24 May 2011

Chelsea yamtimua rasmi Ancelotti

LONDON, Uingereza

KOCHA Carlo Ancelotti, juzi ametimuliwa kazi baada ya kumaliza ligi kwa kipigo cha goli 1-0 ugenini dhidi ya Everton.Lakini inaelezwa kuwa kibarua cha
kocha huyo kilishafutwa wakati Chelsea, ilipofungwa na Manchester United katika Uwanja Old Trafford Mei 8 mwaka huu.

Katika mechi hiyo iliyokuwa ya kuamua nani atakuwa bingwa United, ilifungwa bao lake la kwanza haraka katika sekunde ya 37 kupitia kwa Javier Hernandez 'Chicharito', hadi mwisho wa mchezao ilipata mabao 2-1 na kujihakikishia ubingwa kwa mara ya 19.

Mechi hiyo iliivua rasmi ubingwa Chelsea na kuifanya imalize ligi bila ya kuwa na kombe.

Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kwa sasa anasaka kocha wake wa saba tangu alipoichukua timu hiyo ya Stamford Bridge miaka minane iliyopita.

Habari za kutimuliwa Ancelotti, zilitokea juzi baada ya kupulizwa filimbi ya mwisho katika mechi ya ugenini dhidi ya Everton.

Tangazo la kutimuliwa kwake kazi limekuja kwa haraka na haikuweza kukwepeka.Ancelotti alikuwa tayari 'amechinjwa' tangu Chelsea, ilipofungwa dhidi na United ambapo gazeti la SunSport lilitabiri siku moja kabla ya mechi iliyochezwa Old Trafford.

Kitu ambacho kimebakia kuwa siri ni kocha gani anachukua nafasi ya kocha wa kitaliano.

Guus Hiddink ana nafasi kubwa kwa kuwa ni mtu wa karibu wa Abramovich, amekuwa akifundisha timu kucheza soka nzuri, alipata mafanikio yake wakati akiwa kocha wa muda, alitwaa na ubingwa wa kombe FA 2008 baada ya kuchukua nafasi ya Luis Felipe Scolari, katikati ya msimu.

Kwa sasa ni kocha wa Uturuki, lakini bilionea ya Abramovich yanaweza kutatua tatizo hilo. Hiddink anapewa nafasi pamoja na aliyekuwa msaidizi wa kocha Jose Mourinho, Andre Villas-Boas wa Porto.

Villas-Boas alikuwa msaidizi wa Mourinho Stamford Bridge na kabla ya kujitengenezea jina mwenyewe kwa kutwaa ubinwga wa Ureno akiwa Kocha Mkuu.

Kocha wa Barcelona, Pep Guardiola naye yumo kwenye orodha ingawa amesaini mkataba mpya katika Uwanja Nou Camp.

Kocha wa zamani wa Barcelona, Frank Rijkaard na Mdachi mwingine Marco van Basten nao wanatajwa kuwemo kwenye orodha ya mmoja wao kuchukua nafasi ya ukocha Chelsea.

Mwingine anayetajwa ni kocha wa Tottenham, Harry Redknapp ambaye amepata mafanikio katika msimu miwili kwenye Uwanja wa
White Hart Lane, ameifanya timu yake kucheza soka nzuri ya kushambulia na kumfurahisha Abramovich.

Redknapp analipwa pauni milioni tatu kwa mwaka Spur, lakini kama atahamia Chelsea anaweza kulipwa pauni milioni tano pamoja na bonasi.

Chelsea kwa siku za karibuni imekuwa bize kujaribu kuwavutia makocha wapya kufanya kazi na kocha mwingine mpya.

Mchezaji wa zamani wa Blues, Gianfranco Zola alishaombwa na inaonekana kama yuko tayari kurejea.

Lakini Steve Clarke, amekataa kurejea Bridge.

Amechagua kusaini mkataba wa miaka mitatu akiwa msaidizi wa Kenny Dalglish, katika Liverpool licha ya kupewa ofa nzuri na Chelsea.

No comments:

Post a Comment