Godfrey Ismaely
RIPOTI iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) inaonesha kuwa Jeshi la Polisi nchini linaongoza kwa katika vitendo vya
kupokea rushwa kutokana na tabia za watendaji na maofisa wake kujihusisha na upokeaji wa rushwa ili kuachia watuhumiwa kuwa huru.
Taarifa hiyo iliyotolewa na TAKUKURU kwa mara kwanza baada ya Rais Jakaya Kikwete kuitaka taasisi hiyo kuweka wazi ripoti hiyo baada ya kukaa kimiya kwa miaka mwili kuanzia 2009.
Ripoti hiyo iyonadaliwa kwa kuwahoji watu wa kada mbalimbali inaonesha kuwa wananchi kwa hawana imani na jeshi hilo kutokana na maofisa na watendaji wake kujihusisha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa hasa kwa watuhumiwa, hivyo kuchangia kushindwa kupata ushirikiano wa karibu kudhibiti vitendo hivyo.
Inonesha kuwa asilimia 62.7 ya wananchi hao hawana imani na jeshi hilo kwa kuwa halizingatii maadili, huku asilimia 44.6 wakisema kuwa maofisa wa polisi ndiyo vinara wa kupokea rushwa, asilimia 55 walisema kuna uhusiano mzuri kati ya jeshi la polisi na wao katika kuwakatama wahalifu,
Lakini asilimia 54 walisema jeshi hilo haliridhishi katika utendaji wake, 34 walisema kuwa polisi huwa hawana hamu ya kulisaidia jeshi hilo hususani kuwakatamata wahalifu katika muda muafaka
Ripoti hiyo inaeleza kuwa mahakama inashika nafasi ya pili katika kujihusisha na vitendo vya rushwa na kushindwa kufikia misingi ya utawala bora, kwa kuwa katika maelezo ya watu waliahojiwa walisema kuwa majaji, mahakimu na makarani wao huwa wanapokea rushwa ili kuharakisha kesi za husika.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo inaeleza kuwa asilimia 73.2 ya watu waliohojiwa walisema kuwa huduma za mahakama zinatolewa kawaida wala hazina mabadiliko, huku asilimia 68.6 hawatambui kama kuna vitendo vya rushwa, 87.4 .
Watu wengine walisema hawatumii mahakama kutatua matatizo yao, huku asilimia 57.9 ikisema kuwa watendaji wa mahakama wakiwamo majaji huwa wanapokea rushwa mahakamani bila kificho.
Ripoti hiyo inaitaja sekta ya elimu kuwa inashika nafasi ya tatu ambapo kuwa wananchi mbalimbali walihusishwa katika ukusanyaji wa taarifa hiyo asilimia 81 walidai kuwa utoaji wa huduma unaridhisha kidogo, asilimia 11 walisema hutoaji wa huduma ni mzuri huku asilimia 18 wakisema kuwa huduma ni mbaya.
Ripoti hiyo inafafanua kuwa wahojiwa walisema kuwa kiwango cha elimu kinashuka kutokana na mfumo wa maisha, mfumuko wa gharama za kuendeshea maisha na uhaba wa walimu wazuri.
Walisema ingawa gharama za ada katika shule za msingi zimefutwa, pia shule nyingi zimekuwa zikitoza gharama mbalimbali ambazo wakati mwingine hazina maelezo kwamba zinaenda kufanyia nini katika shule husika.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wakusanyaji wa taarifa ambao walikuwa utawala bora na timu ya kukusanya takwimu za rushwa 2009, asilimia 30.2 ya watoa taarifa ilisema kuwa hawana makisio halisi ya fedha zinazotozwa, huku asilimia 46.4 walisema huwa wanalipa kwa mwaka sh. 500,000, huku asilimia 20 ya wahojiwa ikisema kuwa huwa inalipa sh. 500,000 hadi sh. 200,000 kwa muhula mmoja.
Sekta ya Afya inashika nafasi ya nne kutokana na huduma nyingi zinazotolewa na vituo vya afya hapa nchini kutolewa kwa upendeleo kwa baadhi ya makundi ya watu huku asilimia 65 ya wahojiwa wakisema kuwa inaridhisha kidogo na wakati mwingine wakisema kuwa kuna unafuu kidogo.
