23 May 2011

Sitta, Mwakyembe wazidi kuandamwa

*Ole Porokwa asisitiza walishiriki kuasisi CCJ
*Adai kushiriki moja ya vikao nyumbani kwa Sitta


Na Mwandishi Wetu

KIZUNGUMKUTI cha uasisi wa Chama Cha Jamii (CCJ), kimeendelea kuwazunguka makada waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
vigogo walioko serikali, ambapo 'muasisi' mwingine amejitokeza akiweka hadharani madai yake juu ya waliohusika katika mpango huo.

Daniel Ole Porokwa, ambaye alijitambulisha kuwa ni kada wa CCM, akizungumza jana na waandishi wa habari Dar es Salaam, alikiri kuombwa kuwa mmoja mwanzilishi wa CCJ, akidai kuwa alishawishiwa kufanya hivyo baada ya kukutana mara kadhaa na Bw. Nape Nnauye, Dkt. Harrison Mwakyembe, Bw. Fred Mpendazoe na Bw. Samuel Sitta.

Alidai kuwa katika mikutano zaidi ya mitano aliyofanya akiwa na Bw. Nnauye na Dkt. Mwakyembe, wenzake hao walimweleza mpango wao wa kuanzisha chama cha siasa kuwa umelenga kuondokana na utawala wa kiimla wa CCM, kwa hoja kuwa chama hicho kilipofikia hivi sasa, hakiwezi tena kuaminiwa kukabidhiwa madaraka kuongoza dola.

Kwa madai ya Bw. Porokwa, viongozi hao aliokuwa akikutana nao katika mipango ya kuanzisha CCJ, walisema CCM haiaminiki tena machoni mwa Watanzania na kimepoteza mvuto mbele ya umma, kwa sababu kimeacha misingi yake, iliyowekwa na waasisi wake, akiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

"Nimeamua kufanya hivi (kutoa madai hayo) kwa misingi miwili mikuu. Kwanza, sisi kama viongozi ni sharti tuwaoneshe wananchi wetu na wanachama wa chama chetu njia sahihi tunayotakiwa kupita, tuamini katika hiyo njia tunayoelekea. Pili, mmoja wa msingi mkuu wa chama chetu ni kusema ukweli...uongo na fitina ni mwiko.

"Ni kweli niliwahi kuombwa kuwa mmoja wa wanachama waanzilishi wa CCJ. Nilikutana mara kadhaa na Mheshimiwa Nape Nnauye, Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe na Mheshimiwa Fred Mpendazoe.

"Aidha nilikutana mara moja na Mheshimiwa Samwel Sitta baada ya Mheshimiwa Nape na Mwakyembe kunitajia kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ, nami kutaka uthibitisho wa hicho walichonieleza. Naye Sitta alieleza kuwa nilichoelezwa na Nape na Mwakyembe hakina chembe ya mashaka," alisema Bw. Porokwa.

Aliongeza sababu nyingine ya kuamua kusema hayo ni baada ya kuwasikia Bw. Nape na Dkt. Mwakyembe wakimkana Bw. Mpendazoe, ambaye ndiye aliyeibua tuhuma hizo za vigogo wa CCM na serikali waliohusika kuanzisha CCJ, akijenga hoja kuwa itakuwa ni vigumu kwa chama hicho na serikali yake kuwatumikia wananchi;

Kama viongozi wake wamefikia hatua ya kusigana kiitikadi na kutokuwa wamoja katika masuala ya msingi ya utawala na uongozi wa nchi, kwa maslahi ya Watanzania wote.

Akijibu shutuma hizo baada ya kupigiwa simu na Majira, Bw. Sitta ambaye alisema alikuwa safarini kutoka Arusha, alijibu;

"Hivi waandishi wa habari hili suala...people can change parties let alone kuanzisha vingine...kwa hiyo amenizungumzia mimi...let us forget it, sisi tunashughulikia mambo makubwa zaidi ya hayo," alisema kisha akakata simu.

Naye Dkt. Mwakyembe alipoulizwa bila kufafanua alisema 'Muulizeni huyo Porokwa kama aliacha kugombea ubunge kwa sababu ya pesa, leo kapewa shilingi ngapi ili azungumzie suala hilo.

10 comments:

  1. Ole Parokwa amesema, inaweza kuwa kweli lakini! Lakini watanzania tujiulize Ole Parokwa anamsemea nani? Kama anasema ukweli kwa kukuwa anataka ukweli utaafanye huru basi hilo ni jema. Lakini watanzania wezangu Ole anamsemea Edward Ngoyan Lowassa! Hili linalonitilia shaka!

    ReplyDelete
  2. ole anatafuta umaarafu kaupitia migongo ya watu hana kipya!

