24 May 2011

Mfugale Mtendaji Mkuu TANROADS

Na Edmund Mihale

WAZIRI wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli amemteua, Bw. Patrck Mfugale kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).Taarifa iliyosainiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Herbert Mrango na kusambazwa kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilieleza kuwa uteuzi huo unaanza Mei mwaka huu na utadumu kwa miaka mitatu.  

"Kwa mujibu wa sheria ya Wakala wa Serikali (Excutive Agencies Act No 30 ) ya mwaka 1997 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009, Waziri Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Injinia Patrick A. L Mfugale kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS)," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Bw Mfugalea alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS na amewahi kushika nafasi mbalimbali katika serikali na kusimamia ujenzi wa barabara na madaraja muhimu kwa taifa.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa Bw. Mfugale pia aliwahi kushika majukumu maalumu katika wizara hiyo kama Mkurugenzi wa Idara ya Barabara za Mikoa.

Bw. Mfugale ambaye ana Shahada ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Roorkee India, na Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu Loughborough cha Uingereza, ni mhandisi aliyesajiliwa na amehudhuria mafunzo ya Ujenzi na uchumi, Mafunzo ya miradi na utunzaji wa barabara pamoja na ujenzi na utunzaji wa madaraja.

No comments:

Post a Comment