Na Amina Athumani
RAIS wa Zanziba, Ali Mohamed Shein, leo atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kufunga mashindano ya netiboli kwa nchi za Afrika Mashariki yanayofanyika kisiwani
Zanzibar.
Mashindano hayo yalianza Aprili 29, mwaka huu, kwa kushirikisha timu 17 kutoka Kenya, Uganda, Tanzania Bara, Zanzibar na Zambia, ambayo ilialikwa.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa visiwani Zanzibar, Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA), Rahma Bakari, alisema ufungaji wa mashindano hayo utafanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar, na kwa kwamba, Rais amethibitisha kushiriki.
"Mashindano yanaendelea vizuri na leo tunahitimisha kwa michezo ya fainali, Rais Shein, amekubali kuwa mgeni rasmi," alisema.
Alisema fainali za mashindano hayo kwa upande wa wanaume zitawakutanoisha mabingwa watetezi Prison ya Kenya dhidi ya Polisi Zanzibar, ambao ni mabingwa wa mwaka juzi.
Kwa upande wa wanawake, mshindi wa jana jioni kati ya Jeshi Stars na bingwa mtetezi, AIC ya Uganda dhidi ya JKT Mbweni ya Bara na Prison ya Uganda.
Rahma alisema kwa upande wa wanawake, Zanzibar ilishindwa kutinga hatua ya nusu fainali, baada ya kuzidiwa mabao na JKT ya Bara.
Alisema kwa sasa, Zanzibar imehamishia mawazo yake katika timu ya wanaume, Polisi Zanzibar, itakayokuwa ikijaribu kuwavua ubingwa Prison ya Kenya, leo.
No comments:
Post a Comment