MWANAMUZIKI Beyonce Knowles kwa sasa yuko studio akiwatengeneza wimbo wa 72 katika studio ya Columbia.Wafanyakazi wa studio ya Columbia mjini
New York kwa sasa wanaumiza vichwa juu kuunganisha kazi iliyokwishamalizika ya kurekosi albamu yake ijayo.
Tayari kuna mkusanyiko wa vichwa vya albamu vinne, hakuna iliyoamliwa lakini albamu hiyo inatarajiwa kuwepo madukani wakati wa kiangazi.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka jijini humo kilisema: "Wafanyakazi wa lebo wamemwachia Beyonce kufanya mambo, hawataki kumwingilia wakati akitengenza albamu.
Chenzo hiyo kilisema kuwa wafanyakazi wameamua kumwachia huru mwanamuziki huyo kwa kuwa amejiandaa na anafanya kazi yake vizuri.
"Sasa tuna kazi kubwa ya kusikiliza nyimbo zote na kuamua nyimbo gani za kuweka katika albamu."
Tumepata mwelekeo mpya kwa wimbo mmoja wa Girls huku Beyonce akisema kuwa baadhi ya nyimbo zake zina vionjo tofauti.
Alisema: "Nimeanza kuvutiwa na kazi la Fela Kuti."
No comments:
Post a Comment