Na Rehema Mohamed
WANANCHI wa eneo la Makongo Juu ambao wamejenga katika maeneo yasiyo rasmi wametakiwa kuanza kubomoa majengo yao ikiwa ni hatua ya awali ya
kupanga upya makazi ya eneo hilo.
Upangaji upywa wa eneo hilo unaaza na upanuzi wa barabara ambapo wananchi waliojenga katika hifadhi za barabara wametakiwa kuvunja na kupisha mita 10 kwa kila upande wa barabara.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka wakati akizungumza na wananchi waeneo hilo kuhusu uboreshaji wa makazi ya eneo hilo.
Prof. Tibaijuka alisema kuwa upangaji upya wa eneo hilo utazingatia ramani iliyochorwa mwaka 2005 ambapo miliki 2,220 za viwanja zilitambuliwa.
Prof. Tibaijuka alisema kutokana na uboreshaji wa eneo hilo baadhi ya maeneo yatatwaaliwa na serikali kwa ajili ya kuweka huduma muhimu kama kituo cha afya, soko na kituo cha polisi ambapo wamiliki wa viwanja hivyo watalipwa fidia.
"Kutokana na hatua hii viwanja vyote vitatambuliwa upya kwa mujibu wa ramani ya awali, kama ikibainika watu zaidi ya mmoja mmejenga ndani ya kiwanja kimoja itabidi wakubaliane mmoja abaki, kwani haiwezekani kumilikishwa wote," alisema Prof. Tibaijuka.
Watakaobakiwa na viwanja baada ya ramani kusomwa upya, watatakiwa kujenga nyumba za kisasa na wasiokuwa na uwezo huo Shirika la Nyumba la Tifa (NHC) litajengea nyumba hizo kwa makubaliano maalumu.
"Nyumba zinazoependekezwa kujengwa hapa ni za kisasa kama maghorofa kuanzia nne hadi tano, ili wananchi wengi waweze kupata maeneo ya kuishi, kama mnavyoona idadi ya watu imeongezeka tofauti na awali," alisema.
Alisema kuwa uboreshaji wa eneo hilo utawezesha wananchi wake kupata huduma muhimu kwa urahisi kama maji ambayo limekuwa tatizo sugu.
Wakati huo huo aliwataka wananchi waliojenga katika viwanja vya Tanganyika Parkers kubomoa nyumba zao kwa kuwa viwanja hivyo havikutengwa kwa ajili ya wananchi kujenga makazi.
Aliongeza kuwa hakutakuwa na faraja kwa wananchi wa Makongo Kaskazini waliojenga karibu na kambi ya Jeshi.
"Hakuna faraja kwa wananchi wa Makongo Kaskazini, rais pekee ndiye mwenye mamlaka ya kubadili umiliki wa ardhi na si rahisi kuchukua eneo la jeshi kugawa kwa wananchi kwa sababu ni hatari kukaa karibu na kambi, hivyo ni bora mkatafuta maeneo mbadala ya kuishi mapema," alisema.
Haya kumekucha watu wa Kigamboni wamewekwa rehani tokea 2008 na hawajajuwa hatma yao hawapati mikopo,hawauzi viwanja tena na wala hawaruhusiwi kujenga na mpk sasa wamekaa rumande isiyo na majibu leo tena tunahamia makongo sijui itakuwaje maana miradi hii haiko wazi.mfano Kigamboni mradi wote unatakiwa zaidi ya trillion 12 hatujaambiwa zinatoka wapi, na watu mpk leo hawajafanjiwa tathmini haijaambiwa watalipwaje hivi nchii hii tuna nia njema kweli lakini inakuwaje watu wanaishi kama wakimbizi? mtu keshastaafu kajikita sehemu amalize umri wake leo unamtoa hujui anaenda wapi!!tuwe wa kweli isiwe mkajiona mambo yenu swafi lakini wengine wanateketea
ReplyDeleteThat is the cost of development. Accept change!
ReplyDelete