Na Zahoro Mlanzi
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mbwana Samatta nyota yake inazidi kung'ara baada ya Klabu yake mpya ya TP Mazembe kumpeleka kufanya majaribio katika
timu za Arsenal ya Uingereza na Anderletch ya Ubelgiji Desemba mwaka huu.
Samatta ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', alisaini mkataba wa miaka mitano hivi karibu wenye thamani ya sh. mil. 150 na mabingwa wa hao wa Afrika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mlezi na Mshauri wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo alisema wameshamalizana na TP Mazembe na sasa Samatta ni mchezaji halali wa mabingwa hao wa Afrika.
"Namshukuru Mungu safari ilikuwa ya mafanikio na tumerudi salama, rafiki zetu walitupokea vizuri wakiongozwa na Mwenyekiti, Katanga Musa Katumbi na Meneja, Fredrick ambapo tulisaini mkataba bila matatizo yoyote," alisema Kasongo.
Alisema wamesaini mkataba wa miaka mitano, ambao kila baada ya miaka miwili lazima wakae tena chini kuzungumza ambapo pia suala la marupurupu limeachwa kutokana na timu hiyo kutoa marupurupu mengi kwa wachezaji wake.
Kasongo alisema mbali na kukamilisha suala hilo, pia klabu hiyo imewaambia wana mkataba na timu za Arsenal na Anderletch ambapo kila mwaka hupeleka wachezaji wanane kwenda kufanya majaribio na kwa mwaka huu, Samatta ni miongoni mwa wachezaji watakaokwenda huko.
"Unajua TP Mazembe wana mkataba na Arsenal na Anderltch wa kupelekeana wachezaji kufanya majaribio, Samatta atakwenda huko na atakaa kwa muda fulani na klabu hizo zikivutiwa na kiwango chake, yeye mwenyewe ndiye atakayeamua klabu atakaoichezea," alisema Kasongo.
Wakati huo huo, Kisongo alisema timu hiyo inatoa marupurupu ya kutosha kwa wachezaji wake ndiyo maana wachezaji wengi wanashindwa kwenda kucheza Ulaya kutokana na fedha za ziada wanazozipata.
Alisema timu hiyo hupewa maslahi makubwa, jambo ambalo linazidi hata mishahara wanayopata na ndiyo maana klabu nyingi za Ulaya zinashindwa kuchukua mchezaji kutoka katika timu hiyo.
Haya bwana mdogo Mbwana Samatta, umelitoka soka la Tanzania ambalo kwa kiasi halijakua kama la wenzetu hao. Jitume kijana ili hatimaye tukusikie Ulaya ukicheza soka la wenye kulijua. Baada ya Arsenal tutasikia Man U; halafu Barca; halafu tena sijui wapi. Kaza buti, Mungu yuko nawe.
ReplyDeleteMUNGU AMUONGOZE LAKINI ISSUE YA MSINGI SAMATTA ASIBWETEKE MAANA WACHEZAJI WETU WANATABIA YA KUJIONA WANAWEZA KITU KINACHOPELEKEA DHARAU NA KUPUUZIA MAZOEZI..SAMATTA ISSUE YA KWANZA ATAFUTE NAMBA YA KUDUMU TP MAZEMBE ILI ACHEZE MECHI NYINGI VINGINEVYO ATAISHIA HAPO NA ATARUDI KAMA HARUNA MOSHI...VILE NAOMBA TEAM KUBWA KAMA SIMBA,YANGA,MTIBWA NA NYINGINE WATAFUTE WACHEZAJI CHIPUKIZE MITAANI HASA MIKOANI KWANI WAPO WENYE VIPAJI ZAID YA WAGENI WANAOGOMBANIA..VILE HII ITATUSAIDIA KUJENGA TAIFA STARS YA BAADAYE.BY LAMU ELIZAYO,P-UDSM
ReplyDelete