Na Rabia Bakari
CHAMA cha UPDP kimekitupia shutuma Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kudai kuwa kelele zinazopigwa na chama hicho kupinga serikali ya
Rais Jakaya Kikwete, lakini kimekuwa kikipenyeza maombi ya siri ya kusaidiwa ili kujipanua.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya Bakhresa Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa UPDP, Bw. Fahmi Dovutwa alisema kuwa CHADEMA wamekuwa wakisimama na kumpinga Rais Kikwete, ambapo wamefikia hatua ya kuomba asifike mwaka 2015,
Alisema hata hivyo wamekuwa wakifanya mawasiliano ya siri na Rais Kikwete kuomba msaada wa fedha ili kuimarisha chama mfano msaada wa elimu walioomba katika jimbo linaloongozwa na mbunge wa chama hicho.
"Maombi hayo yamefanya na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Zitto Kabwe kwa niaba ya chama chake, bila shaka ameambiwa na Katibu Mkuu Bw. Wilbrod Slaa mbaye naye ameelekezwa na sekretarieti. CHADEMA hawakuishia hapo tu kwa Rais Kikwete bali wametembeza bakuli hata kwa wanaowatuhumu kuwa ni
mafisadi, wameomba na wamepewa watu hawa wanatuchezea shere,"alisema Bw. Dovutwa.
Alisema kuwa kwa matusi na kebehi zinazofanywa na CHADEMA dhidi ya Rais Kikwete bila aibu mchana, lakini ajabu wamekuwa wakizungumza na CCM usiku, na kufika mbali zaidi kwamba kwa kitendo hicho ni cha kisaliti na kama kweli CHADEMA kungekuwa na waadilifu, Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Freeman Mbowe na Dkt. Slaa wangejiengua.
Aliionya CHADEMA kujifunza kupitia chama cha FORD cha nchini Kenya, ambacho kiligawanyika baada ya kiongozi wa kutokea magazetini asubuhi Ikulu na aliyekuwa Rais wa Kenya Bw. Daniel Moi, na kuonya viongozi hao kuacha usaliti kwa wafuasi wao.
Bw. Dovutwa alitoa jukumu la amani na utulivu wa nchi kuwa mikononi mwa waandishi wa habari, na kuepuka uchochezi wa CHADEMA ambao mnamo miaka ya hamsini, vita vingi vilivyopiganwa vimetokana na mikono ya waandishi wa habari.
Dovutwa umefilisika huna sera, nilifikiri ungemsifu rais Kikwete kwa kusaidia wananchi kwa elimu bora, na kuipongeza CHADEMA japo ni wapinzani lakini wanaona tija ya wananchi kupata kile kilicho bora 'Maisha Bora kwa Kila Mtanzania' Kwa mtazamo wangu, ingekuwa chama pinzani kinaomba msaada kwa ajili ya kununua FUSO ungesema wanalengo la kujisaidia wenyewe na siyo wanachama, lakin wanachoomba ni msaada wa elimu. CHADEMA ni chama makini kwa watu makini, na kitabakia kuwa Sauti ya watu ambayo ndiyo sauti ya Mungu. Dovutwa hamia chadema kuna sera, acha kujikombakomba kwa mafisadi ambao kila kukicha wanatunyonya ili wao waendelee kutawala. Chadema.... kwa maendeleo ya taifa...
ReplyDeleteMimi nadhani siasa itakuwa imemshinda kwani hatutegemei kuona kiongozi anapinga maendeleo kwa wananchi wake . Ina maana yeye angekuwa rais serikali yake ingependelea maeneo ambayo chama chake kimeshinda tu. Namshauri kama amekosa yakuongea ni bora akae kimya tu hakuna atakayemwuliza ila asiendelee kukipinga CHADEMA kwani kipo kwa ajili ya watu na sio kwa ajili ya chama tuu.
ReplyDeleteDovutwa ni nani?mbona mimi simfahamu?mimi nadhani tuispoteze muda kumjadili mtu ambaye hana umuhimu kwenye siasa za Tanzania,he is just boot leaker,anatafuta umaarufu kuptia mgongo wa chadema,kama sikosei si ni yule mgombea anayevaa uniforms za night support security company?
ReplyDeleteSikujua kuwa UPDP nacho ni chama cha siasa,hivi uwa bado kipo?chama gani hakina hata mwenyekiti wa mtaa Tanzania nzima achilia mbali diwani au mbunge,nadhani anatumiwa,sio makosa yake.
ReplyDeleteDovutwa is another HIOPELESS CHAP in this country. hivi huyu Dovutwa inakuwaje hadi anaweza kusimamishwa kuwa mgombea uraisi? CCM haya yote yatawatokea puani.waharibifu wakubwa wa mfumo
ReplyDeleteDovutwa hajafislisika kama ambavyo mcgangiaji mmoja amesema kwani anayefilisika ni mtu ambaye aliwahi kuwa na kitu fulani sasa hana, Dovutwa hajawahi kuwa na lolote hivyo hawezi kupewa hadhi ya kufilisika. Huyo ni mchovu wa kisiasa tu.
