26 May 2011

Man City yamtega Ronaldo kwa euro mil. 200

LONDON, England

KITITA cha Manchester City, ilichotenga kwa ajili ya kumnasa nyota wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo kimebainika kwamba ni euro milioni 200.Vyanzo vya
habari vinaeleza kuwa hivi sasa kuna watu wanaofanya kazi kwa niaba ya timu hiyo, ili kuhakikisha wanamnsa nyota huyo wa zamani wa Manchester United.

Vyanzo hivyo vilieleza kuwa Manchester City, inataka kutoa dau la euro milioni 200 ili kumrejesha Ronaldo, England na kumkabidhi mkataba wa jumla ya euro milioni 17 kwa mwaka, ikiwa ni zaidi ya euro milioni 7 kwa fedha anazolipwa Real Madrid.

Hata hivyo Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anadaiwa kukataa ofa hiyo na akawaeleza kuwa, ili waweze kumnasa Ronaldo ni lazima wajipinde na kujikamua euro bilioni moja.

No comments:

Post a Comment