Na Amina Athumani
VODACOM Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala ataondoka leo kwenda Bukoba kwa ajili ya kutembelea vituo vya watoto yatima.Genevieve atafanya ziara hiyo
ya siku mbili, ambapo atatembelea vituo viwili vya watoto yatima, pamoja na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hao.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency anayoratibu mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema mrembo huyo atatembelea kituo cha Nusura yatima na Umri yatima, vilivyopo katika mji huo.
"Mrembo wetu wa Vodacom Miss Tanzania ataondoka kesho (leo), akiwa na Mkuu wa itifaki, Albert Makoye ambapo watakaa huko kwa siku mbili na kazi kubwa itakuwa ni kutoa misaada mbalimbali kwa yatima," alisema Lundenga.
Alisema ziara hiyo ya kijamii ni moja ya shughuli kubwa anazotakiwa kufanya mrembo wa Tanzania, ambapo zipo ndani ya mkataba wake katika kipindi chote anachoshikilia taji hilo.
No comments:
Post a Comment