LONDON, England
KOCHA Msaidizi wa Manchester City, David Platt amesema amefurahi msimu huu kufanya kazi na mchezaji mtukutu Muitaliano, Mario Balotelli.Ukiwa ni msimu wake wa
kwanza kuchezea klabu hiyo katika ligi ya England, mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya Inter Milan amekuwa kivutio kwa kuambulia kadi za njano na nyekundu huku akipachika mabao.
Kutokana na hali hiyo, Platt alisema jana kuwa ni presha tupu kufanya kazi na Muitaliano huyo.
"Unapaswa kumpa sifa Robbie (Mancini), nadhani Robbie ana imani naye," alisema Platt.
"Kila mmoja anapoondoka nchini mwake na kwenda kucheza katika mfumo mwingine wa uchezaji inakuwa ni vigumu unapokuwa uwanjani hususani katika umri wa miaka 20," aliongeza kocha huyo.
Alisema vilevile mchezaji huyo alikuwa majeruhi mwanzoni mwa msimu na akasema hakuna wasiwasi kuhusu hilo kwani amekuwa akifanya vitu ambavyo mara nyingine vimekuwa vikipamba mbele ya kurasa za vyombo vya habari huku vikimkosoa mno.
"Lakini nadhani kwa yeye kama binadamu imekuwa rahisi kwake kuvikabili ni kijana mzuri," alisema.
No comments:
Post a Comment