20 May 2011

Kikwete kuongoza harambee Yanga

Na Elizabeth Mayemba

RAIS Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa uwanja na jengo la mtaa wa Mafia la Klabu ya Yanga, inayotarajia kufanyika
Julai 7 mwaka huu Dar es Salaam.

Jumla ya fedha zinazohitajika kwa klabu hiyo ili kukamilisha ujenzi huo kwa upande wa uwanja ni sh. bilioni tano na jengo la Mafia litagharimu sh. bilioni mbili.

Akizungumza Dar es Salaam jana Msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema walimtumia Rais barua ya kumuomba awe mgeni rasmi tangu wiki tatu zilizopita, hivyo wanasubiri majibu ili waendelee na taratibu nyingine.

"Tumemwandikia barua mheshimiwa Rais wiki tatu zilizopita, hivyo tunatarajia atakubali ombi letu ili aweze kushiriki katika harambee hiyo," alisema Sendeu.

Alisema siku hiyo ya harambee wameandaa chakula cha jioni, ambapo kutakuwa na tukio la uchangiaji wa fedha kwa klabu hiyo kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa uwanja na jengo lao.

Sendeu alisema wameona ni vyema wakamshirikisha Rais kwa kuwa ni mtu anayependa maendeleo ya soka nchini na amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo.

Alisema pia watazialika kampuni, mashirika, wafanyabiashara maarufu nchini pamoja na wanachama ambao watakuwa tayari kuchangia, ili kufanikisha ujenzi huo.

Kamati ya Ujenzi ya klabu hiyo, inaongozwa na Mwenyekiti wake, Mbaraka Igangula.

8 comments:

  1. NDUGU SENDEU NI KWELI UTAPATA PESA KWA SABABU RAISI AKIWEPO PALE LAZIMA PONJORI, SUNCHE NA KAPETO, KANJIBAI WATAKUJA KUJIPENDEKEZA SANA.

    ILA PENGINE TUSIWE WABINAFSI SANA, TUMWACHE RAISI AFANYE KAZI YA NCHI KATIKA NGAZI YA KITAIFA NA SIO KUMUALIKA KWENYE KILABU.

    ANGEALIKWA TAIFA STAR HAPO INGEKUWA SAWA.

    DONT KIP BIZE OUR PREZIDENT KWA VIJIMAMBO.

    MH. ANAKAZI NYINGI ASIJE ACHA SIFA MBAYA!!!

    ReplyDelete
  2. rais wetu anapenda sana michezo hivyo kualikwa na wana Yanga sioni kama ni jambo la kumpotezea muda. Yeye atawajibu wana Yanga najua atakubali kama muda wake utakuwa muafaka. Raisi anaweza kualikwa na mwaliko wake unategemea nafasi yake hivyo nina imani kwamba yeye kama mwamna michezo ataweza kuhudhuria hii itategemea nafasi yake kama Rais wa Nchi hii. Msiwe mnatanguliza eti ana kazi nyingi mojawapo ya majukumu yake ni hayo kwa wanamichezo, burudani nakadhalika.

    ReplyDelete
  3. hao wanaopinga ni simba wanaona wivu tu

    ReplyDelete
  4. haya bana mumeshinda msisahau kumpigia mdundiko kaumisi

    ReplyDelete
  5. Sitaweza kuja sababu nimetingwa sana na shughuli za kitaifa. Nawatakia harambee njema.

    Rais

    ReplyDelete
  6. JAMANI HUYO NI RAIS WETU SASA KWELI SIKU HIYO RAIS AKOSEKANE OFISINI ASHINDE JANGWANI? NI BORA ANGEMTEUA MWENYEKITI WA MTAA WA JANGWANI AMWAKILISHE NDIYE YUPO JIRANI ZAIDI NA HAPO.JAMES KIMARO - TAZAMA IRG.

    ReplyDelete
  7. wanasimba hawata fika wanatayarisha jeneza, sijui litakua lao au la wydad.

    ReplyDelete
  8. Dduuhh, Tarehe 7 july jeneza hilo atakuwa keshajizikia mwenyewe wakati huo tutaunganisha Harambee na arobaini yake!! Duuh poleni sana watani

    ReplyDelete