11 May 2011

Nape apania kujibu mapigo ya CHADEMA

Na Gladness Mboma

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nauye amesema leo atajibu mapigo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa
kuanika waraka unaoonesha ufisadi mkubwa wa viongozi wake kwenye mkutano ambao utafanyika mkoani Singida .

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana akiwa njiani kwenda Singida, Bw. Nnauye alisema kuwa kilichozungumzwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa kuhusu kupata waraka wa siri wa CCM zinazoelezea sababu za chama hicho kushuka umaarufu ni uzushi ambao amezoea siku zote.

Bw. Nnauye alikuwa anazungumzia 'waraka wa siri' aliodai kuwa nao Dkt. Slaa kwenye mkutano wake mkoani Rukwa, ukieleza sababu chama hicho kupoteza mvuto kwa wananchi, lakini akiuponda kuwa hauzungumzii hali ngumu ya maisha ya Watanzania.

"Mimi ninachoweza kuzungumza ni kwamba hata sisi CCM tuna waraka mkubwa unaoonyesha ufisadi mkubwa wa viongozi wa CHADEMA na ninakwenda kuuanika kwenye mkutano Singida leo na asubiri mapigo yake na siyo huo wa kutengeza," alisisitiza.

Alisema kuwa atazungumzia yote yaliyoko katika waraka huo, na mambo yote atayaweka hadharani na kusisitiza kwamba asipende kuchokoza CCM wakati wanayo mabaya yao.

Bw. Nauye alisema kuwa pamoja na madai yote ya CHADEMA kuwa wamenasa waraka wa siri wa CCM, wao ndio mafisadi namba moja na kwamba chama chao ni masikini, lakini bado wanakifanyia ufisadi mkubwa.

"Dkt. Slaa anatushangaza anapodai kwamba amekamata waraka wa siri, mbona kila kitu kipo hadharani na yote tulikwishazungumzia, tunapenda afahamu kwamba CCM hata siku moja haifanyi maamuzi ya siri,  hiki si chama cha siri ni cha Watanzania," alisema.

Alisema kuwa wenzake wamemdanganya ni waraka wa siri ambao wameutengeneza wenyewe na kusisitiza kwamba hakuna siri inayozungumziwa hadharani, kwani wakati wakiwa Dodoma, Zanzibar, Dar es Salaam, Iringa, Kibaha na pia walipozungumza na wahariri wa vyombo vya Habari walizungumza kila kitu bila kificho.

Bw. Nnauye alisema kuwa Dkt. Slaa anaweweseka hasa baada ya kukosa agenda ya kuzungumza katika mikutano yake na kuanza kuibu uongo mbao hauna manufaa yoyote kwa Watanzania na kumtaka kutoa siri ya waraka huo hadharani.

"Hakuna siri yoyote tunayoongea hadharani, ninachomuomba atoe waraka huo wa siri hadharani na tuone kama yote yaliyomo hayajazungumzwa, Slaa aache uzushi wa kuwataka kuwahadaa Watanzania wamuone kuwa ni mtu wa maana wakati si lolote na si chochote," alisema.

Jana gazeti ili lilimnukuu Dkt. Slaa akisema kuwa CCM wanasema wanajivua gamba, basi na wao CHADEMA watawavua nguo kwa kuwa uwezo wao wa kuwatumikia Watanzania umefikia mwisho na kuitaka iwapishe.

Alisema kuwa pamoja na waraka huo kupigwa mhuri mkubwa wa neno 'siri', wao CHADEMA wameupata na ndani yake CCM imeeleza sababu zilizosababisha kushuka kwa umaarufu wake, miongoni mwa Watanzania, lakini akasema kuwa chama hicho kimegundua mapungufu hayo kikiwa tayari kimechelewa, kwani wananchi wameonesha kila dalili ya kukichoka.

11 comments:

  1. Nape, Slaa atakugaragaza hadi utapoteza umaarufu wako kama Kikwete, Lowassa, Rostam Chenge. Acha kushindana naye we bwana mdogo. Mafisadi wa CCM wamekuweka hapo kwa kuwa wao wamemshindwa. Nakuonea huruma sana.

    ReplyDelete
  2. NAPE UMECHEMKA, NILIVUTIWA NA KASI YAKO YA KUZUNGUMZIA MAGAMBA MMEWAPA SIKU 90 WATOKE KATIKA CHAMA THEN KATIBU WAKO MKUU ALIKUPINGA HADHARANI KUWA KATIKA NEC HAKUKUWA NA AJENDA YA KUWAPA MAFISADI SIKU 90, KUMBE ULIZUSHA?, AU ZILIKUWA CHUKI ZAKO KWA LOWASA?, AU WAKUU WA CHAMA CHAKO WANAWAOGOPA MAGAMBA COZ WATAMWAGA MBOGA?, KATIKA HILI MMEPWAYA, MNAPINGANA HADHARANI, HUYU ANASEMA HIVI, YULE KESHO ANAKANUSHA, KAMA ISHU YA DOWANS, SITTA NA NGELEJA, NA WEREMA HUYU TULIPE,HUYU MKILIPA PATACHIMBIKA. MMETUONGOZA KWA HADAA NA WAZAZI WENU KWA MUDA MREFU, MOLA AMETUONEA HURUMA JUU YA MATESO YENU CCM KWETU WANANCHI, AMETULETEA DK WILBROAD PITER SLAA, HAMUNG'UNYI MANENO WALA HARUDI NYUMA KAMA NYINYI MAGAMBA,MAFISADI,NA WEZI. HAUNA CHA KUONGEA NAPE MBELE YA MPIGANAJI DK SLAA NA WATZ WA SASA WAKAKUELEWA, CCM MMECHAFUKA NA MNALEA UFISADI. AM DONE!.

