12 May 2011

Viwango vya FIFA vyaitia 'gundu' Tanzania

Na Addolph Bruno

KOCHA Msaidizi wa timu ya Birmingham inayoshiriki Ligi kuu Uingereza, Andy Watson amesema wachezaji nchini, wanashindwa kucheza soka la kulipwa kutokana na kukosa
viwango vya ubora wa soka vinavyotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambapo Tanzania haipo katika nafasi nzuri.

Birmingham inatarajia kuja nchini kucheza na timu za Simba Julai 7 na Julai 12, mwaka huu itacheza na mabingwa wa Tanzania Bara Yanga.

Akizungumza Dar es Salaam jana, kocha huyo alisema watahakikisha timu hiyo itakapokuja nchini itaacha historia ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa wachezaji wa Tanzania na wa nchi jirani.

Alisema ujio wa timu yake utasaidia kuwapa changamoto na kuwapa nafasi wachezaji wa Tanzania kujifunza.

"Sisi hatukuwahi kufika Afrika, tunayofuraha kupata nafasi hii, tutahakikisha ujio huu unakuwa wa kihistoria na kuacha hisia za soka la Uingereza lakini si tu soka bali kutangaza utalii," alisema Watson.

Alisema watatembelea vituo vya utalii, ambavyo watapangiwa na kuyafurahia mazuri watakayoyaona kuitangaza Tanzania nchini Uingereza, ili uhusiano huo uweze kuzaa matunda mazuri.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Rage ambao ni wanaratibu wa ziara hiyo alisema wanayofuraha kuona malengo ya kuileta timu hiyo yanaendelea vizuri.

1 comment:

  1. Good initiative... it's about time Simba to open doors for international contracts

    ReplyDelete