31 May 2011

Viwango Man United v Barcelona

BARCELONA

VICTOR VALDES: hakuwa na kazi kubwa, alifungwa bao na Wayne Rooney lakini hakuwa katika presha. Alioneshwa kadi ya njano. Alikuwa na alama 8 kati ya
10.

DANI ALVES: alicheza vizuri mno, alikuwa akipanda mbele na kumpa wakati mgumu Patrice Evra ambapo hawezi kumsahau. Alipewa kadi ya njano, alipata alama 9.

ERIC ABIDAL: Beki mweusi kutoka Ufaransa, alicheza muda mfupi baada ya kurejea uwanjani baada ya kufanyiwa operesheni ya kuondoa uvimbe katika ini.

Alikuwa shujaa wa Barca aliwadhibiti washambuliaji wa United waliokuwa wakitaka kupata chai, lanchi na chakula cha usiku kwa kupitia njia yake. Alama 10.

GERARD PIQUE: Beki mzuri zaidi wa kati! Alicheza vizuri na muda mwingi alikuwa kama mshamabuliaji namba tisa kwa kucheza mbele. Alama 9.

JAVIER MASCHERANO: Alikuwa ni beki namba tano ambaye alichukua nafasi ya Puyol ambayo hakuwa fiti sana, Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool alifanya kazi kubwa kumficha Javier Hernandez, 'Chicharito'. Alama 7.

SERGIO BUSQUETS: Nanga! alikuwa akisambaza mpira kwa Iniesta na Xavi. Ilipohitajika alikuwa akirudi katika ulinzi na kwenda mbele kushambulia. Alama 8.

XAVI: Mtaalamu. Akistaafu soka mashabiki watakosa burudani. Lakini si kwa Michael Carrick. Alimficha Giggs. Alama 10.

ANDRES INIESTA: Mtaalamu. Ni mchezaji mzuri hususan kama Xavi. Aliwapa wakati mgumu wachezaji wa United. Alama 10.

PEDRO: Mfungaji wa bao la kwanza, alimpeleka sokoni Van der Sar. Walinzi wanne wa United mawazo yao yote yalikuwa kwa Messi. Alama 9.

LIONEL MESSI - Nyota wa timu. Alicheza vizuri zaidi. Ni mwanasoka ambaye United watamwota katika historia yao. Alifunga bao la pili. Alama 10 kwa 10.

DAVID VILLA: Alicheza vizuri mno na alifunga bao zuri la tatu na kufanya kipa wa United Van der Sar kustaafu soka kwa huzuni. Alama 9.

Wachezaji wa akiba:

KEITA alichukua nafasi ya Villa dk. 85. Alama 5.

PUYOL alichukua nafasi ya Alves dk. 88. Alama 5.

AFELLAY  alichukua nafasi ya Pedro 90. Aliingia kusherekea. Alama 5.


MANCHESTER UNITED

EDWIN VAN DER SAR: Kipa huyo wa kiholanzi hakutaka mambo yawe yalivyokuwa. Alifungwa  bao la kwanza na Pedro alifungwa bao la pili kwa shuti jepesi na Messi. Kati ya alama 10 alipata 5.

FABIO: Ni mmoja kati ya wachezaji wa United wachache aliyeonekana kutulia na mpira na kupeleka mbele. Alama 6.

RIO FERDINAND: Pamoja na kufungwa ukweli ni kwamba hakucheza vibaya sana katika sehemu ya moyo wa ulinzi kwa United. Alama 6.

NEMANJA VIDIC: Alicheza rafu lakini hakuweza kumudu kasi ya wachezaji wa Barca pamoja na pasi zao. Alama 6.

PATRICE EVRA: Ilikuwa ni mechi mbaya zaidi kwa mchezaji huyo wa Kifaransa akiwa na United. Alichangia kufungwa goli la kwanza. Alama 4.

ANTONIO VALENCIA: Amerejea United mwishoni mwa msimu baada ya kuwa majeruhi, lakini alipotea Wembley. Alioneshwa kadi ya njano. Alama 5.

MICHAEL CARRICK: Alicheza vizuri kipindi cha pili lakini alipotea katika mchezo huo. Alipata kadi ya njano. Alama 5.

RYAN GIGGS: Babuuu! akiwa na Rooney mbele walijaribu kutafuta magoli si kama wachezaji wenzao. Alama 6.

JI-SUNG PARK: Alitarajiwa kutumika kutengeneza nafasi kuiangamiza Barca, lakini alishindwa. Alama 5.

WAYNE ROONEY: Alifunga bao pekee la United kwa nafasi aliyopata, lilikuwa goli zuri. Alama 7.

JAVIER HERNANDEZ: Chicharitooo! Alifichwa. Hakuweza kupatiwa pasi na wachezaji wenzake. Alama 5.

Wachezaji wa akiba:

NANI aliiingia badala ya Fabio dk. 69. mchezo ulikuwa umekwenda wakati anaingia. Alama 5.

SCHOLES alichukua nafasi ya Carrick dk 77. Inaweza kuwa mechi yake ya mwisho, amemaliza vibaya. Alama 5.

No comments:

Post a Comment