17 May 2011

CHADEMA wamvaa Makinda nyumbani

*Wataka katiba mpya imzuie spika kuwa mbunge

Na Tumaini Makene

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetaka mabadiliko ya katiba yaguse pia uendeshaji wa bunge, kikitaka spika wa bunge asiwe
mbunge wa jimbo lolote la uchaguzi na ikitokea hivyo basi ajiuzulu nafasi hiyo ya ubunge ili wananchi wake wapate uwakilishi ulio sahihi.

Hatua hiyo imedaiwa itamsaidia spika na yeye afanye kazi zake kwa uhuru bila kupendelea chama chochote bungeni, kikisema mabadiliko hayo yaanze sasa wakati huu Spika Anne Makinda, kwa madai kuwa ameonesha dhahiri uwezo mdogo na kupendelea chama tawala, ambacho yeye ni kada mkongwe.

Kauli hiyo na nyingine zilitolewa katika Mkutano wa hadhara wa chama hicho , uliohutubiwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho katika Viwanja vya National Housing mjini Njombe jana.

Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema, Bw. Freeman Mbowe na Naibu katibu Mkuu, Bw. Zitto Kabwe kwa nyakati tofauti walizungumzia umuhimu wa spika wa bunge kutokuwa mbunge wa chama chochote cha siasa, ambapo mwenyekiti huyo wa chama alisema kuwa aliwahi kuingia matatani juu ya suala hilo hata kushtakiwa katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki na Madaraka ya Bunge, akipigania uhuru wa cheo cha spika.

Bw. Kabwe alisema kuwa ni wakati mwafaka sasa, Tanzania ikaiga mfumo wa Kenya, ambako spika hapaswi kuwa mbunge na iwapo mmoja wa wabunge akifanikiwa kushinda nafasi hiyo basi hutakiwa kujiuzulu ubunge, ili awapatie wananchi wake haki ya kupata mwakilishi mwingine wa kuzungumzia kero zao na yeye abaki huru kuendesha bunge kwa misingi ya haki bila upendeleo.

Kuhusu amani ya nchi, Bw. Mbowe alisema kuwa chama hicho kinathamini na kiko tayari kuilinda amani ya nchi kwa nguvu zote, ilimradi serikali iliyoko madarakani iendelee kutumia amani na utulivu uliopo, kutengeneza fursa kwa ajili ya ustawi wa wananchi maskini nchini.

Bw. Mbowe alisema "tunaipenda sana amani ya nchi, tunawaenda Watanzania wote na ndiyo maana tunawashirikisha katika elimu ya namna nchi yao inavyopaswa kuendeshwa...lakini kitu ambacho hatukubali ni maneno hayo ya amani na utulivu kutumika kuwatia hofu Watanzania huku watu wachache wakiendelea kunufaika na utajiri wa nchi huku wananchi wao wakizidi kudidimia.

"Tunataka amani na utulivu wa dhati unaotokana na kila mtu kupata haki ya fursa ya kujiendeleza, kupata elimu bora, afya bora na kipato, tunahitaji kuona ustawi na maendeleo ya wananchi na nchi yetu si watu wachache kunufaika...amani na utulivu utumike kupunguza umaskini na ukali wa maisha ya Mtanzania sio kumtisha na kumtia hofu," alisema Bw. Mbowe.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa alizidi kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwajibika kwa wananchi kwa kuhakikisha wanapata maisha bora, akidai kuwa kiongozi huyo ni dhaifu katika uongozi, hivyo asitake kuhamishia udhaifu wa uongozi wake kwa mawaziri kuwa ndiyo wenye matatizo.

"Anataka kujiweka mbali na matatizo ya wananchi wake, sisi tunasema Kikwete huu ni mzigo wako, wananchi wakikosa elimu bora si kosa la waziri, wakikosa afya bora si tatizo la waziri...wewe ni rais mtendaji chukua hatua na maamuzi.

"Rais Kikwete aache usanii, nimemwangalia kwenye tv wakati akifunga semina elekezi anazidi kuwalalamikia mawaziri wake...Kikwete tumeshamtajia ufisadi wote, tunatakaa achukue hatua kuanzia kwenye Tangold, Kagoda ambayo inazidi kumpatia kigugumizi, Meremeta na ufisadi mwingine ambayo tulishamtajia na majina ya wahusika kila kitu wafikishwe mahakamani, serikali lazima iwatumikie wananchi wake, aache usanii," alisema Dkt. Slaa.

