16 May 2011

Nape: Ikithibitika nilipeleka siri CCJ nitawajibika

Na Grace Michael

SIKU moja baada ya Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Fred Mpendazoe kuanika wazi kuwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Bw. Nape Nnauye alikuwa ndio injini ya uanzishwaji wa Chama cha Jamii (CCJ) na alikuwa akivujisha siri za Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema yuko tayari kuwajibika endapo siri hizo zitatajwa hadharani.

Bw. Nnauye aliweka msimamo wake jana baada ya kuhojiwa na Majira kuhusu  tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake na CHADEMA.

“Tuhuma ya mimi kuwepo kwenye mkakati wa uanzishwaji wa CCJ ni uzushi usio na mashiko kwani jana (juzi) niliposikia ndo nikaanza kuuliza hata ofisi zao zilipo...lakini kubwa waeleze pia CCJ ilikufaje na hizo siri wanazodai nilikuwa nawapa wazitaje hadharani nitawajibika,” alisema Bw. Nnauye.

Kuhusu tuhuma za kula mishahara miwili wa CCM na wa Mkuu wa Wilaya, alisema kuwa tangu ateuliwe hata mwezi haujaisha tangua ashikea nafasi hiyo hivyo kukanusha kupokea mishahara miwili.

Tuhuma nyingine ambayo ilielekezwa kwake ni ya kuhusika na kula fedha zilizotokana na ufisadi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ambapo kwa hilo alidai kuwa wakati ufisadi huo ukifanyika yeye alikuwa masomoni India.

“Ushauri wangu kwa CHADEMA wajifunze kula vya kuchinja waachane na vya kunyonga,” alisema.

Akifafanua usemi huo alisema kuwa CHADEMA wanatakiwa waishi kwa kufanya kazi halali na sio kupika majungu na kupandikiza chuki kwa Watanzania kwa kuwa mwisho wa uongo ni aibu na akasema kuwa mwisho wa chama hicho umefika.

Juzi Bw. Mpendazoe akihutubia wananchi wa Mbamba Bay mkoani Ruvuma alianika mpango mzima wa waliohusika na uanzishaji wa CCJ na kuweka bayana kuwa Bw. Nnauye ndiyeo aliyekuwa akitumika kuandaa katiba ya chama hicho na kukusanya siri mbalimbali za CCM.

Alisema kuwa “Nape ni mnafiki, msaliti na mhaini ndani ya CCM kwa kuwa alishakula njama za kukiangusha CCM...tulifanya naye vikao vya siri hadi tukaanzisha CCJ leo anaitetea CCM ambayo alikuwa ameiona haifai, ni mnafiki mkubwa,” alisema Bw. Mpendazoe.

Alisema kuwa Bw. Nape ndiye alikuwa akitumika ndani ya CCJ kwenda kwa wafadhili kupokea fedha za kuanzisha chama hicho na ndiye aliyehusika kutafuta pango la chama.

Alikwenda mbali kwa kusema Rais Jakaya Kikwete anaongoza chama feki kwa kuwa kina watu wanafiki na walishamdharau kwa uongozi wake dhaifu lakini yeye aliwapa vyeo bila ya kuwajua unafiki wao.

18 comments:

  1. Ndugu zangu watanzania tufanye kazi. Jana nimeangalia CNN 'Fututre cities' nimepata aibu kuona jinsi warwanda wanavyoisafisha kigali na kuwapa waatoto wao 'one child, one laptop'
    Licha ya kuangalia siasa TUFANYE KAZI!
    tuache uvivu, wanasiasa walio wengi ni waongo.Ona huyo mzee,Mpendazo, mara ccm, mara ccj, mara chadema. Ona Slaa ccm sasa chadema.
    Ona nape CCJ, CCM ataishia SISIHApa.
    Tuache malalamiko, tufanye kazi nchi yetu bado ni bomba! Mlioajiliwa acha kusoma magazeti wakati wa kazi, huu ni unyonyaji wa pesa za umma. Atakayeingia ni huyohuyo, 'the difference is the same' wote ni wapenda madaraka na pesa. Chapa kazi utunze familia yako. Mtakaonipinga haya,mtaula vumbi!

