji na wasionewe huruma.

    ReplyDelete
  2. Ahaa walitumwa hao! wabara amkeni si mnaona hamtakiwi unguja? wazenji wanaoishi huko bara mnalionaje hili?

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu anonymous 9:51 hapo juu, Wazenji wanaoishi huku bara wana masikio - wamesikia; na ndugu zao walio Zenji wana macho - wameona. Ushauri wa bure kwao - waaanze kufungusha na kuondoka mapema kabla Wabara nao hawajaamua kufanya kweli. Hatuwezi kuona ndugu zeti wakifa maskini wakiwa kwao na sisi huku tukenue meno kufurahia. HAIWEZEKANI!!!

    ReplyDelete
  4. Sheri ichukue mkondo wake, iwe fundisho kwa wengine, kwani wengi wao hawapendi kabisa kuwaona wabara huko Unguja hivyo sheri isipochukua mkondo wake itakuwa hatari zaidi.

    ReplyDelete
  5. Hii dunia tunapita njia, tupendane kama dugu moja, Unguja mnatakiwa kuiga upendo waliona Wabara kwa Wauguja,sijawahi kusikia Nyumba, bar, kanisa, au banda la raia kutoka Unguja limechomwa huku bara, hii inaonyesha upendo tulionao kama dugu,Wabara wameshawavumilia muda mrefu na kimya kingi kina kishindo chake. hivyo nashsuri wote walio husika wachukuliwe hatua stahili, ili iwe fundisho kwa wengine.

    ReplyDelete
  6. Sie wote ni ndugu, bala na visiwani, ni damu moja. Hata baba wa taifa, Nyerere na Karume walielewa ilo ndio maana waliweka muungano. Naelewa jamaa wa Zanzibar, na bala vile vile wanapiga kelele kuhusu muungano, lakini kusema kweli tatizo si muungano ni uongozi mmbovu uliopo sasa, hawana msimamo. Kuna watu wachache au wengi, sina huakika kwa kweli,ndiyo wanafanya haya mambo ya kinyama(ujambazi) ili kutia doa undugu wetu. Na viongozi wengine wanataka kuuza mji kwa watu wa nje'. WaTanzania tunatakiwa tuwe wazi kimawazo, kwani kuona si kuelewa. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

    ReplyDelete
  7. Wananchi wa Pwani Mchangani ni Waislamu na vitendo vya hao jamaa wa Bara vya kuuza ngono hadharani ni kinyume wa utamaduni wa Waislamuna kamwe hawatokuwa tayari kuvumilia uovu huo. Nchi ni ya Wazanzibari, kwahivo wasilazimishwe kuukubali uchafu huo kwakuwa eti Wabara ndugu zao na wana uhuru wa kufanya wayatakayo. Wazanzibari wakikerwa kwa kitu, mara jamaa wa Bara wamekuwa ni mtindo wao kuwatisha Wazanzibari kuwa nao wapo Bara. Jee wanataka kuwafukuza? shuruti wafahamu kuwa Wabara wameanza kuhamia Unguja kwa wingi tokea karne zilizopita, kabla ya Wazanzibari kuhamia Zanzibar. Wakaazi wengi wa Unguja pamoja na baadhi ya viongozi ni wenye asili ya Bara, kwahivo wawache maneno ya kejeli.

    ReplyDelete