16 May 2011

Suarez, Forlan waitwa Uruguay

 MONTEVIDEO, Uruguay

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Luis Suarez na mshambuliaji wa timu ya  Atletico Madrid, Diego Forlan ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha Uruguay
kitakachocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani iliyopangwa kufanyika Mei 29 mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Copa America.

Wachezaji hao wanaungana na nyota wa timu ya  Napoli, Edinson Cavani katika kikosi hicho cha wachezaji 23 waliotangazwa juzi na ambao waliisaidia Uruguay kumaliza michuano ya fainali za Kombe la Dunia ikiwa katika nafasi ya nne.

Mbali na wachezaji hao,kiungo wa Bologna, Gaston Ramirez ameitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi hicho wakati beki wa  Seville, Martin Caceres ameachwa kutokana na matatizo ya bega.

Baada ya kuwataja wachezai hao wanaokipiga nje ya nchi baadaye Kocha, Oscar Tabarez aliwataja  wachezaji wanaocheza soka la ndani ya nchi hiyo ili kukamilisha kikosi chake.

Michuano hiyo ya Kombe la Copa America itafanyika Julai nchini Argentina na kikosi kamili kilichotangazwa na kocha huyo ni walinda mlango Fernando Muslera (Lazio) na Juan Castillo (Colo Colo).

Mabeki ni  Diego Lugano (Fenerbahce), Diego Godin (Atletico Madrid), Andres Scotti (Colo Colo), Mauricio Victorino (Cruzeiro), Jorge Fucile (FC Porto), Maximiliano Pereira (Benfica) na  Alvaro Pereira (FC Porto).

Viungo ni  Egidio Arevalo Rios (Botafogo), Sebastian Eguren (Sporting Gijon), Diego Perez (Bologna), Walter Gargano (Napoli), Gaston Ramirez, (Bologna) na  Alvaro Gonzalez, (Lazio).

Washambuliaji ni Abel Hernandez (Palermo), Sebastian Abreu (Botafogo), Sebastian Fernandez (Malaga), Alvaro Fernandez (Seattle Sounders) na Nicolas Lodeiro (Ajax).

No comments:

Post a Comment