*Apigwa marufuku kufika mgodini Noth Mara
*Aeleza masaibu yaliyompata akiwa gerezani
Na Hellen Magabe,Tarime
MAHAKAMA ya Wilaya ya Tarime imwaachia kwa dhamana wanachama wanane wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo
Mbunge wa Singida Mashariki pamoja na aliyewahi kugombea ubunge Jimbo la Tarime, Bw. Mwita Mwikwabe kwa masharti ya kutofika katika Mgodi wa North Mara hadi watakaporuhusiwa.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Bw. Yusto Luboroga Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Bw. Casmil Kria alisema Bw. Lissu na wenzake wamepata dhamana kwa masharti yakutoonekana eneo la mgodi huo hadi watakaporuhusiwa kwa madai kuwa wanaweza kusababisha uchochezi kwa ndugu wa wafiwa. Kesi yao itatajwa tena Juni 27, mwaka huu.
Bw. Lissu ambaye ni mwanasheria wa CHADEMA na wenzake wanashtakiwa kwa makosa matatu ya kuzuia shughuli za hospitali kufanyika, kukaa katika eneo la mochari bila kibali pamoja na kusababisha mkusanyiko usio halali, na kuwazuia ndugu kuchukua miili ya ndugu zao.
Akizungumuza baada ya kutoroka katika Gereza la Komaswa Bw Lissu alisema kuwa akiwa na wenzakea saba walifanyiwa vitendo vya kinyama na Jeshi la Polisi hata. Hivyo alisema kuwa hajutii kuingia gerezani kwania kwa asingejua mateaso wanyoyapata Watanzania katika gereza hilo.
Bw. Lissu alisema alipelekwa katika gereza hilo akiwa amekanyagwa na askari watatu shingoni, ubavuni na mgongoni bila kuonewa huruma lakini alivumila mateso hayo.
"Tuliwekwa kama samaki nikakanyangwa kama nilivyo waeleza na hii nguo walinichania wakati tayari nikiwa nimepanda katika gari mnaweza kuona ilivyochafuka ilikuwa nzima wakasema chaneni hilo kombati lake na kweli likachanwa," alisema Bw. Lissu
Alisema ingawa wamefanyiwa udhalilishaji huo lazima atawaeleza Watanzania yote yanayofanywa na Jeshi la Polisi kwa raia wasio na hatia kwa kuwabambikia kesi.
Alishangazwa kuona kesi nyingi ni za kuwambikia na kusema kuwa kanda maalumu ni mwavuri wa kulida uovu hasa katika mgodi.
Alisema alibaini kuwa kesi hizo ni za kubambikiwa baada ya kuzungumza na mahabusu aliokuwa nao usiku kucha na kugundua matatizo ya rushwa na unyanyasaji ni ya hali ya juu.
Alisema kuwa anaamini kuwa hakuna gereza lolote nchini linalofanya mambo kama hayo hivyo kuahidi kushughulikia kesi zaidi ya 300 za kubabikiziwa kesi za mauaji mpaka zinakwisha.
Alifafanua kuwa endapo waliohusika na tuhuma hiyo wangekuwa na busara wangejiuzuru akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Khamisi Kagasheki kwa kauli aliyoitoa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ambayo ilionesha kuunga mkono mauaji hayo ya Wakazi wa Nyamongo.
Naye aliyewahi kwa mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho, Bw. Mwita Mwikwabe alisema walitawanywa kila mtu katika kituo chake ambapo alishuhudia mateso mkubwa wanayopata Watanzania wawapo katika vituo hivyo.
Alisema akiwa katika gereza la Sirali alishuhudia mtoto mwenye umri wa miaka 12 ambaye ana kesi ya mada akiwa amechanganywa na watu wazima.
Bw. Waitara kitendo hicho ni chuo cha muda mfupi na hawajasikitishwa na vipigo wala manyanyaso waliyoyapata bali wameshiriki mateso na mahabusu wanaoshikiliwa bila hatia.Alisema kuwa katika gereza hilo lenye watu zaidi ya 660 zaidi ya 3,000 wakesi za mada ambazo ni za kubambikiza
Hata hivyo mwanaharakati za haki za binadamu kutoka chama cha wanasheria ambaye alikubwa na dhoruba hilo Bw. Stanslaus Nyembea alisema kuwa inawezekana Gereza la Tarime likaongoza kwa mateso ambayo pengine yalifanyika kwenye kipindi cha utumwa pekee.
