26 May 2011

Off Side Trick kunogesha Vimwana nusu fainali

Na Victor Mkumbo

KUNDI la Muziki la Off Side Trick la Zanzibar, linatarajia kuungana na bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' katika kutoa burudani kwenye nusu fainali ya mashindano ya
Kimwana wa Twanga Pepeta 2011' yatakayofanyika Mei 27, mwaka huu katika Ukumbi wa Sun Siro, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Mratibu wa mashindano hayo, Maimartha Jesse alisema fainali hiyo itashirikisha vimwana 24 kutoka katika maeneo mbalimbali.

Alisema matayarisho ya mashindano hayo yanaendelea vizuri, ambapo washiriki wanaendelea kujifua vikali kwa ajili ya fainali hiyo.

Mratibu huyo alisema vimwana hao wapo chini ya mwalimu wao Kassim Mohamed 'Super K' pamoja na Husna Idd 'Sajenti'.

Alisema kuwa washiriki wa mwaka huu wameonesha vipaji vya kucheza kwa kiwango cha hali ya juu tofauti na miaka ya nyuma.

Maimartha alisema mshindi katika mashindano hayo anatarajia kukabidhiwa duka la Vipodozi lenye thamani ya sh. Mil 5.

1 comment:

  1. natamani samaki aliwe jukwaani i think patakuwa padogo yaani hapatoshhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhi!

    ReplyDelete