    ReplyDelete
  3. Nape kaza mwendo achana na hao wanaoongea magazetini si na wao waongee wapigwe na kamera tuone kama wanao ubavu kama sio woga wa kukuponda katika maandishi na wao waonekana tuwasikie. Songa mbele, nena usiogope hujawekwa hapo kwa ajili ya mtu fulani watumikie wananchi wa Tanzania usiogope maneno ya kwenye magazeti. Songela zigizigi.

    ReplyDelete
  4. Npe mtoto mdogo wa mafisadi wewe ushawekwa na mabwana zako Slaa atakulipua hadi upoteze mvuto achana naye huyo mkongwe kwenye siasa wewe.

    ReplyDelete
  5. Du, yaani siamini, hivi kweli kuna watu na akili zao bado wanawatetea CCM (Chama Cha Mafisadi). Ok inawezekana ni vitoto au vidugu vya hao mafisadi. Poleni sana kwani watanzania wameshaamka na wanakaribia kuikomboa nchi yao. VIVA SLAA. ALUTA CONTINUA. Hongera Slaa kwa kumlipua pia mtoto wa mkulima, yaani kijiji chote yeye tu ndo ana umeme wa SOLA, anatembelea gari la NUSU BILIONI. PINDA we Slaa is coming to you and be very very afraid......

    ReplyDelete
  6. Tanzania,nafikiri imefikia hatua ya vyama vyote vya siasa kujadiri masuala ys ubunifu ya kusaidia wanachama wao ili wajikwamue na umasikini,km miradi ya kuingizia chama pesa na siyo vijembe na majungu,shindaneni kwenye vipato siyo maneno.sisi hatuitaji siasa,nafikiri itakuwa raha zaidi tukisikia chama kina mradi fulani kinategemea kupata kiasi kizaa na kuwapatia wanachama wake ajira

    ReplyDelete
  7. Kwa mchangiaji hapo juu, nakubaliana na maoni yako kuwa vyama vishindane kwa miradi ya ajira kwa wananchi. tatizo ni kwamba CCM imeshindwa kufanya hivo kwa miaka 50 sasa. Ilichofanya ni kuwatajirisha makada wake na watoto wao, kama akina Ridhiwani, nape. Sasa ili vyama vingine vipate nafasi ya kuwapa ajira watanzania, lazima uozo huu uanikwe hadharani ili wapiga kura wajue na wakinyime kura.

    ReplyDelete
  8. Jamani mnaoelewa kimombo someni hapa.
    Kuwaambia watu kuachana na CCM haitoshi, tuwahimize kudai uchaguzi wa kisasa na ulio nafuu usio na wizi pia,2015 siyo mbali.
    Anglieni masikini wenzetu hapo:

    Hello, I am the 2010 Automated Election Machine.

    I would like to introduce myself. My name is Precinct Count Optical Scan but you can call me P.C.O.S.

    For the first time in history, the Philippines will be embracing technology and will transform greatly the electoral system of the country. I’m so glad to be part of this history.
    visit me automated election to see more! hehehe! tuamke!
    I’m honored to be one helping the Philippines move away from the known flaws of the old ways. I am proud to say goodbye to dagdag-bawas.

    Why am I here? What can I do to make your election accurate, easier & faster? What can I do to protect your ballot and guarantee that who you voted for will truly win?

    * You will not need to count and canvass votes for your local and national elections. I will do it for you. There will be no room for mistakes.
    * I will limit/remove flying voters. If a precinct has 400 registered voters, I will only accept 400 voters.
    * I will not accept overvoting. This means that if you voted for two candidates for president, I will not count them. I will count the rest of the ballot though, so your votes will still be counted for other positions.
    * Since I will do all your counting and canvassing, we will not tire our teachers for days and weeks.
    Hehehe,sisi mwezi he!

    ReplyDelete
  9. Nape tulikuamini sana wakati unaanza mbio zako dhidi ya mafisadi wa nchi hii. Lakini nadhani umeshindwa kujua ni kwa nini chadema wanapata cha kuzungumza. Kwa kukusaidia tu kijana mwenzetu ni kwamba kaza buti kupambana na mafisadi kama ulivyotuhakikishia mwanzo, hapo utakuwa umewamaliza CHADEMA. Lakini ukijiingiza kwenye malumbano hakuna utakachoshinda la zaidi utapoteza na utapwaya sana. Epuka kuongeza maadui. endelea na mafisadi ukimaliza anza na Dr. slaa kama utakuwa na muda na uwezo.

    ReplyDelete
  10. "tunapenda afahamu kwamba CCM hata siku moja haifanyi maamuzi ya siri, hiki si chama cha siri ni cha Watanzania,"
    Nape asidhalilishe watz, CCM sio chama cha watz bali ni chama cha mafisadi na magamba.

    ReplyDelete
  11. Nape kaza kamba kaka, ni walewale waropokao na wakosao cha kufanya kama slaa, kushindwa kwake kusifanye aweweseke, naona uzee unamsumbua, ni kipi walichotoa wao kusaidia wananchi, zaid ni kuropoka tuuuuuu... slaa aongee.... nape anyamazeeee... kunya anye kuku... akinya bata kaharisha. Jeff wa ukweli-morogoro

    ReplyDelete