Na Mwali Ibrahim
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka amemhadharisha, Mada Maugo kuwa asitarajie kupata ubingwa katika pambano watakalorudina siku kuu ya
Idd el Fitr ya pili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Pambano hilo la ubingwa wa UBO, linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kg. 72 ambalo litasimamiwa na Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO).
Akizungumza kwa simu akiwa Morogoro, Cheka alisema atahakikisha Maugo hafikishi raundi ya sita, ili asije kulalamika kama katika pambano la awali la kufunga na kufungua mwaka ambapo alimzidi kwa pointi na kumfanya kulalamika kuwa ameonewa.
Alisema upiganaji wa Maugo anaujua vizuri hivyo hawezi kumpa shida hata kidogo, kwa kuwa ngumi hazijui hivyo asubiri kutolewa mapema katika pambano hilo.
"Maugo hana kitu, hata kupigana kwenyewe hajui hivyo hanipi shida hata kidogo nasubiri tu kuibuka na ubingwa wangu basi," alisema Cheka.
Alisema kwa sasa pambano linalompa shinda na kushindwa kujua kama atashinda au atapigwa ni dhidi yake na Mkenya, ambalo litakuwa ni la kirafiki linbalotarajia kufanyika Juni 25 mwaka huu, Dar es Salaam na kudhaminiwa na kituo cha redio cha Times FM.
No comments:
Post a Comment