    ReplyDelete
  2. Hapo Umenena Dokta Ng'otzi, wanasiasa hawana uzalendo wala dhamira ya kweli ya kutuletea maendeleo ya kweli. Rwanda nchi iliyokuwa katika vita muda mrefu, iko mbali sana kimaendeleo. sisi na "viongo" wetu tunabaki kudanganyana. afadhali kila mtu aangalie ustaarabu wake. nchi imewashinda lakini kila mmoja na familia yake asikubali kushindwa maana ni aibu

    ReplyDelete
  3. Nape sio mtoto wa mzee Mnauye,ni mtoto wa mgongoni,hivi baba yake ni nani?yawezekana naye sio Mtanzania kwani mama yake wakati anaolewa kwa mzee Mnauye alikuja naye mgongoni.

    ReplyDelete
  4. Mi c kubaliani na Dr Ngo'tzi kwa %100. unajua kuna suala la Micro economics hili una deal na masuala ya uchumi individual ila kuna Macro economics hili una dili na masuala ya uchumi kitaifa. Dr utakuwa mbinafsi kama wewe mambo yako safi na hujali jamii inayoteseka kwa kuwatetea kupitia habari au mawazo na kukemea ufisadi na ubotevu wa rasilimali. nakuomba hebu pitia ripoti ya CAG kwenye mtandao uone halmashauri zinavyo tafuna hela za walipa kodi(kodi yako), nami niliona jana CNN kuhusu ruwanda, Kagame c mchezo ana utashi wa uongonzi na upendo wa wananchi, wame funga optic cable kwa mawasiliano, uwezi kufananisha Kagame na Kikwete ama Mkapa. Kagame ni Mzalendo wa kweli. tunazo Rasilimali za kumwaga hapa TZ. ila tuna viongozi mabomu. Huduma za Afya, Elimu, Urai zote hutolewa chini ya kiwango sana. Tatizo ni Mfumo wa uongozi. hebu tuwe na uungwana na kuweka mbali ubinafsi tuwapiganie wasiona uwezo na umaskini ili tuwakwamue kwa kubadili chama. tusimhukumu mtu ama chama kabla hajatenda. waliona madarakani tayari wameshindwa. tuwapiganie umma c ubinafsi. ila kila mtu afanfanye
    kazi kama vitabu vya dini vinavyo sema asanteni

    ReplyDelete
  5. Dr.Ngozi maneno mazito sana hayo, i salute you..

    ReplyDelete
  6. Tuna tatizo kubwa katika nchi hii, tuna chama cha CCM chenye mtandao mkubwa, na kilichotawala kwa karibu miaka 50, kimefanikiwa kuifanya nchi iwe na utulivu lakini hatujapata maendeleo ya kuridhisha na kimedhoofishwa sana na ufisadi na kwa upande mwingine tuna Chadema, chama ambacho kinaendesha na watu wachache kama kampuni binafsi, rasimilimali za chama hichi zinamilikiwa na kuliwa na watu wachache, conflict of interest za kutosha na hakina mtandao wa kutosha nchi nzima, hivi tumelogwa? ukisubiri yeyote kati ya vyama hivi vikufanyie lolote unapoteza muda wako, fanya kazi kwa bidii na maarifa uifanye jamii yako iishi maisha mazuri leo,kesho na kwa miaka mingi ijayo.

    Wanasiasa wote baba yao ni mmoja, sio Dr.Slaa wa JK, Sio Lowassa wala pacha wake Mbowe, wote hawa hawana lolote la kukufanyia Mtanzania, chukua jukumu, tumia akili yako, ifanikishe jamii yake.

