27 May 2011

Serikalia kutoa upendeleo kwa wanaosoma sayansi

Na Dunstan Bahai

SERIKALI imesema itaendelea kutoa upendeleo kwa walimu na wanafunzi wanaosomea masomo ya sayansi ili kupata wataalamu wengi wa fani hiyo hapa nchini badala
ya kuwategemea kutoka mataifa yaliyoendelea.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Kimataifa wa Kemia (IYC) ambayo kwa Tanzania inaadhimishwa Dar es Salaam.

Hafla ya uzinduzi huo iliandaliwa na Tume ya Taifa ya UNESCO kwa kushirikiana na Chama cha Wanakemia Tanzania ambapo kauli mbiu yake ni ‘Kemia-maisha yetu, mustakabali wetu’.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Prof Mbawala  alisema kwamba masomo ya sayansi kwa nchi ambazo zimeandaa watu wake, zimepiga hatua kubwa za kimaendeleo duniani.

“Kemia inachukua sehemu kubwa ya binadamu, huwezi kuzungumzia maendeleo kama watu wa nchi husika si wajuzi wa kemia. Kemia inaingia kila sehemu ya uzalishaji mali na maisha ya binadamu kama vile viwandani, mashambani, hospitalini, usindikaji wa vyakula na shughuli mbalimbali zinazomhusu binadamu na mazingira yake kwa ujumla,” alisema Prof. Mbarawa.

Alisema serikali imekusudia kwa dhati kuwekeza katika Kemia kwani vijana wengi wakijua masomo hayo nchi na watu wake watapiga hatua kubwa za kimaendeleo na vitu ambavyo vinaingia nchini vilivyotengenezwa nje vitatengenezwa hapa hapa.

“Watoto wetu lazima wawe na mwamko wa kupenda masomo ya sayansi…wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi tunakusudia kuanzisha mashindano ya masomo ya sayansi kwa wanafunzi wote nchini,” alisema.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO nchini, Profesa Elizabeth Kiondo alisema mwaka huu maadhimisho hayo yatatoa nafasi ya kupitia shughuli mbalimbali za kemia, kukuza tafiti na kusaidia maendeleo ya kemia katika elimu hapa nchini.

Uzinduzi huo umeshirikisha maonyesho ya kisayansi na hasa masuala ya kemia, uwasilishwaji wa mada mbalimbali za kemi na wataalamu waliobobea katika fani hiyo.

Maadhimisho hayo hufanyika duniani kote ikiwa ni pamoja na kusherehekea mafanikio yaliyopatikana kupitia kemia na mchango wake katika ustawi wa mwanadamu kuelekea maisha bora katika dunia salama.

Aidha maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 100 ya tuzo ya Nobel iliyotolewa kwa Bi. Marie Curie na hivyo kutoa nafasi ya kutambua mchango na ushiriki wa wanawake katika sayansi.

5 comments:

  1. Nawapongeza serikali kwa kuliona hili, ila pia inahitajika kuboresha maslahi kwa watu waliobobea kwenye mambo ya Sayansi katika sekta mbalimbali. Watu wengi wenye uwezo wa kumudu vizuri taaluma ya Sayansi huikimbia kutokana na kutokuwa na maslahi pindi wanapofuzu (haina future). Utakuta mtu aliyesomea sayansi kwa muda mrefu sana, labda mpaka ngazi ya Shahada ya pili bado yuoi chini kimaslahi kulingana na mtu wa Diploma katika fani ya akaunti. Hivyo bado kunahitajika kufanyika maboresho ya kimaslahi kwa waliobobea kwenye sayansi kama kweli tunataka kukimbizana na karne ya 21 (Sayansi na teknolojia).

    ReplyDelete
  2. Professor Tunashukuru kwa kauli yako ya kutaka kutoa upendeleo kwa wanaosoma sayansi lakini naona kama ulikuwa unapiga siasa tu, kwa kuwa umealikwa kuwa mgeni rasmi kwenye hayo maonyesho ya Kemia, kwa sababu hujasema huu upendeleo utakuwa wa namna gani.badala yake umesema utaanzisha mashindano ya masomo ya sayansi.Huu ndio upendeleo? ningetegemea ungesema kuanzia mwaka huu wanafunzi wote watakaojiunga na vyuo vikuu kusoma sayansi watalipiwa kwa 100%.na mishahara ya wahitimu wa sayansi itaanzia Millioni moja.Usifikiri hotuba mnazotoa hatuzifuatilii.Kama huna mipango endelevu ya kuboresha hiyo sayansi heri uiache tu usianze kudanganya watu.sayansi ni ngumu na inachukua muda mrefu mpaka mtu aweze kubobea, kwa hiyo ni matumaini yetu kuwa mngeonyesha nia thabiti ya kui support ili watu wahamasike kusoma, badala yake mnaiongelea majukwaani tu.Tuendelee na Mizaha kama ya Prof tuone kama tutafika mahali.

    ReplyDelete
  3. Shida siyo kutoa ahadi tu katika hafla maalum kama hizi, ila shida ni pale inapotokea kuwa msomi wa kemia au sayansi kwa ujumla akawa na maisha magumu baada ya elimu yake, huku watu kama wanasiasa, wabunge na watunga sera wengine wakawa na maisha mazuri ya kulipwa 12mill kwa mwezi. Kama serikali inataka kuendeleza sayansi na wanataaluma hiyo na ifanye hivo kwa vitendo badala ya ahadi hewa ambazo tumezizoea miaka na miaka. Nchi hii wanasiasa ni wataalamu sana wa kuongea mambo mazuri wakati wa hafla kama hizi na kisha kusahau, kuacha kufuatilia, mpaka tena hafla nyingine ikija. Let us be more serious!!

    Alfred Mwakivike, Arusha.

    ReplyDelete
  4. siyo solution ya kuiweka nchi katika taifa endelevu tuna wataalamu wengi sana hapa nchini wanasayansi wakiwemo je wana mchango wowote kwa taifa au wanasiasa ndo wamegeuka kufanya maamuzi ya kitaalamu mbona tumeona wimbi la wataalamu wa sayansi wakikimbilia siasa ili nao wale baada ya kukaa na udokta wao au uprofessor wao bila kushirikishwa kutoa mawazo ya kitaalamu nchi na sera zake zibadirishwe mawazo ya wataalamu ndo yaongoze nchi na wanasiasa wawasikilze wataalamu na kazi zao zibaki wanasiasa na siyo kutoa mawazo ya kitaalamu wakati hawana utaalamu pi fungu la reseach halipo unakuta vyuo vinalia fungu la reseach halipo prof hajawahi kufanya reseach toka apate uprofesor hili taifa linaangamia dunia inakwenda mbele Tanzania tunarudi nyuma kama hakuna reseach taifa litaendelea vipi kama wanasiasa ndo wanatoa maamuzi ya kitaalamu taifa litaendelea vipi, ebu angalia swala la umemem na waziri wa anayehusika ni mwanasheria hajui hata terminology yeyote ya umeme lakini unakuta ndo mwamuzi wa mwisho ifike sehemu wizara iongozwe na mtaalamu na siyo mwanasiasa wabunge waswe mawaziri ili wataalamu wamshauri raisi kuiongoza nchi na wanaisasa wabakie kuibua hoja bungeni ili wataalamu waamue na watengeze sera jamani watanzania tuamke reaky we are dying

    ReplyDelete
  5. Rafiki zangu mliotoa idea hapo juu Nawasapoti,HUYO Prof.amesema hayo naona kwa sababu amekua mgeni rasmi tu.

    ReplyDelete