ReplyDeleteMwanzoni nilidhani ni Uganda People's Democratic Party "UPDP" Kumbe ni ya Tanzania?. Sawa mzee Dovutwa Fahmi Dovutwa! Umesafisha nyota mwayego!!!
ReplyDeleteNdoo maana aliugua tumbo la kuharisha akjiondoa kwenye uchaguzi,nadhani tuweke kipengele cha kupitia milembe kabla ya kujaza form ya kugombea urais kwenye katiba mpya,dovutwa si mzima tutakuja kumpa nchi kichaa cku moja
ReplyDeleteCHADEMA ni chama makini kwa watu makini, na kitabakia kuwa Sauti ya watu ambayo ndiyo sauti ya Mungu. KOTE INAWEZEKANA UMESEMA SAHIHI ILA KIPENGELE HICHO KINANITIA MASHAKA UNALENGA NINI ?
ReplyDeleteBaada ya kusoma maneno yenu ni kua naona ni chuki tu maana kama kiongozi wa chama chake na anaona mambo yanayofanyika kinyume na kusema vipi mtamshutumu?? naona woe nyinyi mna chuki binafsi na chadema mnayoidhania kua ni chama cha wote walala hoi au ni kwa manufaa ya umaa ni uongo kwani huyo Freeman Mbowe ni kama dicteta tu hataki mtu awe na wadhifa kama wake kabisa japo sio yeye aloanzisha chama anachojua ni kupata pesa na kuendeleza miradi aloachiwa na baba yake anawafanya watu wajinga wapo wanamuamini lakini ni wale wasomjua wanaomjua wanajua toka afanye kazi bank miaka ya 80 na wizi alioufanya na pia ni muuzaji mkubwa wa madawa ya kulevya na haya ni wachache wayajuayo atawadanganya nyinyi msomjua lakini watu wengi kama yeye atakazania kua rais wa chama chake hawatojiunga kamwe kweli anawadanganya watu wasomjua , mimi sipo chama chochote lakini chadema ni uoza mtupu kuliko ccm bora cha mrema mara mia
ReplyDeleteMatatizo ya watanzania ni kuwa na majibu rahisi kwa maswali magumu.Haya hata Nyerere alituasa sana.Kila mtu ana uhuru wa kusema na kusikilizwa.Kwani kina Mbowe kwenye ulingo wa siasa walitokea wapi?si kwenye majukwaa haya haya!tuchambue mambo----ushabiki si tija.Kila Chadema ikiguswa si sawa----vyama vingine sawa---ajabu kweli!!!!!!!
ReplyDeleteMimi naona huyu wala siyo mwanasiasa, ni sawa na mwanamke mpiga majungu, hata aliokuwa anawahutubia wanafanana naye! tunasema waafrika wengi ni watumwa ktk nchi zao lakini wanajiona kama watu huru! huyu ni mgonjwa hata kufikiri, anahiyaji tiba na shule ya bure
ReplyDeleteDovutwa yupo sawa na ndio hata mmoja yule Mheshimiwa mmoja ambaye amepata wapiga kura kwa sababu ya kipaji chake cha kurap wa pale Mbeya Mjini aliropoka mbele ya wapiga kura wake kuwa wampige mawe Mkuu wa nchi na ndipo Mheshimiwa Mbowe akaona huyu kijana anataka atukosanishe na Muheshimwa Rais akaamua kumkana yule mwana hiphop hadharani hii ni kuonesha hawa Chadema ni magumashi wakubwa na nikweli kuwa huwa wanapata msaada kutoka kwa Mkuu wa Nchi, mimi sina chama chochote lakini nimejaribu kufuatilia sera na mienendo ya vyama vyote nimeona wote ni watafuta maslahi tu.
ReplyDeletewatu hawa dizaini ya akina Dovutwa wanapoteza muda tu, na nafasi gazetini. msiwe mnawaweka, wanachafua hewa tu
ReplyDeleteDovutwa ukiliangalia hata jina lake na jinsi alivyowatelekeza wafuasi wake saa ya mwisho na jinsi alivyosababisha hasara kwa mpicha wake mbovu kuwepo kwenye karatasi za kura wakati akijua hagombei ni msaliti kwa umma. Anatumia system ya "Kama huwezi kumshinda, jiunge naye". Hana issue!
ReplyDeletekaka anonymous leo umewakalia watu shingoni hata wasitoe mawazo yao?ni kweli dovutwa hakuwa na mtaji hivyo hawezi kupewa hadhi ya mufilisi,lkn pia hata chadema nao ni nguvu ya soda tu kwn huwezi fuga mbwa kwa kutegemea jirani, nao wakipata 20 bl watapiga tu kelele mpk ziishe kwa hiyo we tulia tu.
ReplyDelete