Alisema kuwa kuna udhalilishaji wa hali ya juu kwani unapofika gerezani unavuliwa nguo zote na kufanyiwa unyama ambapo alisema wengine huvuliwa nguo mlangoni lakini wao walivulia nyuma ya mlango kwa kupewa heshima
Alisema kuwa alishangaa kuona mtu anavuliwa nguo na kukaguliwa sehemu ambazo hakutegemea na nguo zake hutupwa kwa polisi aliye ndani ya gereza na kuuliza nguo hizo ni mali ya nani hivyo mwenye nazo hunyanyuka na kuifuata akiwa mtupu.
Bw. Lissu na wenzake saba walikamatwa wakiwa hosptalini kuangalia usalama wa miili ya watu waliouawa na polisi katika Mgodi wa North kwa madai ya kuwa walivamia mgodi baada ya kupata tetesi kuwa miili hiyo itachukuliwa na Jeshi la Polisi.
Wakiwa hosptalini hapo ghafla polisi walifika na garia tatu aina ya Land Rover Defender na kuzima umeme hosptalini hapo na kutumia gari moja kama taa na kuwakamata na kuwapiga na baadae kupora miili hiyo kama ilivyokuwa imekisiwa na baadae kwenda kuitelekeza mstuni.
Hiyo ndio nchi yetu ambayo dr mmoja wa saikolrojia alisema kwa nini WATANZANIA WANA JAZBA ndio hiyo
ReplyDeleteUkiwa mpinzani TZ ni lazima ukubali ya MANDELA wa AFRIKA KUSINI,POLENI na lazima kuyaongelea bungeni
Tatizo tulilonalo sisi waTZ ni kutokumjali mwenzako kila mtu aliyeoko gerezani ni jambazi tujue kila mtu anaweza kuingia gerezani.
Magereza yaye na huduma zote za binadamu WABUNGE TETEENI TUTAANZA KUWAPELEKA kama MISRI WANAVYOMSITAKI rais wao
kaka Lisu umeonyesha practical leadership kwa kuonyesha mfano kwa kukubali kwenda jela kwa ajili ya kutetea wanyonge that is true leadership badala ya kukaa nyumbani na kula good time na familia yako huko unapigania haki ya wanyonge wanaouwawa ndani ya nchi yao kama wavamizi. Muendelee na moyo huohuo watanzania wanawaona na wanawapima kama kweli mko tayari kupigania haki za wanyonge na mnaonekana kuwa mtafaulu huo mtihani.
ReplyDeleteWananchi tuwe makini sio kulaumu kila kitu au kuvalia njuga mambo bila kuyafanyia upembuzi yakinifu, na kujiona kila kitu ni haki yako mwishowe ni majuto na mateso. Watu wengi wanaiga mambo au kutumia nguvu wakati Nchi ina sheria zake na utaratibu wake wa kupeleka malalamiko na hasa siku hizi kuna Taasisi nyingi zinazotetea haki za Raia na mali zao kwanini tusifate hizo taratibu mpk tuharibu ndio watokee watu kujifanya kimbelemble front?LHRC na wenzake NGO 50 ziko ktk umoja kwa ajili ya kutetea wananchi tuamke. Kuna pumba aina nyingi kwa viongozi uchwara hawa walichosomea ni jazba zisizo na tija kwao na kwa raia,zaidi ya kuongeza matatizo na chuki tuwe makini sana.Tunataka tuwe kama NATO kuwasaidia waasi hatufiki
ReplyDeleteMimi ni yule yule Hafidh mwanaharakati kutoka Visiwa vya Zanzbar.Kwanza natoa pole kwa ndugu na jamaa wote waliopoteza ndugu zao kwa kuuawa.
ReplyDeleteMimi napenda nimjibu kijana hapo juu inaonyesha ni mwana wa CCM damu na haya ni mawazo mgando wa walio wengi kutoka CCM, maana nilipitia habari kutoka vyanzo vya habari vya leo kua Mama Spika nae anatoa kauli kama hii kua wabunge waliopata maswahiba hayo wameyataka wenyewe !! maana hawajui mipaka yao !! dahhh ama kweli mwisho wa maji ni tope , huu ni msemo unaotumiwa sana Zanzibar.mm napenda nimhoji mama Spika tu hajui kwamba Mh. Tundu Lissu ni Mbunge na Waziri kivuli wa Sheria na Katiba ? sasa Mama umeona wapi waziri (Kivuli) akawa na mipaka ?! ikiwa ataona sehem ya Tanzania kuna mahala pana tetesi ya uvunjifu wa sheria za nchi kwa nini asiende kufatilia na kujua mwenyewe ukweli ? Mama naona kama unalikoroga sasa !!kama hiyo haitoshi ukiachana na Ubunge yule ni mwanasheria wa Chadema ambacho ni chama cha kisiasa Tanzania sasa kuna tatizo gani kama chama cha kisiasa kufatilia jambo na kumtuma mtu wake wanaemuamini kwenye sehemu ambayo wanayohisi ina mashaka !! au pia vyama vina mipaka ?!! mama hebu tuweke wazi mana naona akili zinatuzunguka kwa comments zako.