Akihutubia mkutano wa Mbinga Mjini juzi katika mkutano wa hadhara katika mfulululizo wa mikutano ya Operesheni Sangara ya CHADEMA katika Nyanda za Juu Kusini, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Kabwe Zitto alisema "kuiondoa CCM madarakani si dhambi wala si uhaini, lazima tukiondoe kwa kura mwaka 2015 na CHADEMA iko tayari na imeiva kuchukua dola kuongoza nchi hii huo ndiyo wajibu wetu kama chama cha siasa.

"Mmesikia leo hata katika vyombo vya habari wameanza propaganda eti tunataka kupindua nchi, CHADEMA haina nia hiyo, wanataka kutafuta sababu ya kuzuia harakati na mchakato huu wa kuwakomboa Watanzania kwa kuwapatia elimu...tutaiondoa CCM kwa kura mwaka 2015...kama CCM wataondoka kabla ya hapo watakuwa wamejitakia wao wenyewe kuondolewa na Watanzania kwa sababu wameshindwa kushughulikia umaskini na ukali wa maisha unaowamaliza sasa Watanzania...wameshindwa kushughulikia elimu, afya na kuweka mazingira ya kila mwananchi kunufaika na utajiri wa nchi hii," alisema Bw. Kabwe.

Kwa upande wake Kada wa CHADEMA, Bw. Fred Mpendazoe amezidi kuwaandamana 'wenzake' aliokuwa nao CCM, akisema kuwa serikali ya chama hicho iliyoko madarakani kwa sasa, haiwezi kusimama pamoja kwani baadhi ya viongozi wake walishafikia hatua ya kukiasi chama hicho kwa sababu ya kutofautiana itikadi na misimamo, katika kuongoza nchi kuwatumikia wananchi.

Bw. Mpendazoe ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa CCM Jimbo la Kishapu, mkoani Shinyanga, alisema kuwa baadhi ya viongozi walioko serikalini waliwahi kukiasi chama kinachoongoza serikali sasa na wakaamua kuunda chama kingine kiitwacho Chama Cha Jamii (CCJ) kwa ajili ya kupinga chama chao.

19 comments:

  1. Ama kuishiwa na sera ni uvuvuzela haswa!! Viongozi wanajuwa kabisa sasa ni wakati wa mchakato wa katiba sasa hivyo vifungu si wavipendekeze wakati ukifika?hawana ya kusema nyumbani kwa mama makinda zaidi ya kuweweseka,nyimbo kuhusu kagoda,tangold na meremeta,namuuliza mchungaji silaha muda laiokaa bungeni kashindwa kupata jibu leo analiuliza barabarani?N akama kashindwa mawakili anao mahakama zipo si ayapeleke wamsaidie ni kiongozi dhaifu hana alijuwalo zaidi ya kubwabwaja na kukashifu huyo mpendazoo ni muhuni yeye alishajijuwa anapigwa chini na ccm, akaijifanya anahama kwenda ccj leo anajifanya alikuwa na wenzake hivi kwa nini asiwataje wakati walipotoswa kusajiliwa? Awataje leo ni kufilisika kisiasa na ni muongo. watu ni werevu wanajuwa walitendalo na wanajuwa nani mkweli na nani mpayukaji.naamini kweli ccm ni chama kubwa sera za cdm haziwezi kusikilizwa kama hawajakitaja au kukikashifu enezeni sera zenu mtakufa na kijiba cha roho

    ReplyDelete
  2. Lo! kama weye ni wa ccm basi ndo mana nchi inakwenda mrama, mbona huoneshi kama una uelewa na hoja za msingi.
    Inamaana ufisadi uliofanywa kagoda,meremeta na nk huoni ndugu, kwani weye macho yako watazamia wapi? na akili yako ipo sehemu gani ya mwili?au weye mmoja wao?? huenda!!
    Twaweza tusiichukie ccm ila waliofanya ufisadi tukawachukia.

    katiba mpya lazima, kwa sababu hiyo iliyopo sio ya ccm, sasa mbona weye waongea kama katiba iliyopo ni ya CCM, au kuna jambo lakukera likibadilishwa baba ako atakosa ulaji au usikute weye mwenyewe utakosa ulaji.Kama nawe ni wa CCM itabidi nujivue gamba kwani kwa akili hiyo ulonayo waidhalilisha CCM.

    Kifupi acaha kujipendekeza na ushabiki usio na kichwa wala miguu!

