Na Elizabeth Mayemba
MECHI ya mchujo ya kuwaniwa kucheza fainali za Mataifa ya Afrika 'All Africa Games' kwa vijana wenye miaka chini 23, kati ya Tanzania na Uganda (The Kobs), lililochezwa
Aprili 30, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, limeingiza sh. 32,982,000.
Katika mechi hiyo, Vijana Stars iliondolewa baada ya ugenini kufungwa 2-1, na mechi ya marudiano mabao 3-1, hivyo kuaga kwa jumla ya mabao 5-2.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema mapato hayo yametokana na watazamaji 24,078 walionunua tiketi, ambapo watazamaji 22,117 walilipa sh. 1,000, watazamani 1,749 walilipa sh. 5,000 na 212 walilipa sh. 10,000.
"Watu walioingia uwanjani hawakuwa wengi sana, na hayo ndiyo mapato yaliyopatikana," alisema Wambura.
Katika hatua nyingine, uchaguzi wa klabu ya Villa Squad umepangwa kufanyika kati ya Juni 2 na Juni 20, mwaka huu.
Wambura alisema Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewasiliana na Kamati ya Uchaguzi ya Villa Squad na kuitaka kupanga tarehe ya uchaguzi inayokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi.
Alisema Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya Villa, atawatangazia wanachama wa Villa tarehe ya uchaguzi inayokidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi, baada ya kupata maelekezo ya mchakato wa uchaguzi yaliyotumwa kwake jana.
Msemaji huyo alisema, tarehe ya Uchaguzi wa Villa haitakuwa Mei 22, mwaka huu, kama ilivyotangazwa jana, na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Villa Squad.
SAWA HIYO NI TIMU YA TAIFA YA VIJANA BASI HAKUNA MCHANGANUO WA MGAO WA HAYO MAPATO?
ReplyDeleteAU NDIO GHARAMA ZA KAMBI,USAFIRI,WAAMUZI NA USAFIRI HATA VIFUTA JASHO KWA VIJANA HAKUNA? WEKENI WAZI BASI TUJUWE HATA KWA MSHANGAO!!