Na Peter Mwenda
ALIYEWAHI kuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kibaha kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Habibu Mchange ametangaza kuwania
nafasi ya Uenyekiti wa Baraza la Vijana wa chama hicho (BAVICHA).
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Bw. Mchange alisema anagombea nafasi hiyo kwa sababu uzoefu alionao katika chama ngazi ya taifa anaamini atajenga BAVICHA kukilinda chama hicho ili kushinda uchaguzi ujao na kuandaa viongozi wa baadaye wa chama.
"Matatizo yanayoikabili nchi yanaathiri sana vijana ambao mimi nataka kuwatumikia kama vile kupanda kwa gharama za maisha, bei ya umeme, kushuka kwa kiwango cha elimu, kuongezeka kwa kashfa za ufisadi, ukosefu wa ajira kwa vijana," alisema Mchange.
Alisema kumekuwa na matatizo mengi nchini ya utoaji wa ajira kwa upendeleo, kuporomoka kwa huduma bora za afya ni dhahiri kuwa Serikali na chama tawala kimeshindwa kuwatumikia wananchi wake hivyo dawa yake pekee ni kuunganisha akiwa mwenyekiti wa BAVICHA.
Bw. Mchange ambaye mbali ya kuwa mwanaharakati na mwanasiasa, ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) akisomea fani ya Sayansi ya Siasa na Utawala alisema anataka kuona vijana wa Chadema wanakuwa nguvu ya mabadiliko na kutoa ushauri wa kitaalamu.
Alisema anajivunia mafunzo na malezi ya kisiasa aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa kitaifa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti, Bw. Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Bw. Willibrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe.
Alisema uwezo na uzoefu huo ndani ya CHADEMA utamsaidia kukitendea haki chama na watanzania wapate fursa ya kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wote ili kila mmoja afaidike kupitia kwa kijana wenye uchungu kama wake yeye.
Bw. Mchange alisema mafanikio aliyowahi kuyapata wakati alipogombea Ubunge Kibaha na kupata kura 10,450 kati ya 26,574 zilizopigwa na mpinzani wake kushinda kupata kura 14,028 anaamini kuwa ilikuwa dalili za wananchi kuona kuwa anao uwezo wa kufanya kazi ya kutumikia wananchi bila kutetereka.
sasa nyie chadema ndio mtatufanyia nn ss vijana mnatakumdanganya nani?acheni mambo yenu ya uongo kuwadanganya watu na akili zao wajanja mbinu zenu tumezijua
ReplyDeleteumeorodhesha matatizo mengi yanayowakabiri vijana ila ukueleza utafany nini ili tuyatatua hayo matatizo.au kwako wewe ukiwa kiongozi tu inatosha. matatizo yataisha yenyewe? tuache ujanja ujanja. tuseme tatizo na njia ya kulitatua ili tukubari kuwa kweli unauwezo huo. maana kujua tatizo ni jambo moja na kujua jinsi ya kulitatua jambo jingine.lazima mnaotaka uongozi mtueleze jinsi gani mtakavyoweza kutuongoza katika kutatua matatizo tuliyonayo watanzania ili tuchague mwenye njia sahihi ya kuyatatua hayo matatizo. kujua kama tuna matatizo kila mtu anajua ila njia ya kuyatatua hayo matatizo ndiyo tunayoitaka ili tuchague njia sahihi na salama.
ReplyDeleteNyinyi chadema ni waongo na sera zenu hizo.Nyinyi wenyewe mnafuata maslahi,halafu mnatuzuga ati mtatekeleza maslahi ya vijana.Halafu kitu kingine mnatuboa ni kuanzisha maandamano yasiyo na msingi. Wanaumia wengine,wanafaidi wengine. "CHAMA CHA MAANDAMANO"
ReplyDeleteHaya Bw. Habibu tutaona mwisho wako una kasoro nyingi ambazo hazitakiwi na chama hicho,ukipita itakuwa maajabu panya kupita kwenye tundu la sindano
ReplyDelete