    ReplyDelete
  7. Binadamu wameumbwa kila kukicha akili na mawazo yao ni kutafuta riziki zao kwa kusema uongo,kufatilia mambo ya watu, kuzua
    kufitinisha na kulalamika maisha magumu, na kutaka kipato kikubwa bila kuhangaika, kila kukicha kazi yako ni uzushi na kushabikia mambo ya uongo. Hao watu wa siasa ndio riziki zao ziko ktk kusema uongo na kuwahadaa watu ili wawasikilize na kuyaamini maneno yao,wewe na akili zako uchwara unataka dezo na kukubali kila pumba unashabikia mwisho wa siku unalalamika huna chakula, ada ya watoto nk, poleni sana nakubaliana na kauli yako Dr,Ngozi watu wengi ni wavivu

    ReplyDelete
  8. Siasa lazima ziwepo, ila zinatakiwa zisiwe za kushibisha matumbo yao walio madarakani.Inapaswa wawe na uchungu wa kimaendeleo wa nchi yao. wakibadili mitazamo yao nchi itafika mbali.

    alafu swala la amani ni asili yetu watanzania hakuna mbwa yeyote aliyetufanya sie tuwe hivi tulivo isipokua neema za mungu kwa nchi hii.

    ReplyDelete
  9. Bado hatujafika kwenye siasa hizo, siasa zetu hapa ni ajira tu, viongozi wetu wa kisiasa wapo pale kwa sababu wanataka waingize mapato, siasa zetu hazijabase kwenye imani bali matumbo yao na familia zao.

    Tanzania viongozi wanahama vyama sio kwa sababu chama hakina muelekeo anaohutaka bali ni kwa sababu kakosa cheo, tumeona hilo kwa dr.Slaa alipokatwa jina lake kugombea Ubunge kupitia CCM, leo hii utamsikia Dr.Slaa akilia kwa uchungu namna serikali inavyotoa mishahara isiyo fair lakini nyuma ya pazia yeye na mwenyekiti wake wanajitafunia tu pesa za chama chao, yeye mwenyewe anajikatia mshahara iliyo fair lakin kwenye chama chake anajikatia pande la Million 7 wakati mtumishi anayemfuatia ana Laki 6 tu,kama hauwezi kutenda fair leo utatenda ukiingia ikulu?..the beautifu one is not yet born, Mtanzania komaa na familia yako, uwe na maisha unayoyahitaji, vinginevyo kalaghabao.

    ReplyDelete
  10. Mtu hazuiwi kusema chochote atakacho maana tuna uhuru wa kuongea iwe sahihi au pumba, kote ni kuongea.Hivi hao wanaoitwa wavivu wanapanga foleni kwa nani? pia ukisema watu wasisome magazeti , wewe ulijuaje kama hukusoma habari hii ktk gazeti?halafu chukua ktk hali ya kawida, wewe kama una viatu vyako kila ukivaa mara kisigino kimetoka, umekipeleka kwa fundi mara kadhaa bado hakifai, si utanunua kipya ili angalao upumzike kidogo? hali kadhalika chama kishaonekana kulegalega , achana nacho chagua wengine nao tuone utashi wao ukoje, hayo mambo ya kung'ang'ania hao hao nani anaumia? kwani nani kasema (CCM) wana HATI MILIKI YA NCHI HII? walikaa wapi kikao na MUUMBA akawambia " NINAWAUMBIA TANZANIA MTATAWALA NYIE HADI KIAMA" kila aliyeko amadrakani alikuta watu akajifunza akaweza, halafu nikuambieni inategaemea na uzalendo wa kweli wa mtu, Kagame wa Ruandwa ndiye alipanga mpango wa kutungua ndege iliyoua marais wawili mwenyewe akiwa Uganda, lakini kwa kuwa alikuwa na uzalendo,alipoingia madarakani akaondoa ukabila,maana ndo ulikuwa unasumbua, na mambo anayoyafanya sasa pale kikweli kweli yamefunika ule uasi, tofauti ya hapa Tz kule mtu kuelimisha watanzania tu kwa maneno kuhusu hali ya nchi ilivyo,hana hata mbua mkononi mwake, anaambiwa anachochea vurugu, maskini wtz, tunaridhika eti na amani na utulivu wa CCM, mdomoni tunatamka amani moyoni tunanung'unika maisha magumu, amani iliyopo tz ni mwenyezi Mungu ametufunika, na sio chama fulani msidanganyike, na kunung"unika ni dhambi bora uwe wazi ujulikane kuliko kuwa wanafiki, unafiki huzaa uasi na kuingia msituni, lakini mtu anayesema hisia zake mbele ya umma kila mtu anasikia wala hana lawama hata mbele za Mungu, kwanza nani haoni kinachoendelea TZ, kiko wazi tu na kazi tunafanya ktk mazingira hayohayo magumu, watoto wetu wanasoma ktk shule hizo hizo wanazofundishwa mambo ya computer wakati majengo yenyewe ni hoi.

