Na Pendo Mtibuche, Dodoma
WAAJILI nchini wameaswa kuacha tabia ya kuwa na mtazamo hasi juu ya vyama vya wafanyakazi na badala yake wafungue milango wazi kwa ajili ya mazungumzo.Imefahamika
kuwa migogoro mingi sehemu za kazi ambayo wakati mwingine hulazima wafanyakazi kufanya migomo na maandamano inatokana na baadhi ya waajiri kuona vyama vya wafanyakazi havina umuhimu sehemu za kazi.
Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara na Taasisi za Fedha (TUICO), Bw. Omar Ayubu wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa chama hicho.
Bw. Ayubu alisema kuwa kwa sasa ipo haja ya waajiri kuacha milango wazi kwa ajili ya mazungumzo na majadiliano na maelewano sehemu za kazi, ili kuondoa malalamiko ambayo si ya lazima kati yao na waajiriwa.
"Imefika wakati tunalazimika kufanya migomo na maandamano na tunapofanya hivyo tunawakumbusha waajiri kuwa mazungumzo hayapo, hivyo lazima yafanyike kwani mwajiri na mwajiriwa ni watu ambao wanategemeana."alisema
No comments:
Post a Comment