Na Zahoro Mlanzi
TIMU ya Simba, inatarajia kuondoka nchini kesho usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la Misri kwenda nchini humo wakiongozwa na Muhsin Balhabou, ambaye ni
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kwa mantiki hiyo, timu hiyo inaweza kutua jijini Cairo usiku wa manane endapo itaondoka na ndege itakayotoka jijini Dar es Salaam majira ya saa moja usiku na kuendelea kitendo kitakachowafanya wakazi wa huko kuishtukia timu hiyo imeshatua nchini mwao.
Timu hiyo inatarajia kucheza mchezo wao wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco Jumamosi kwenye Uwanja wa Petrosport Jijini Cairo kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Misri.
Akizungumza Dar es SAlaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeshawatumia majina ya waamuzi wa mchezo huo.
"Licha ya kutuma majina hayo, kama tunavyojua timu hiyo ipo kambini Zanzibar na taratibu za safari zinaendelea ambapo katika safari yao itaongozwa na Muhsin Balhabou na wataondoka Jumatato usiku (kesho) na Egpty air," alisema Wambura.
Akizungumzia suala la wachezaji Mbwana Samatta na Patrick Ochan kuichezea timu hiyo, alisema waliwaomba CAF kuwapa ufafanuzi juu ya hilo kabla ya Ijumaa na kwamba wana imani ndani ya siku mbili watapata taarifa kamili.
"Ijumaa wafanyakazi wa CAF hawafanyi kazi na mchezo ni Jumamosi, hivyo kesho (leo) au keshokutwa (kesho), tunaweza tukawa na jibu kamili juu ya suala hilo ila kwa sasa wametutumia majina ya waamuzi tu," alisema Wambura.
Ofisa akizungumzia sula mchezo huo kuchezeshwa na waamuzi wa Misri, alisema hakuwezi kukawasaidia Waydad kwaniCAF wamefanya hivyo ili kuzisaidia klabu hizo kwa kuwa kama waamuzi wangetoka mbali zaidi wangewajibika kuwalipa.
Alisema kuwachukua waamuzi kutoka ndani ya Misri gharama yake ni tofauti na kama wangechukuliwa waamuzi kutoka nje ya nchi hiyo.
Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo ni Farouk Mohamed atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Mohamed Waleed na Hassan Sherif, mwamuzi wa mezani ni Omar
Fahim huku Kamishna ni Magdy Shams El Din kutoka Sudan.
Mimi ninawasiwasi na waamuzi maana hao wote wanatoka katika nchi za Kirabu!najua wanaweza kutunyonga.
ReplyDeleteNi kweli mdau wa hapo juu.Hata mimi nahisi Waarabu watabebana
ReplyDeleteIjapokuwa ni hivo, Misri imekuwa daima na migogoro na timu za Kiarabu za kaskazini ya Afrika. Yaliwahi kutokea mapigano si mara moja wala mbili baina ya Timu Za Miisri na Algeriaa na nakumbuka hata Tunis. Ilifika hadi kuitiana mabalozi wa nchi hizo.
ReplyDelete