Huku asilimia 50 ya waliohojiwa wakisema kuwa watendaji mbalimbali wamekuwa wakitoa huduma za afya kwa upendeleo hasa kwa kujihusisha na vitendo vya kupokea rushwa, asiliamia 71 ya madaktari wameelezwa wanajihusisha na vitendo vya rushwa.
Kwa upande wa wauguzi, asilimia 68.2 ya wauguzi wasaidizi katika Vituo vya Afya ndani ya kata asilimia 67.5 hujihusisha na vitendo vya rushwa ili kutoa huduma kwa wagonjwa hivyo kuwawia vigumu kufanikisha malengo yao ya kupata huduma bora ya afya pindi wanaposhindwa kutimiza vigezo.
Hali hiyo ilileta utata huku watafiti wakilazimika kuwaeleza wahojiwa wanapolinganisha huduma za afya kwa sasa na miaka mitatu iliyopita wanaionaje, asilimia 53 walisema kwa kiasi kidogo huduma imeboreshwa lakini asilimia 11 ikisema haielekei
Na asilimia 52.5 walisema huduma ya afya wanatarajia itaboreshwa zaidi huku asilimia saba ya watu waliohojiwa ikisema kuwa wanatarajia huduma hiyo kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyo kwa sasa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo inaeleza kuwa wahojiwa kati ya asilimia 70, asilimia sita walisema kuwa sababu zinazochangia huduma za afya kuwa mbaya ni pmaoja na mazingira mabaya ya kufanyia kazi kwa watendaji wa afya, kutopatikana kwa vitendea kazi vya afya miundombinu mibovu, kutokuwapo kwa wataalam wa kutosha katika sekta ya afya pamoja na njia nyingine za kuhamasisha na kuboresha sekta za afya.
halafu serikali inataka tuwe na amani!! amani inavunjwa na vyombo vya dola
ReplyDeletetakukuru yenyewe vipi kwani nao pia ni wala rushwa wakubwa.
ReplyDeleteHii sio mara ya kwanza kwa takwimu kama hizi kutolewa. Lakini bila hata hizo takwimu kutolewa, sisi wananchi tunaona hali halisi. Ukiona polisi na mahakama haviaminiki katika nchi yoyote, ujue aidha hiyo nchi haina uongozi au kama upo hawawajibiki. Raisi ana uwezo wa kutokomeza rushwa kwa 90% kwa wiki moja tu, kama akiamua kufanya hivyo. Nataka kumtia moyo, inawezekana. Mbona Sokoine alitokomeza ulanguzi (rushwa) na hakuwa raisi? Lyatonga Mrema je, alipokomesha vitendo vya namna hiyo alikuwa raisi? Namshauri raisi, kungoja kuletewa taarifa za nani mpokea rushwa zaidi, haina tofauti na kutumia muda kumwambia mtoto aandike kama anaona mvua, na ni wakati wa masika!
