Na Mwali Ibrahim
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka anatarajia kurudiana na Mada Maugo katika pambano lililopangwa kufanyika siku kuu ya Idd el Fitr.Akizungumza kwa
simu jana akiwa mjini Morogoro Promota wa pambano hilo, Kaike Siraju alisema mtanange huo wa marudiano utakuwa wa ubingwa wa WBO wa raundi 10 ambalo litafanyika Morogoro.
Alisema ameamua kuwapambanisha mabondia hao kwa mara ya pili, baada ya pambano la awali la kufunga na kufungua mwaka kulalamikiwa na Maugo, kutokana na kuzidiwa kwa pointi moja na mpinzani wake huyo.
Siraju alisema mabondia hao tayari wamesaini mkataba ambapo Cheka, amesaini mkataba huo jana Morogoro wakati Maugo naye pia anatarajia kusaini mkataba huo.
Alisema pambano hilo ndiyo litamaliza ubishi wa kuwa nani bingwa wa halali kati ya mabondia hao.
No comments:
Post a Comment