18 May 2011

LHRC yataka hatua zaidi waliochoma vibanda Zanzibar

Na Agnes Mwaijega

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhakikisha wale wote waliohusika katika uchomaji wa mabanda ya biashara
katika Kijiji cha Pwani Mchangani Mei 7, mwaka huu wanafikishwa mahakamani.

Pia kimetaka serikali kutolifumbia macho suala hilo na kuwawajibisha viongozi wote walioshindwa kutimiza wajibu wao kuzuia tukio hilo kujiuzulu au kuchukuliwa hatua kali na maamlaka ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jan,a Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Bw. Horald Sungusia alisema watu waliohusika katika tukio hilo lililosababisha hasara ya zaidi ya sh. milioni 200 ni 60 lakini waliofikishwa mahakamani ni tisa tu.

Alisema LHRC inataka kuona haki inatendeka ili kupoza hasira na chuki zinazoendelea kujengeka kwa waathirika wa tukio hilo kwa sababu walikuwa na vibali vyote ambavyo vinawaruhusu kufanya biashara zao.

Aliongeza kuwa LHRC kinalaani tukio hilo ambalo ni kinyume cha katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Tukio hilo ni la hatari sana na ni kinyume cha sheria," alisema.

Bw. Sungusia alisema zipo tetesi kwamba jamii ya Zanzibar ina ubaguzi ambao ndiyo unasasabaisha uhalifu kama huo kutokea hivyo kuitaka serikali kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais kuingilia kati suala hilo ili kuendelea kujenga mahusiano mazuri kati ya wananchi wa pande zote mbili za muungano.

"Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania isipoliangalia suala hilo na kulifanyia kazi, litasababisha uhasama na chuki ndani ya jaamii ambayo inaweza kusababisha mauji kama yale yalitokea Rwanda," alisema.

Alisema LHRC inataka kuona haki inatendeka ili kupoza hasira na chuki zinazoendelea kujengeka kwa waathirika wa tukio hilo.

Alisema serikli ya Mapinduzi Zanzibar ina wajibu wa kuhakikisha waathirika wa tukio hilo wanapatiwa fidia kulingana na hasara waliyopata ili kufufua mitaji yao pamoja na huduma za kijamii kulingana na mahitaji yao.

Pia kimeisistiza serikali hiyo kuchukua hatua kali dhidi ya watu au makundi ambayo yanachochoea chuki, uhasama na ubaguzi baina ya wananchi kwa kutazama kabila, dini na sehemu mtu aliyotoka.

Pia kimewataka viongozi wa dini kujitahidi kujenga jamii yenye amani, umoja, ushirikiano na kuhimiza waumini wao kuheshimu imani au dini za watu wengine.

1 comment:

  1. LHRC munashangaza kuwa ni kitengo cha sheria lakini mnakurupuka kama walevi, kwanza fanyeni uchunguzi kubaini hayo mabanda ni ya kina nani,pili angalieni lugha mnazozitumia kama vile "wazanzibari ni wabaguzi" huu ndio uvunjifu wa amani na ubaguzi, vile vile suala lenyewe liko mahakamani kwa hiyo nyinyi kama taasisi hamutakiwi kuishurutisha mahakama kutoa maamuzi yanayowafurahisha nyinyi, huku ni kukurupuka na upuuzi wa watu wajinga na kutaka sisi tuamini ni wasomi na watetezi, rudini madarasani bado munaonekana mambumbumbu wa sheria.

    ReplyDelete