    ReplyDelete
  3. jamaa kachemka, natafuta umaarufu lakini ni kama kipandikizi fulani hivi alikuwa wapi siku zote hizo? kina mpendazoe wapo wengi, hafai kuwa kiongozi majungu tu ndiyo anaweza. Parokwa huna jipya unatia kichefuchefu.

    ReplyDelete
  4. Na nyie waandishi wa habairi muwe munaangalia habari za kutoa magazetini hasa siku ya Jumatatu watu tukiwa na hamu ya kujua nini kinaendelea Tanzania.
    Sasa Huyu mliyemleta leo OLE PAROKWA ni nani hana hata jina, hajawahi kufanya lolote la maana hapa Tanzania mmeweka hapa, anatuchafulia ukurasa wetu. Ikiwa mtu yeyote akiongea mnaandika baadaye mtaandika takataka.
    Kazi ya Satta akiwa Bungeni wote tuliona, Kazi ya Mwakembe akiwa bungeni wote tuliona, Walifanikiwa kuangusha ukuta wa Babeli. Kumbukeni Richmond ilikuwa ikiliwa Tsh mil. 300 kila siku. hawa watu walijitoa mhanga na kuokoa Jahazi kwa ajili ya watanzani mpka leo wanawindwa.

    Sasa Huyo Ole Parokwa amewahi fanya nini katika Tanzania yetu, zaidi ya haya Majungu anayetuletea. Mbona haongelei ufisadi wa CCM, Mbona hasemi Ubovu wa Kikwete kushindwa kuongoza nchi, mpake leo Tanzani inakosa umeme.

    Binafsi Mwakyembe, Sitta kutaka kuanzisha chama kingine sioni Tatizo ni Uhuru wa kila Mtanzania, na wala hakina Madhara yoyote kwa maendeleo ya Nchi.

    Mimi naona Tatizo la msingi Ni Kikwete kuendelea Kukumbatia Mafisadi akina Lowasa Rostamu na Chenge, Kikwete kukosa muellekeo wa kuongoza nchi, haya ndo mambo ya Kuzungumzia.

    Watanzani nawaomba tushugulikie mambo ya yanayoendeshwa vibaya ili nchi iende vizuri siyo Tuchafue watu waliofanya vizuri ili eti kila mtu aonekane mbaya.

    OLE PARAKWA UNATAKIWA KUJENGA JINA KWA KUPAMBANA NA MAOVU SIYO KUJENGA JINA KWA KUCHAFUA WALIOFANYA VIZURI ILI WOTE MUONEKANE OVYO.

    ReplyDelete
  5. UKWELI SIKUZOTE HUSIMAMA PEKE YAKE HII NDIYO TABIA YAKE WACHA WATU WASEME NA WANAFIKI WABINAFSI WASALITI TUTAWAJUA KAMA KWELI AKINASITA WALIKUWA NA UCHUNGU NA TAIFA HILI MADARAKA WALIYOPEWA YASIWADANGANYE TOKENI NJE MUWASAIDIE WATZ BADO TUNAIMANI NA NYIE WACHENI WOGA NA WEKENI PEMBENI UBINAFSI PLZ WE NEED YOU FOR CHANGE!

    ReplyDelete
  6. Ninachikiona hapa ni kuwa siku zote mtu ukiwa umeajiriwa na unaona msimamo wa mwajiri wako haueleweki unaanza kuweka misingi ya baadae ikiwa utatemwa uwe na pa kujishikia,Huo ndio ukweli sasa hapa hata kama kina Sitta,Nape na Mwakyembe walishauriwa kuasisi lakini bado walikuwa hawajatemwa wala hawakuwa wasaliti walisubiri kama wangetoswa wapate kujinasua kwa CCJ,huyo mpenda dezo yeye alishajuwa kabisa kule kwake asingepita na chama kilishamtaarifu kitamtosa akawahi lakini haraka haraka haina baraka wenzake wameula sasa kebehi au fitina za nini? Mzee Sitta keshadai yeye alikuwa ni mtaji wa uraisi kwa hiyo alifuatwa na sio ccj tuu,kuna baadhi ya vyama vingine vilimfata huyo Mpendadezo si mwaminifu,simstahmilivu hana subira ana tamaa na ndio maana hata jina lake CDM lilipokatwa kinondoni, akaikmbilia segerea ktk ubunge kapigwa chini,sasa anatapata ili aweze anagalau aweze kupata posho ya kila siku kwa muda huu. CDM wakae wamwangalie sana.Nape,Mwakyembe ni wapiganaji wa kweli na hawawezi kukatishwa tamaa na watu wenye fitina na tamaa uchwara

    ReplyDelete
  7. HIVI WATU KAMA HAWA MNAWAOKOTA WAPI?MAANA AMEZUKA TU NA KUTOA SHUTUMA ZA AJABU AJABU MBONA ALIVYOKUWA KATIKA TRAIN MOJA HAKUONGEA LEO YUKO PENDING NDIO ANASEMA HAO VIGOGO WANASIMAMIA CCJ.