    ReplyDelete
  3. muongo wewe unashiba vya ikulu ndiyo maana unaropoka hayo. tatizo la watoto waliolelewa na kina mama wa nje ndiyo, kutojua nchi inakokwenda, wewe huna habari kwamba ccj iliibuka? sasa ni wakati wa kujua nani kenge na nani mamba. acha ujinga wako, nani huwa anakula ugali ukiwa unagali uji wa kukorogwa? tunalazimika kuyasikia haya kwa kuwa tayari yameiva. huna sera mbumbu wewe. tea yawezekana kisomo chako ni cha kuunganisha ndiyo maana hujui ukweli, mnapata zero sekondari halafu mnatumia majina ya waliokufa ili mfufuke. hayawani!!

    ReplyDelete
  4. Inawezekana sana kwamba Rais wa Nchi hii ikawa msanii NDIYO, hebu angalia, yeye kila siku anapanda pipa kwenda nje ya nchi, lakini anawaambiwa mawaziri, naibu na makatibu waende vijijini waliko wananchi kwani yeye hajatoka kwa wanacnhi? Chama kimekosa mwelekeo, angali Nape anabwabaja maneno kila kukicha hajiulizi kwa nini CCM ilikosa kura za vijana wengi uchaguzi uliopita. Angalia mtoto wa Rais wetu badala ya yeye kufanya mikakati ya jinsi ya kukikomboa chama na kuongeza vijana ili tupate nguvu ya kushinda uchaguzi mwaka 2015, anaanza kubwabaja maneno ooh wapinzani waende mahakamani wakathibishe kama yeye ni Bilionea. Hivi nani hakujui kwamba unamiliki VX jeusi umepaki pale maskani kwako?? Huo muda wa kusema unatembele CAMRI unautoa wap?? Acheni ulimbukeni kuwaona watu hawajui wafanyalo.

    ReplyDelete
  5. tuhuma,ushahidi,mawakili waliobobea mpaka kupewa zawadi marekani mnao chadema,je tatizo nini hamfungui kesi mahakamani ili muoneshe mfano kuwa mpo makini na kupambana na ufisadi hata mwaka 2015 tuwachague.mmeshalalamika sana kuwa rais kikwete ni dhaifu na tumewasikia na kuwaelewa.je wewe DR slaa ambaye siyo dhaifu na unahushahidi wa kutosha mbona haufungui kesi mahakamani ili kutusaidia wananchi tunaodhurumiwa kwa ufisadi wa kagoda.tangold na wengine,au baba nawe pia dhaifu kazi ni kulalamika tuu matendo hakuna.chama chako kina watu waliobobea katika sheria akina Mabere,Lisu je mnashindwa nini kutusaidia sisi watanzania maskini unaotupigania kwa kufungua kesi mahakamni ili hao wanaotuhumiwa sheria ichukue mkondo wake, au mpaka muingie ikulu ndiyo mtakuwa na ushupavu na nguvu ya kuwashitaki? je mnataka nasi tukiibiwa mali zetu mtaani tujitahidi mpaka tuingie ikulu ndiyo tuwachukulie hatua za kisheria wezi wetu hata kama ushahidi tunao kama mlivyokuwa nao nyie huo wa kagoda,tangold n.k?

    ReplyDelete
  6. watu wengine akili zao ziko nyayoni na macho yao yako mgongoni, tusiwalaumu. Wananchi wengi hawaijui katiba sisiemu hawataki kuwafundisha wanahisi kuwa wakiijua tu watatoa mapendekezo yatakoyowagharimu, huu ndio wakati wa kuanza kuandaa we chelewa tu , ukiona moshi unafuka ujue moto karibu utawaka. Pia kila kitu kina mwisho alivuma Iddi Amin yuko wapi, hata sisiemu wakati wao wa kuvuma uko ukingoni.Hii katiba mpya ndio itakayoondoa kinga ya ma-Rais kutoshitakiwa, ikiondolewa kinga utaona kama watoto wa marais ( wote wajao ) watatanua wanavyotaka, leo anamaliza shule kesho ana majumba hadi mikoani, inakaa akilini kweli? serikali ingekuwa makini takukuru wangafanya kazi yao , kisha ndio hatua ya kwenda mahakamni hivyo vyote serikali ina mkono wake hapo nani athubutu, tena ujue Rais hashtakiwi, upo hapo?

