05 May 2011

Samatta agoma kwenda Ulaya

Na Zahoro Mlanzi

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Mbwana Samatta amekataa sh. milioni 200 kutoka kwa Klabu ya Austria Vienna ya Austria kutokana na klabu hiyo kumuhitaji kwa ajili
ya majaribio, badala ya kumsajili moja kwa moja.

Klabu hiyo ilikuwa imetenga zaidi ya sh. milioni 200 kwa Samatta, endapo angefuzu majaribio ambapo inashiriki Ligi Kuu ya nchini humo ya Austria Bundesliga.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam juzi, Mshauri wa mchezaji huyo ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa African Lyon, Jamal Kisongo alisema wakati wanasaini mkataba wa Samatta kwenda TP Mazembe, walishapokea ofa mbalimbali za mchezaji huyo kutakiwa Ulaya.

"Unajua huyu kijana (Samatta), ana bahati sana, huwezi amini alitengewa mamilioni ya fedha na Klabu ya Austria Vienna ya Austria, ambazo ni zaidi ya zile zilizompeleleka Mazembe, lakini tulifikiria mbali na kuamua asiende huko.

"Uzuri Mazembe walikubali moja kwa moja kumsajili na wakataja dau lao, lakini hiyo timu nyingine walimuhitaji kwa majaribio alafu akishafaulu ndipo watoe hayo mamilioni yao, tukajiuliza asipofuzu itakuwaje ndipo tulipoona bora aende Mazembe," alisema.

Alisema endapo klabu hiyo ingeonesha nia ya kumsajili moja kwa moja kama ilivyofanya TP Mazembe, basi wangekubali Samatta aende kucheza soka la kulipwa nchini humo.

Kisongo alisema hata hivyo ana uhakika TP Mazembe, kutokana na timu hiyo kujulikana karibu ulimwenguni kote, hana shaka akiwa na bidii basi atazidi kusonga mbele kwa kucheza Ulaya.

Historia ya Austria Vienna, inaonesha kwamba ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi ubingwa wa ligi ya kwao kwa kutwaa mara 23, Kombe la Austria Super mara sita, Kombe la ligi mara 27 na ilishawahi kushiriki michuano ya Ligi ya Ulaya mwaka 1978.

2 comments:

  1. Mdogo wetu uamuzi wako sawa kabisaa,kwani waswahili wanasema"HERI TISA NENDA USIRUDI,KULIKO KUMI NENDA RUDI"

    ReplyDelete
  2. It the normal and standard process of getting a job, you do interview with your potential employer and if you get the job you go through probation period. Nobody will hand you that such money just like that...they want to see your skills and work ethics. Life is about taking risks....big risk, big reward!! You took a shortcut to success…

    ReplyDelete