*Dkt. Bilal mgeni rasmi
Na Mwali Ibrahim
MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Khalib Mohamed Bilali leo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika sherehe za utoaji tuzo kwa
wanamichezo bora wa mwaka 2010 zinazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) katika Hotel ya Movenpick, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto alisema sherehe hizo ambazo zimedhaminiwa na Kampuni ya Bia ya serengeti (SBL), zitaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV.
Pinto alisema maandalizi yamekamilika, ambapo utoaji wa tuzo hizo utasindikizwa na kundi la THT na Wanne Star.
Alisema tuzo hizo zinavipengele 17 ambavyo vitahusisha michezo ya riadha, wavu, netiboli, karate, kikapu, soka, judo, ngumi za kulipwa, ngumi za ridhaa na wanamichezo chipukizi na pia kutakuwa na tuzo ya heshima.
Aliwataja wanamichezo wanaowania tuzo hizo kuwa ni Samson Ramadhan, Marco Joseph, John Bazil, Zakia Mrisho, Mary Naali na Magdalena Mushi ambao wanashindania riadha.
Wengine ni Khamis Mcha, Mrisho Ngassa, Shadrack Nsajigwa, Juma Kaseja, Asha Rashid, Mwanahamis Omari na Fatuma Omari ambao wanacheza soka.
Wanaocheza ngumi za ridhaa ni Revocatus Shomari, Selemani Kidunda na Said Dume wakati ngumi za kulipwa ni Karama Nyilawila, Mbwana Matumla na Francis Cheka.
Pia kutakuwa na tuzo za wanamichezo wanaocheza nje ya nchi michezo mbalimbali ambao ni Hasheem Thabit, Henry Joseph, Rogers Mtagwa na Nizar Khalfan.
Tuzo nyingine itakwenda kwa wachezaji wa nje ya nchi wanaochezea nchini ambao ni Emmanuel Okwi wa Simba, Yaw Berko wa Yanga na mwanakickboxing Kanda Kabongo.
Alisema, kila mchezo umetoa wanamichezo watatu ambao, atateuliwa mmoja kulingana na alivyofanya vizuri katika mashindano mbalimbali na ataingia katika tuzo ya jumla ya mwanamichezo bora wa mwaka.
No comments:
Post a Comment