ReplyDeleteyeah mie pia nakubaliana na waliosema lakini je TAKUKURU wamechunguzwa nao maana ni watanzania walewale ka waliopo polisi na mahakamani mie maoni yangu pengine TAKUKURU kugongana na polisi katika kazi zao wanahuhasama nao Pia kwa kesi zao kushindwa mahakani kwa kutopeleleza vizuri zinaweza zikawa sababu kwa takwimu zao lakini jamani ebu angalia rushwa ndogo ndogo zilivyojaa serikalini kila mahali toka kijijini hadi uongozi wa kitaifa hebu hurumieni hawa watanzania maisha mazuri kwa kiongozi yanayotokana na rushwa yana matokeo mabaya baadaye yataliangamiza taifa huko mbele haiwezekani mtu ajirimbikizie mali na wenziye wana kufa njaa wabunge wanalipwa hela nyingi lakini hta kazi zao hazioneshi kuwatetea waliowatuma wanakalia viti vizuri kuliko hata bunge la uingereza jamani hili taifa limelaaniwa, si raisi peke yake kila mmoja apinge rushwa na takukuru wafanye kazi ya kitaalamu siyo kuvizia watu waishauri serikali sera nzuri na adhabu za rushwa ziwe kubwa na jinsi ya ya kuthibisha shitaka ihamie kwa anaye shitakiwa kwani rushwa si mauaji ni msururu wa wahusika sheria ibadirishwe anaye kamatwa na rushwa ndo adhibitishe kuwa mali aliyonayo haikutokana na rushwa
ReplyDeleteHaya yanayoelezwa kuhusu Jeshi la Polisi na Mahakama, Hivi nani Asiye jua katika Nchi yetu kuwa hawa ni VINARA wa RUSHWA na tatizo viongozi wa Nchi ndiyo wanao walinda.Watu wanapiga kelele kila siku Lakini Viongozi wanajifanya hawasikii wala hawaoni sasa angalieni wenyewe hiyo AMANI tunayoipigania itakuwepo kweli,waliopewa majukumu ya kuilinda na kuitetea haki wao wanaivunja, Nchi yetu serikali imeshindwa kuongoza wanadanganya wananchi, hivi kweli wanaelewa umuhimu wa jeshi la polisi na mahakama popote pale duniani lakini nchini kwetu wanalichukulia kama masihara, huku ndiko kutakako leta matatizo na viongizi mnayajua haya ila kwa kuwa vichwa vyenu havisikii maumivu hamjali licha ya hii mifano yote inayotokea duniani ila siku itakapo tokea ndiyo mtakapo tia akili, Rais mubarack yuko jela anasubiri hukumu,Rais mabotu alikufa kama yatima, mali na miungu watu vyote vinakwisha,kufatana na katiba yetu RAIS na WAZIRI mkuu ndiyo wenye maamuzi ya mwisho nawaomba kama ni kondoo basi vaeni ngozi ya simba nchi inaharibika na wabaya wenu ni hao mnaokula nao mezani, uwa nyani usimtizame machoni.
ReplyDeleteSwali langu kwetu sote Watanzania! Ni nani asababishaye UTOAJI NA UPOKEAJI WA RUSHWA? Kama ninavyofahamu ni kwamba mtoaji rushwa na mpokeaji wote ni wakosaji! Mbona tunashambulia upande mmoja tu ule wa mpokeaji? Je mtoaji naye ana sehemu gani katika kusababisha hali hii?. Kama unajua unapotoa rushwa ni kosa kwanini utoe? Ni vema sote tushikamane; kama mtu akionekana anatoa rushwa na yule ampaye kabainika kuipokea basi wote wawajibishwe kisheria la sivyo tutakuwa tunapiga hewa pasipo mafanikio. Ninakumbuka siku moja nilikuwa nasafiri kwa gari langu na mwendo wangu ulikuwa kasi na nikapigwa tochi na askari wa uasalama barabarani, akaniambia ninakosa na kwa kuwa kweli nilikuwa na kosa nikakubali; akaniambia nitoe chochote bila stakabadhi; mimi nilikataa na kumwambia aniandikie stakabadhi ya shiringi elfu 20 ambayo ndiyo faini ya kuzidisha mwendo, bila sitabadhi ilikuwa chochote kile!!!!!! Nilitoa 20 elfu na nikapata stakabadhi yangu. Ni mfano mdogo tu lakini ipo mikubwa kweli kukiri kosa ili uhukumiwe si kazi rahisi, Mashehe, Makasisi na Mapadiri na Wachungaji nk. isaidieni jamii kujua hili. Kukomesha rusha rushwa kutakuja tu kama sehemu zote mbili zitatiliwa umuhimu. Yakumbukwe ya Baba wa Taifa JKN!
ReplyDeleteHaisaidii kusema kila siku hilo tumeshajua siku nyingi tunataka vitendo
ReplyDeleteVitendo vipi unavyotaka? Mojawapo ya vitendo ni kutotoa rushwa au hongo na cha pili ni kutopokea. Watanzania wote tusikubali kununua haki kwa njia yoyote ile, bali kila mmoja ajitahidi kujipatia haki yake kwa njia za halali na abinikapo mtu kufanya kinyume cha hilo asikubalike katika jamii.
ReplyDelete