    ReplyDelete
  11. Basi tufikiri kumtafuta mwanasiasa aina ya Kagame...kama kila mtu atatulia,no doubt atatokeza Lowassa,mara nyingi nimefikiri anapingwa sana kwa sababu he would have a great many greedy individuals wetting their pants!!!

    ReplyDelete
  12. Mtowa maoni ya ya mada ya uvivu sijui kaitowa wapi hiyo kauli labda angefafanua zaidi wananchi wafanye nini wakati viongozi tulionao ndio hao ambao hawana uchungu na nchi kazi yao kubwa ni kufuja mali za nchi na kujilimbikia mali wakati wanachi wao wanaishi kwa shida kubwa sana.Tanzania tuna maliasili nyingi sana kulinganisha na nchi nyingine za Afrika lakini utekelezaji wa mambo kwa viongozi wa nchi ndio tatizo kubwa sana.

    ReplyDelete
  13. Maisha muhimu na siasa muhimu pia,ok ikiwa watu tutaamua kuwa busy na family ni sawa lakini hyo pesa tutatoa wapi?ikiwa mtaani hakuingiliki hakuna umeme hakuna huduma zozote za maana nchi inazidi kutafunwa tutakaa kimya mpk lini?

    Ukweli nchi haina wazalendo kabisa wapo kimaslahi zaidi,wanasiasa wote ni baba na mama m1,mimi naishi nchi moja ya middle east hii nchi haina Rais ni ya kifalme ni kweli mfalme anakula anavyotaka lakini nchi ina maendeleo ya hali ya juu wapo series kwa kila kitu nchi inafata sheria,lakini kwetu nchi ya Demokrasi haina faida yyte viongozi wizi wanakula mali za umma,Mahakama hazifanyi kazi,Taasisi za kuzuia rushwa ndio wala rushwa wakubwa tutafika lini hali hii.Viongozi wote matajiri,,,,Mungu Ibariki Tanzania huenda hata watoto watapata nafuu

    ReplyDelete
  14. Hata kama kweli Nape alikuwa muasissi wa ccj,hivi nyie waandishi mnashindwa kumuuliza huyo Mpendazoe wakati akianzisha ccj alikuwa hajaiona chadema. Nyie wadanganyika ni wapumbavu sana mnapakwa mafuta na wanasiasa ili mtafunwe vizuri. Mpendazoe uliishachezea hela chooni ikatumbukia

    ReplyDelete
  15. Mpendanzoe unaonesha ni jinsi gani usivyo mtunza siri. Kama ulivyokuwa CCJ pamoja na Nape na unatoa siri zake inamaanisha ukihamia chama kingine utaendelea kutoa hata siri za CHADEMA. Naishauri CHADEMA kuwa mwangalifu sana na MPENDANZOE kwani ni mnafiki.