    HUO NI UNAFIKI MKUBWA TENA NI FUNGU LA KUKOSA BABA SITTA VITU VYAKO TULIVIONA NA TUNAVIKUBALI HAO WAZUSHI WANAKUHARIBIA TU LAKINI WATANZANIA TUKO NYUMA YAKO, HAO NI MAADUI ZAKO TU NDIO WANAKUCHAFUA USIJALI KAZA UZI PIGANA BABA NA MAFISADI,TANZANIA NI HURU HATA KAMA UNATAKA KUHAMA CHAMA NI KWASABABU YA UTENDAJI HAKI NA SI KUNG'ANG'ANIA MADARAKA KAMA WENGINE NA HAMNA WANACHOKIFANYA.

    WATANZANIA TUTABAKI MASKINI KAMA TUTASHIKILIA MISIMAMO YETU YA UBINAFSI,CHUKI,TAMAA,MAJUNGU,UFISADI NA VITU KAMA HIVYO.

    WAANDISHI PIA MUWE NA KIWANGO KULINGANA NA MAADILI YA KAZI YENU SIO KILA HABARI YA KUANDIKA BILA UCHUNGUZI WA KINA WANAPOTEZA NAFASI ZA KUANDIKA MAMBO YA MSINGI NA YA KUJENGA WATANZANIA MNAWAFUNDISHA NINI WATOTO NA KIZAZI HIKI KAMA SI KUWAPANDIKIZA CHUKI, TUSIWE KAMA JAMII YA NDUGU ZETU WA MKOA FULANI WANA MSIMAMO WA KUUWA MTU HAWARUDI NYUMA.

    ReplyDelete
  8. ole Pakacha, na Mabwana zake wa Monduli na Igunga ati wamemtuma awachafue Sitta na Mwakyembe. Porokwa hao siyo size yako. Halafu mbona umechukua tu walio na ugomvi na boss wako Lowasa, nakumbuka Nape walizinguana na Lowasa juu ya project ya jumba la umoja wa vijana, Sitta na Mwakyembe Vs Edward ndo kabisa paka na panya. Ole Porokwa huo u-monduli wenu wa kuwa mnaoganize misururu ya maandamano ya watu na magari kumupokea fisadi Lowasa kila anapoumbuliwa unataka kutuletea hadi Dar! Pambafu kabisa, kwanzania hebu tuambie ulipewa shiling ngapi kwa kazi hii ya kuongea na waandishi, usitaje ulizopewa kufuta azima yako ya kumpinga Edward huko jimboni kwenu. Nape, Sittta na Dr Mwak, kaza buti, we are before you guys. CCM kweli mafisadi wameamua kuwavuruga, wafukuzeni ndo mtakuwa salama vinginevyo Kikwete chama kitakupasukia ten times na kitafilia mbali, achana na Lowasa na Rostams, wakale hizo pesa zao na wake zao, sisi hatuwahitaji!.

    ReplyDelete
  9. WAANDISHI NI VIZURI MKAFANYIA KAZI VITU MNAVYOAMBIWA KABLA YA KUANDIKA MAGAZETINI HUYO OLE PARAKWA ANATAFUTA UMAARUFU TU.NI VIZURI AKAJENGA JINA KWA KUPAMBANA NA MAFISADI WAKUBWA WATATU HAPA NCHINI AMBAO HATA MTOTO WA SHULE YA MSINGI UKIMUULIZA ATAWATAJA ATAJENGA JINA KULIKO KUFANYA MAMBO YA KIPUUZI NA YA KITOTO KAMA ANAYOFANYA.

    ALEX JOHN. DODOMA

    ReplyDelete
  10. Sitta na Mwakyembe ni Viongozi makini sana. Hawa Watu wakiongea wenye masikio hawasikii. Hata wakiwa bungeni walitenda mambo je hamuoni. Hawa hawana woga wowote na nina hakika hawamwogopi mtu yeyote ila Mungu tu peke yake. Wanaheshimu tu taratibu zinazoendesha nchi. La ajabu ni lipi wakianzisha vyama, ni haki yao. kwani kutoka CCM ni ajabu au dhambi? Nchi yetu ilikuwa ya chama kimoja na kilikuwa ni CCM. Kwa mfumo wa vyama vingi kuanza ni lazima watu watoke CCM vianze vyama vingine na ndivyo ilivofanyika na itaendelea kufanyika hivyo. na hata watatoka vyama vingine kuanza vyama vingine au kuhamia vyama vingine. Haya Sitta kawapa kibwagizo kuwa si tu kuanzisha chama bali anaweza kuhamia chama kingine !!!!!!!!!
    Hata hivyo mwalimu alisema kuwa watakaokiuwa CCM nai CCM wenyewe !!!. "DALILI YA MVUA NI MWAWINGU" Je hatuoni hilo?

    ReplyDelete