24 May 2011

Ndugu wa waliouawa North Mara wamtaka Ocampo

Na Mwandishi Wetu, Tarime

WAKATI ndugu wa marehemu waliouawa siku saba zilizopita katika mgodi wa North Mara uliopo wilayani hapa wakitarajia kuzika miili ya ndugu zao kesho, jana
walimwomba Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Bw. Luis Moreno Ocampo anayeshughulikia makosa ya kuwashughulikia waliofanya mauaji hayo.

Mmoja wa wanandugu hao ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema
itakuwa vema endapo Ocampo atawasaidia na Watanzania pia ambao
wamekosa imani na serikali yao kwani mauaji hayo hanajirudia mara
kwa mara bila ufumbuzi na wahusika hawachukuliwi hatua yoyote.

Alisema wamekuwa wakimskia Ocampo akiwasaidia sana raia wa Kenya, hivyo
wana imani hata hapa nchini anaweza kuwasaidia na tatizo hilo likaisha,
kwani hivi sasa hawana imani ya kuendelea kuishi Nyamongo wakiwa kama
raia halali wa Tanzania.

Alisema kuwa wamechoka kuona ndugu zao wanauawa kama nyumbu, ilihali hata nyumbu hawaezi kuuawa bila kibari maalumu, iweje wao wauawe tena na askari wa Kitanzania wanaolipwa mishahara itokanayo na kodi zao.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Singida Mashariki, Bw.Tundu Lissu amewambia waandishi wa habari kuwa mazishi yatafanyika
kesho na miili ya marehemu itaagwa katika uwanja wa mpira wa
sabasaba na baadaye kusafirishwa katika maeneo mbalimbali husika.

Bw. Lisu ambaye pia ni mwanasheria wa CHADEMA, aliyasema hayo nje ya nyumba ya kuhifadhia maiti baada ya Dkt. Greshon Nyaike kufanya uchunguzi katika miili minne iliyohifadhiwa katika Hosptali ya Wilaya mjini hapa na kuwataka waandishi kueleza ukweli kuwa miili hiyo iko salama.

“Miili iko salama na chama kiligharamia dawa ya kuhifadhia miili
kiasi cha kuwa salama hata ndani ya miezi mitatu, sasa nashangaa
na kusikitishwa na taarifa za uongo kuwa miili imeharibika si kweli
kabisa,” alisema.

Alisema sababu ya msingi iliyofanya uchunguzi huo ufanyike ni kutaka
kujua na kuona ni sehemu gani za miili hiyo zilizopingwa risasi ili
kuwachukulia hatua waliohusika.

Alifafanua kuwa endapo mtu akiwa amepigwa kichwani au kifuani
in amaana kwamba alimpiga risasi amekusudia lakini akiwa amempiga
miiguni itajulikana kuwa mtu huyo hajakusudia kuua isipokuwa alikuwa
katika harakati za kujihami.

Alisema ingawa mwili mmoja wa marehemu Chacha Mwasi Bisaru (25)
uliibiwa na kuzikwa kwa Komaswa bila ridhaa ya wanandugu, familia yake
itapata rambirambi sawa na wengine watakaowazika ndugu zao kesho.

Waliouawa katika tukio hilo ni Mwikwabe Marwa (32) mkazi wa
Kitongoroma Serengenti, Chacha Ngoka (19), Mkazi wa Kewanja Nyamongo, Emmanuel Magige (23), mkazi wa Nyakunguru na Chawari Bhoke (27) mkazi wa Bonchugu Serengeti pamoja Chacha
Mwasi Bisaru (25) mkazi wa Komaswa.

3 comments:

  1. Nawapa pole wote wafiwa nawaombea roho zao ziwekwe mahala pema peponi Amiin,Kuna mambo yanashabikiwa kwa nguvu zote kuyageuza kuwa ya kisiasa na watu kutaka umaarufu kupitia vifo hivi tuwe makini na watu wanaokusudia kutugawa.wakati huu tunatakiwa tuwe kitu kimoja na kujuwa kiini na kukomesha kabisa hali kama hizi zisitokee tena.

    ReplyDelete
  2. poleni sn,wafiwa.
    hili swala haliepukiki bila wanopenda haki kuingilia kati bila wanasheria kina Tundu Lisu au wapenda haki CHADEMA kulifuatilia haki haitapatikana.Tumechoshwa na mauaji ya ccm,wanaua makusudi raia halafu wanadai oooh,wanasiasa wanataka kupata umaarufu,umaarufu gani tena anautaka Lisu,Mbowe au Dr.Slaa,mtanzania gani wa leo 2011 hajui kazi,msimamo,na uwajibikaji wa wa2 hao?...
    Siasa ndiyo inaendesha nchi na dunia kiujumla,CCM waliua watu Arusha kisiasa na wakaizima kisiasa hata huko migodini,wanaua wa2 kisiasa,mnakumbuka Bulyankuru wa2 walivyofukiwa wazima,mheshimiwa Mrema anaushahidi wote na ilikuwa kisiasa hvyo hivyo wa2 kulinda nafac zao kwa wageni.
    CCm ndiyo ime2fikisha huku na bila kujali,inasema wanasiasa,RPC anaacha kutuambia juu ya upelelezi wa wauaji,analeta casa eti chama kimoja kinataka kupata umaarufu hii ni haki,wanaona haivumiliki kuzuia miili kuzikwa ili ichunguzwe,lakini inavumilika kwa kuua wa2 waco na hatia wanaodai haki zao..
    CHADEMA endeleeni kutetea haki za wanyonge ndiyo kazi ya chama cha siasa,CCm 2tafika 2,mnapotaka 2fike wala c mbali.......

    ReplyDelete
  3. HAKUNA KITU KINACHONITIA KICHEFUCHEFU KAMA SERIKALI YA CCM,WAKATI FULANI UTADHANI HAWAKUSOMA,AU WANA MATATIZO YA AKILI.MARA NYINGI WANAONGEAGA KAMA WATOTO WADOGO,ZAIDI HUONGEA BILA HATA KUFANYA UTAFITI,WAKIDHANI WANAWAAMBIA WATOTO WADOGO.HIVI KUSEMA WANASIASA WANATAKA WAJIPATIE UMAARUFU KTK MSIBA WA WATU WALIOUAWA NA POLISI.WAMESAHAU KUWA WALISEMA WALIOKUFA NI WAHALIFU,WAKATI HUOHUO WAKITAKA KUTOA SH ML 3 KWA KILA MFIWA JE HII HAIKUWA KUJIPATIA UMAARUFU WA KISIASA? WENYEWE WALITAKA KUFUNIKA DHAMBI YAO,NDIO MAANA WALIKUWA WANASEMA KUWA WANASIASA WANATAKA KUJIPATIA UMAARUFU.CCM IMENICHOSHA KIASI CHA KUNIFANYA KUSHINDWA KURUDI TZ MAANA NAWEZA KUVAA MABOMU NIKAJILIPUA MBELE YA HUYO RAIS WAO.AMESABABISHA NCHI KWENDA MRAMA,MAISHA WA WATANZANIA YAMEKUWA MAGUMU KWA AJILI YA UONGOZI WAKE MBAYA..SASA LINALOBAKI MUNGU ANAJUA ILA TUMECHOKA.

    ReplyDelete