LONDON, Uingereza
TAJIRI Roman Abromovich yuko tayari kutumia pauni nyingine milioni 80, kwa ajili ya kufanya usajili katika majira ya joto ili kuwaleta wachezaji wazuri kwenye kikosi cha
Chelsea.
Bilionea huyo wa Kirusi, anataka kikosi cha Blues kucheza soka ya kufurahisha zaidi, na kushambulia katika msimu ujao.
Januari mwaka huu, alipanga kutumia kiasi cha pauni milioni 72, kwa kuwasaini wachezaji wawili, Fernando Torres na David Luiz.
Mmiliki huyo wa Blues, amekuwa akitaka kuziba nafasi tatu, kiungo mchezeshaji, winga na beki wa kulia na amemwambia Mtendaji Mkuu
Ron Gourlay, kuandaa wachezaji anaowataka.
Wachezaji wanaolengwa wanaaminika kuwa ni nyota wa Arsenal, Cesc Fabregas, wa Tottenham, Gareth Bale na Mholanzi Gregory van der Wiel.
Wachezaji wengine wanaotazamwa ni Wesley Sneijder, Thomas Muller, Adam Johnson, Matt Jarvis, Ashley Young, Jack Rodwell, Marouane Fellaini, Luka Modric na Andrey Arshavin.
Chanzo kutoka ndani ya Blues kilisema: "Roman kila wakati amekuwa akitaka kuona Chelsea ikicheza soka ya kufurahisha.'
Anapenda wacheze mechi na kupata matokeo ya kushida mabao kama 4-3, kuliko kushinda 1-0.
No comments:
Post a Comment