MANCHESTER, England
TIMU ya Manchester City kwa mara ya kwanza imefanikiwa kufuzu fainali za Klabu Bingwa Ulaya, baada ya kuifunga Tottenham bao 1-0 hivyo kupata mafanikio ya
pili katika mashindano iliyocheza msimu huu.
Ushindi huo wa usiku wa kuamkia jana, ulipatikana kwa bao pekee la kujifunga lililofungwa na Peter Crouch, ambaye pia ndiye aliyefunga bao pekee Mei mwaka jana ambalo liliipeleka Tottenham katika michuano ya Klabu Bingwa msimu huu, dhidi ya Man City.
Kwa kupata nafasi hiyo mojawapo kati ya nafasi nne nchini England, inadaiwa kuwa ni mafanikio muhimu kwa mmiliki wa timu hiyo kutoka mjini Abu Dhabi, ambaye aliinunua timu hiyo mwaka 2008.
Jumamosi wiki hii Manchester City, inakutana na Stoke City katika mechi ya fainali ya michuano ya Kombe la FA na inatazamiwa kushuka katika mchezo huo, ikiwa na dhamira ya kumaliza ukame wa miaka 35 ya kukosa ubingwa.
No comments:
Post a Comment