    ReplyDelete
  16. "Hivi hao wanaoitwa wavivu wanapanga foleni kwa nani? pia ukisema watu wasisome magazeti , wewe ulijuaje kama hukusoma habari hii ktk gazeti?"


    Wewe unaonesha huna akili nyingi, Dr. Ng'otsi ameseme tusisome magazeti WAKATI WA KAZI hajasema tusisome magazeti kwani tunahitaji habari katika maisha. Nilivyomuelewa mimi ni kuacha uvivu hata kama hatupangi foleni kwake huu naona ni ushauri wa bure kwani ukifanya bidii wala hata shilingi hatokudai kwani jamaa anazo tayari.
    Cha kushangaza ni kwamba wakati maisha ni magumu wapo watu wanasonga mbele kila kukicha, wengi walikuwa wameanzia kuuza mafuta sasa wanamaduka. Kuhusu umeme kuna vijana wengi wamenunua solar na maisha yao yako MURUA kabisa.
    Kwa upande mwingine siamini kuwa serikali pekee inamtoa mtu umasikini. Mbona kuna tofauti kati ya moshi na sehemu nyingine? wengi wamebaki kulalama : oo hawa wezi? nk...Ndiyo; wapo wengi wezi lakini walio wengi ni watafutaji, wanauza maembe hadi nairobi, wanauza mitumba hadi kibera. Wewe usibaki kulalama fikiri kidogo upate ufumbuzi, wanasiasa wanapita, siku wataondoka msife moyo ndugu zangu kuacha kutafuta! hata wasomali, iraq, Afganistani na sehemu nyingi wanakoteseka watu kamwe hawaachi kujishughulisha.
    Kikwete ataondoka halafu atakufa, CCM na Chadema navyo vitakufa usikubali kizazi chako kife miaka yote.Jitahidi!
    KAMA HUTAPANGA FOLENI KWAKE BASI UTAPANGA CHUMBANI KWAKO UTAKAPOUMWA NJAA.

    ReplyDelete
  17. Hizi nyingine ni siasa, wewe umepewa nafasi kama ya mpendazoe, ndiyo lazima uongee ili uonekane unafanya kazi, ukikaa kimya we unategemea chama kitaendelea kukuhifadhi wakati input yako ni ndogo. Survival ya chama ni kukikosoa kingine zaidi kipendwe chenyewe, sio ajabu. Waache washindane si tuendelee kupata ukweli au uongo. Ila swala la kwamba kila moja akae ndani kidogo linaniuma, kwa bwana NG'OTZ, kwa haraka inawezekana kiasi fulani anajitosheleza, akumbuke wengine wengi bado wako nyuma. Utachapa kazi kwa ajili ya familia yako sawa, lakini kama hali hiyo ya kuchapia kazi kwa ajili ya familia yako ni ngumu bado utakimbilia kujua hivi anayetawala mbona ameliacha hili haoni hali inavyozidi kuwa ngumu. Naunga mkono swala la kutosoma magazeti ukiwa kazi na kwamba huo ni wizi wa fedha za uma, ingawa tatizo kama mfanyakazi mwenyewe hali ikiwa ngumu atalazimika kufuatilia magazeti kufahamu kama kuna unafuu umetangazwa. Ng'otz, think of long run of all people concentrating with only their families and don't think of how things goes around in a street, village, ward, district, region and national, me I think that shouldn't be like that. See many countries are even forced to understand how other countries are going on

    ReplyDelete
  18. watoa maoni wote nadhani mmepitiwa au wengine mmelewa ujirani na mafisadi anayetetea maovu yanayofanywa dhidi ya lasilimali na amanai ya taifa huyo si mzalendo anafanana na wote wanaotuhumiwa kwa ubadhilifu fedha za umma ni kwa ajili ya watz si kwa baadhi ya manyang'au wachache wanaotaka kuvuruga amani kwa sababu wameshiba na watoto wao wanasoma nje ya nchi wakati ukuta wasishindane nao

    ReplyDelete