    ReplyDelete
  7. NI KWELI HAPA KUNA SIASA ZA CHUKI BINAFSI NA WATU WANAJIFANYA HAMNAZO KUMBE WANAZO, HIVI VX NI ISSUE?HATA UKIWA MVUVI UNAWEZA KUIPATA HIVI UNAJUWA KUNA KITU KINAITWA AMBARI INAPATIKANA KANDOKANDO YA BAHARI BEI YAKE KILO NI MILLION 5 MPK SITA NA UNAWEZA IPATA VIROBA HATA 5 NA KILA KIROBA NI KILO 100,NJOO TUKUONYESHE IKAZI ZA KUFANYA SIO KULALALMA ETI UNAKULA UGALI IKULU POA WEWE KULA MAKANDE CDM SIO TATIZO MAISHA NI KUPANGA,NYINYI KTK NCHII HII NDIO MMEKUWA WASOMI, WAJUWAJI, WAJANJA, WAHUNI, WALIPUWA MABOMU NK.UNATOWA MIFANO MAITI TOA MIFANO HAI,KUNA MOSHI WA PLASTIC HAUWAKI NI KUFUKA TU,HIZO KUNI MBICHI NI ZA MOSHI TUU HAZINA MOTO

    ReplyDelete
  8. chadema juuuuu, ccm ifeeeee

    ReplyDelete
  9. DUA YA KUKU HAIMPATI MWEWE

    ReplyDelete
  10. Kinachonishangaza mimi kila siku ni watu toka viongozi kujadili habari ya mtu. Huyu an VX huyu ana hiki badala ya kujadili nini tufanye kwa pamoja ili nchi yetu itokane au ijikwamue na hali mbaya ya uchumi, kilichobaki ni Nape, Mpendazoe , Spika Mama Makinda na mpaka JK anapanda pipa kila kukicha, haendi vijijini na mengine mengi. Hivi kweli Watanzania wengi tumekuwa hatuelewi mchakato wa hali halisi ya maisha nchini mwetu na hatuoni matatizo ya nchi nyingine hata zile zilizo na maendeleo makubwa? Jamani tuacheni kujadili mtu tujadili namna ya kujikwamua kutoka hali mbaya, ili kila mtu na hasa yule ajitahidiye kujiinua kimaisha apate nafasi ya kufanya hivyo kwa amani.Ni vigumu sana rais wa nchi yoyote ile kutohudhuria mikutano mbalimbali nje ya nchi yake na JK kama anapanda pipa kwa ajili yakutuwakilisha katika mikutano hiyo sioni sababu ya kumlaumu maana hata Angel wa Ujerumani na Sak wa Ufaransa wanapanada mapipa kuwakilisha nchi zao. Kuna watu nchini mwetu hawajawahi kutoka hata kidogo lakini maisha yao ni mazuri tu kushinda hata wale walioko Marekani wana hata hizo VX!!!!!!!!!Jitihada na maono mbele!

    ReplyDelete
  11. WAKATI ANAWAAMBIA MAWAZIRI WAKE WAENDE VIJIJINI KWA WANANCHI, YEYE ANAKWENDA MAREKANI DO WHAT I SAY AND NOT WHAT I DO.

    ReplyDelete
  12. We jamaaa tunajadili watu kwa sababu ndio chanzo cha umaskini wetu, watu walio waamini wakawachagua, na sasa wanfanya vitu visivyo na ubinadamu, hawajali maisha ya watu.

    ungeona wanawake wanvyoteseka na mimba vijijini.
    ungeona watu wanoshindia mlo mmoja TZ.

    we achaa bwana lazima tuseme. vx, safari za matanuzi nje ya nchi, watoto wa vigogo kutanua .
    HIZO ZOTE NI PESA ZETU SISI WALALA HOI AMBAZO ZIMEKUSANYWA NA SIRIKALI KUPITIA KODI.
    WE ACHA BWANA INAUMA, INAUMA SANA.

    ReplyDelete
  13. SASA WOTE NAONA MNALALAMIKA HOVYO HOVYO TU BILA KUTOA USHAURI NINI KIFANYIKE. DAWA NI KUWAPUMZISHA CCM NA KUWAPA NAFASI CHADEMA. HAPO ADABU ITARUDI NA MAGAMBA YATAVULIWA KIUKWELIUKWELI.

