Na Edmund Mihale
HATIMAYE Shirika la Umeme (TANESCO) limekiri kuwa na mazungumzo ya kununua umeme wa megawati 112 kutoka kwa kampuni iliyonunua mitambo ya
kuzalisha ya umeme ya Dowans, Symbion Power kutoka Marekani
Taarifa ya TANESCO iliyosainiwa na Meneja Mwasiliano wa Shirika hilo, Bi. Badra Masoud Dar es Salaam jana, ilikiri kuwapo kwa mazungumzo hayo ambayo yanakwenda sambamba na mchakato wa kununua mitambo mipya ya umeme.
Katika taarifa hiyo Bi. Badra alieleza kuwa uamuzi huo wa TANESCO unatokakana na ukarabati katika visima vya gesi katika kisiwa cha Songosongo, ambao umesababisha uzalishaji wa umeme katika mitambo ya Songas kusimama na hivyo kusababisha mgawo mkali wa umeme.
Gesi hiyo hutumika kuzalisha umeme kwenye mtambo wa Ubungo, Tegeta na Songas na ukarabati huo umesababisha upungufu wa megawati 350 kutoka kwenye gridi ya taifa.
Pia Tanesco imelazimika kutoa taarifa hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, Bw. John Mnyika kutoa taarifa akimtaka Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha wote waliosababisha mgawo wa umeme, akiwamo Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja.
Bw. Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Ubungo, alisema hakuna haja tena ya kukodi mitambo ya dharura, badala yake serikali kupitia TANESCO ingenunua mitambo mipya ili kuepuka kuingia katika ufisadi kama wa Richmond.
Alieleza kuwa TANESCO imelazimika kufanya mgawo kwa mikoa iliyounganishwa katika Grid ya taifa kwa siku nane mfululizo kuanzia tarehe 19 hadi 26 Mei, mwaka huu.
Ilieleza kuwa shirika limeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kukabiliana na upungufu wa umeme nchini ikiwemo kukodi mitambo ya kuzalisha umeme na kuanzisha miradi zaidi ili kuongeza vyanzo vya nishati hiyo.
Ilieleza kuwa kampuni 15 zilijitokeza kutaka kukodisha mitambo ya Megawati 260, lakini kati ya hayo tatu zilizorudisha fomu za kuonesha nia ya kukubali na baada ya mchanganuo na kampuni moja ndio iliyokidhi vigezo na ina uwezo wa kuzalisha megawati 70 na mitambo hiyo itafungwa Mkoa wa Tanga eneo la Majani Mapana.
Ilieleza kuwa mitambo ya zamani ya mafuta ambayo ipo TANESCO Ubungo ilisimamishwa kwa kipindi kirefu na haiwezi kutumika kwa sasa kwa kuwa ilishaharibika na vipuri vyake havipatikani kwenye soko na teknolojia yake imepitwa na wakati.
Ilieleza kuwa gharama za kuikarabati mitambo hiyo ni kubwa ukilinganisha na gharama za kununua mitambo mingine mikubwa na mipya.
Kumekuwapo na maoni mbalimbali ya wadau wakiitaka TANESCO kukataa maombi ya Symbion kuiuzia umeme, kwa madai kuwa kinachofanyika ni kiini macho kwa kuwa mradi huo ni sawa na ule wa Dowans na Richmond uliokataliwa na bunge, serikali pamoja na wananchi.
Kulingana na madai hayo ambayo kwa nyakati tofauti yamekuwa yakikanushwa na TANESCO, ni kuwa kila unapoibuka mgawo wa umeme, suala la Dowans hujitokeza, hivi sasa likiwa limejitokeza kwa jila la Symbion Power.
Gazeti hili liliwahi kuandika habari kuwa kwa muda mrefu kulikuwa na hujuma miongoni mwa wafanyakazi wa TANESCO zilizofadhiliwa na mmoja wa wafanyanyabiashara wakubwa nchini, ili kuhujumu baadhi ya miundombonu na kusababisha mgawo wa umeme, kwa lengo la kushinikiza shirika hilo ama kununua umeme au mitambo anayohusishwa nayo.
HAKIKA NCHI YETU HII INAENDESHWA KWA RIMOTI YA WATU FULANI HIVI KWELI INAINGIA AKILINI TANESCO WALISHATANGAZA MGAO WA UMEME MWEZI MMOJA KABLA MPK LEO MGAO UMEANZA NDIO MAZUNGUMZO YANAFANYIKA NI YA NINI? WAKATI SIKU 4 ZIMESHAPITA BADO SIKU 4 WACHA TUKAE KIZANI INAONYESHA WATU HAWAKO SIRIASI NA KAZI ZAO,AU NI HUJUMA AU NI DHARAU KWA WATU WA CHINI WASIO NA UWEZO WA KIMAISHA MAANA WAO HATA JENERETA WANAZO WANA UMEME WA JUA NK,HAWA WATU WALIKUWA WAPI SIKU ZOTE HIZO? HAPA NI MCHEZO WA KUIGIZA TUNATIANA MCHANGA WA MACHO. WAWAJIBISHWE WOTE WANAOLETA USANII NA UZEMBE
ReplyDeleteTunachohitaji ni umeme upatikane, hizo sasa za ufisadi hazina mpango wowote kwa wananchi zaidi ya watu kutafuta umaarufu wa kisiasa. Tuwaache Tanesco wafanye kazi yao
ReplyDeleteSawa umeme upatikane unasahau mitambo hii ilipoletwa mpk kuwashwa ilikuwa tayari maji yamejaa mtera mwaka 2006? na leo utapita muda wa dharura makubaiano bado haiajisha ndio wasiwasi wangu sio siasa hao wana siasa wanaandamana kila kukicha hapa ni hujuma na 10%inagomba
ReplyDeleteTANESCO FANYENI KWELI TUONDOKANE NA AIBU HII NA KERO HII IISHE.WAWEKEZAJI WANASHINDWA KUWEKEZA MPK HALI ITAKAPO KUWA SHWARI!!SIASA WAACHIENI WANASIASA NYIE NI UMEME KWENDA MBELE
ReplyDelete