Na Stella Aron
KAMPUNI ya Qnet ya inayoshughulika na masuala ya mtandao imeandaa matembezi ya hisani maalumu kwa ajili ya kuchangia hospitali ya Ocean Road pamoja na wagonjwa wa saratani ambapo mawaziri na viongozi mbalimbali wanatarajia kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Wakala wa Kampuni hiyo, Bi. Gilda Kaindoah, alisema kuwa matembezi hayo yanatarajia kufanyika kesho ambapo yanatarajia kuanzia katika hospitali hiyo kwenda maeneo ya Ikulu na kurejea tena katika hospitali hiyo.
Alisema kuwa kutokana na kampuni hiyo kuwa na jukumu la hiari la kusaidia jamii imeadhimia kufanya matembezi hiyo kwa nia ya kukufanya sh. milionin 60 ambapo zitasaidia ununuzi wa jenereta kwa ajili ya hospitali hiyo na ukarabati wa huduma nyingine katika hospitali hiyo.
"Mbali na takwimu za Shirika la Afya duniani (WHO )kuonesha kasi ya ongezeko la watu wanaougua ugonjwa huo ni zaidi ya milioni tisa kwa mwaka na kati yao milioni tano hufariki dunia na Tanzania ikiwa na hali mbaya hivyo tume na ni bora tukaanzia na hili, " alisema.
Bi. Kaindoah alisema uwa kulingana na takwimu za WHO za mwaka 2002 wagonjwa wa kansa huongezeka wastani wa watu 21, 000 kwa mwaka idadi nyingine wakipoteza maisha na kusababisha hospitali hiyo kuzidiwa na wagonjwa wanaojotokeza kutaka mahitaji mbalimbali ya tiba .
"Mahitaji katika hospitali hiyo ni kubwa, fedha za nauli kwa wale wanaofika kwa ajili ya huduma na kurudi kutoka mikoani imekuwa ni ngumu hivyo tunaomba kila Mtanzania ashiriki na atuunge mkono katika maanddamano hayo, " alisema Bi, Kaindoah.
Alisema katika matembezi hayo mawaziri mbalimbali wanatarajia kushiriki wakiwemo viongozi mbalimbali wa kitaifa ili kuweza kuchangia hospitali hiyo ambapo yanatarajia kuanza saa 1 asubuhi na kumalizika saa 4 asubuhi.
No comments:
Post a Comment