    ReplyDelete
  14. MTU YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU HAWEZI KUMBEZA DR SLAA.NI YEYE ALIYETUSAIDIA WATANZANIA WENGI KUJUA KAMA KUNA UFISADI..CCM ILIKUWA INAPINGA KWA NGUVU NA KUTUMIA MUDA MWINGI KUWAAMBIA WATU DR SLAA NI MWONGO NA MZUSHI,LEO HII WAMEKUBALI KWAMBA CCM INA MAFISADI.SASA NATAKA NIWAAMBIE SIRI MTOTO WA KIKWETE ANAJENGA HOTELI KUBWA DOHA...WATANZANIA WANAO MTETEA HAWAJUI TU..SITAKI NIONGEE ZAIDI.KUDAI KWAMBA DR SLAA AENDE MAHAKAMANI NI KUSHINDWA KUELEWA KWAMBA MAHAKAMA ZOTE ZIKO CHINI YA UTAWALA WA KIKWETE HATA KAMA UNA USHAHIDI HUWEZI KUMTIA FISADI YEYOTE WA CCM HATIHANI.MBONA MAFISADI WAPO CCM HATA CCM INAWAJUA LAKINI HAIWEZI KUWACHUKULIA HATUA MAANA NDIO UTAKUWA MWISHO WA CCM KAMA WATATHUBUTU KUFANYA HIVYO.CCM WANAFIKI WAKUTUPWA

    ReplyDelete
  15. KUWAPELEKA MAFISADI MAHAKAMANI NI KUPOTEZA MUDA KWANI HAO JAMAA WATASHINDA TU. KWANI MMESAHAHU KESI YA CHENGE ILIVYOKUA. DAWA NI KUWATOA CHAMA CHA MATAPELI MADARAKANI 2015 HAPO NDIPO WATANZANIA TUTAPATA MAENDELEO.

    ReplyDelete
  16. BABA LIZ NA UFISADI NI DAM DAM. KWAHIYO KUWAPELEKA MAFISADI MAHAKAMANI NI KUPOTEZA MUDA HIVI MMESAHAHU KUWA MAHAKIMU WOTE NI WATEULE WA BABA LIZ NA MAFISADI WOOTE NI RAFIKI ZAKE? HAPENDI KUONA RAFIKI ZAKE KAMA RA,AC NA EL WANAKWENDA SEGEREA KULA UGALI NA MAHARAGE. HIVYO ATAJITAHIDI AHAKIKISHE WANAKUA SALAMA!!!

    ReplyDelete
  17. HUO NI UJINGA WENU, LAZIMA TUWADANAGANYE SANA , NA HAKUNA WA KUTUFANYA LOLOTE HATA UCHAGUZI WA 2015 TUNAPETA KWA KISHINDO.
    MNABWABWAJA KUWA SIE MAFISADI, UCHAGUZI UKIFIKA MNAZIKIMBILIA PESA ZETU, NJAA INAWASUMBUA NYINYI.

    ACHENI TUWAKUSANYIE PESA ZA KUWALISHA WAKATI WA UCHAGUZI.

    ReplyDelete
  18. KUNA JAMAA HAPO MWANZO LINACHANGIA ETI KUNA AMBARI BEI YAKE NI KUBWA NA INAPATIKANA BAHARINI,USITUONE WAJINGA WEWE ENDELEA NA DEVIL POWER ZAKO ,ETI AMBARI LABDA AMBARI NI EPA NA WIZI WAFEZA ZA WANANCHI ,IPO SKU UNADHANI MISRI ,TUNISIA SASA LIBYA WALITEGEMEA HAYO? KUNA KITU WANASEMA TIME WILL TELL,HAKI YA MUNGU IPO SIKU VP KUHUSU BAGBO ALIKAMATWA KAMA FALA BAADA YA UDANGANYIFU WA UCHAGUZI ,NA WANANCHI WALIKUA HAWAMTAKI,HAPO WALISUBIRI UCHAGUZI UJAO? NAKWAMBIA WE NGOJA HAIWEZEKANI NCHI IKUMBWE NA MAMBO MENGI HIVO KWA WAKATI MMOJA,MARA UMEME HAKUNA,UFISADI,USANII USANII LIA MAHALI KAMA POLISI RUSHWA MAHAKAMA HOOSPITAL,NK HUDUMA DUNI ,ELIMU DUNI MAISHA YANAPANDA KILA KUKUCHA NINI MAANA AKE HUKU KAULI MBI YA MAISHA BORA KWA KILA MTZ ? MAMA YANGU HAKUNA HIYO WACHA IWE MBAYA PENGNE WATOO WETU WAKUJA KULA GUDTYM.

    ReplyDelete
  19. KUNA UMUHIMU WA SPIKA KUTOKUWA MBUNGE. MANA JIMBO LAKE LINALALA BILA MAENDELEO MANA HANA HATA MAHALI PA KUSEMEA NA KUTETEA MAENDELEO YA JIMBO LAKE.

    ReplyDelete