Anonymous said...
ReplyDeleteKama wewe si mpuuzi kiambie chama chako CCM kitoe tamko la kuwapongeza polisi wake kukatisha roho za watu bila kuwapeleka mahakamani. CCM itakuwa imetoa ruhusa watu kijichukulia sheria mikono.
Nalipongeza sana Jeshi letu la POLISI kwa kazi nzuri saffffi waliyoifanya huko nyamongo, kwakweli Polisi hawakuwafuata hao Raia isipokuwa Raia ndio wavamizi kwa kushawishiwa na Viongozi wa CHADEMA. Mchezo huo mchafu wa Chadema Umegarimu maisha ya Watu, sasa wanajidai wapo Mstari wa Mbele kutetea Uovu wao na wananchi tusiojua kuwa tunaingizwa kwenye mtego ili Chadema wapate pakusemea tunaenda kichwa kichwa msipoangalia watawamaliza na Bado hawataongoza nchi hii. Mbona hawaji Kahama au Nzega kushawishi huko Tarime ndiko wameona Mambumbumbu wa kutaka utajiri wa harakaharaka. Nawewe Tundu Lisu kweli ni Mtundu toka Singida Mapaka huko Nyamongo, Chadema wamekufunga Paka Kengele sasa unaona Mtaji wake? Mbona Ulienda na Mabere Marando yeye anakula kuku wewe unaumia mbavu yeye kwao huku tena na yeye ni mtu wa Kenya hana uchuingu na Nchi hii, kakuacha huko yeye kateleza anakucheka kiaina amepoa zake Dsm kimya. Huko mnakotaka kutupeleka Chadema Tumekwishjua. TUTAILINDA NA KUTETEA AMANI NA UTULIVU WA NCHI YETU. Kidumu Chama Cha MAPINDUZI.
hongera kaka Tundu Lissu....jina lako liko juu katuika historia ya tanzania
ReplyDeleteHatujawa mbali na yaliyokuwa yakifanyika waAfrika ya Kusini. Mauaji ya raia wasio na hatia! eti ni kuulinda utawala. Udhalimu una mwisho wake.
ReplyDeleteNani aliikomboa nchi yake kutokana na udhalimu bila yeye kuteseka? Fikiria Jomo Kenyatta alivyoteseka gerezani kabla ya uhuru wa Kenya. Fikiria Mandela alivyosota gerezani. Ndiyo gharama ya ukombozi. Ila malipo yake yapo baadaye. Viongozi mnaoipenda nchi yetu msiogope mateso. Ndiyo njia ya ushindi. Polisi wao hungata kama mbwa wanapopewa amri ya 'muume huyo'.
ReplyDeleteNyerere alisema mtu akisema anachukia rushwa mwaangalie usoni,huyu kweli?Hakika ndugu Lissu mumeonyesha kwa ukweli mnachukia uchafu unaofanywa na serikali ya CCM hadi kufikia hatua ya kuingia mahabusu.
ReplyDeleteTunawashukuru saana kwa kupigania mapinduzi yenye tija kwa watanzania.
MHESHIMIWA SANA JAKAYA MRISHO KIKWETE, HIVI KWELI KWA MAUAJI HAYA HUSEMI NENO? HAYA BWANA WEWE ENDELEA KULA KUKU IKULU, ILA NINAAMINI KUWA ULITAKIWA USEME NENO AIDHA KULAANI AU KUPONGEZA.
ReplyDeleteKWELI NCHI HII SIJUI INAKWENDA WAPI POLENI WATU WA TARIME IPO SIKU UKOMBOZI UTAFIKA
ReplyDeleteHali ya Tarime imetokea kuwa ya unyanyasaji zaidi baada ya wanayoita kanda maalumu kuanza kazi yake tangia mwaka jana 2010 mwezi wa saba, na kibaya zaidi na cha mauthi ni pale polisi inapotumia ubabe kuwa wao ni polisi na wana silaha ili kuwanyanganya raia mali zao na kuwabambikizia vyesi kama utakataa kuwapatia rushwa,jambo jingine la mauthi ni pale walipoweka kizuizi kirumi ili kujipatia pesa kwa nguvu kutoka kwa wenye magari ukikataa kuwapa pesa watakuzuia hapo zaidi ya masaa sita hadi kumi kwa makusudi kuwa gari yako inamakosa, kama hali hii itaendelea hivi iko siku moja tutakufa wengi ili watakaobaki waishi kwa amani bila manyanyaso
ReplyDelete