17 May 2011

Polisi waua watano Nyamongo

Na Timothy Itembe, Tarime

WATU watano wameuawa na polisi na wengine, baada ya kuingia kwa nguvu katika Mgodi wa Nyamongo kwa nia ya kuiba mawe ya dhahabu.Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya, Bw. Costantine Massawe aliwambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea lilidumu kwa saa tatu baada ya polisi kupambana na watu wanaodaiwa kuvamia mgodi kwa lengo la kuiba mawe hayo.

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema watu waliokufa katika tukio hilo ni watatu, Chacha Ngoko (19) mkazi Wakerende; Emmanuel Magige (27) wa Nyakunguru na Chacha Mwasi (25) Mkazi wa Bisalwi Kata ya Manga.

Mmoja ya watu walishuhudia tukio hilo aliwataja watu wengfine wawili, waliouawa katika serengeti lakini hakukuwa na mamlaka iliyothibitisha vifo vyao.

Kamanda Massawe aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni OCSID wa Kituo cha Tarime Hasani Mayaa aliyepigwa jiwe kichwani mwingine ni ASSP Simoni Mrashani aliyejeruhiwa kiunoni baada ya kupigwa na jiwe.

Alisema watu hao wanakadiliwa kuwa 800 hadi 1,000 walivamia mgodi kwa lengo la kuiba mawe ya dhahabu huku wakiwa na silaha za jadi pamoja na marungu mawe na kombeo.

Alisema kuwa katika tukio hilo polisi walilazimika kuwazuia kwa kuwafyatulia risasi za hewani na mabomu ya machozi lakini
wavamizi hao waliwarushia mawe kwa kutumia kwa kombeo.

Katika harakati hizo polisi walitumia risasi za moto ili kujihami ambapo watu watatu walikufa na wengine watano kujeruhiwa.

Bw. Massawe aliwataka wazee wa mila kuingilia kati jambo hilo kwa
kuwakanya vijana wao kuvamia mgodi.

Taarifa kutoka hospitali zinasema kuwa majeruhi waliaolazwa katika hospitali hiyo hali zao si nzuri kutokana na majeraha waliyopa.

Wananchi walioshuhudia mkasa huo walisema kuwa tukio hilo litokea jana saa 11.00 alfajiri katika eneo la Rampard karibu na kinu cha kusagia dhahabu.

Wawili wauawa Pwani

Na Mwandishi Wetu John Gagarini, anaripoti kutoka Kibaha, Pwani kuwa watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni wezi wa wamekufa kwa kupigwa na watu wenye hasira baada ya kujificha nyumbani kwa mtu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana mjini Kibaha Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Bw. Gregory Mushi alisema watu hao walipigwa na vitu mbalimbali na kusababisha vifo vyao.

Kamanda Mushi alisema tukio hilo lilitokea Mei 15 mwaka huu majira ya saa 11:30 jioni Kijiji cha Lugoba wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Akielezea zaidi juu ya tukio hilo alisema kuwa polisi walipewa taarifa kuwa watu hao walivamiwa na wananchi lakini walikimbia na kwenda kujificha kwa Bw. Juma Miraji mkazi wa Kijiji cha Friends Corner.

“Baadhi ya askari walikwenda kwenye nyumba hiyo wakiongozwa Koplo Rose ambapo walimkuta mtuhumiwa Bw. Zakaria Ngosha (40) makazi mkazi wa Makombe-Lugoba, lakini polisi walishindwa kumtoa kutokana na kuzidiwa nguvu na wananchi waliogoma asitoke,” alisema Bw Mushi.

Alisema ilibidi mkuu wa Kituo cha Chalinze, Bw. Mapalala kwenda kwenye uongozi wa Serikali ya Kijiji Lugoba na kuongozana naye kuwasihi wananchi hao kupunguza jazba ili mtuhumiwa achukuliwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Baada ya muda waliruhusu mtuhumiwa huyo atolewe lakini ghafla wakati mtuhumiwa anapelekwa kwenye gari la polisi kuelekea kituoni waligeuka na kuanza kurusha mawe na matofali na kumjeruhi mtuhumiwa,” alisema Bw Mushi.

Kaimu kamanda huyo alisema mtuhumiwa huyo alizidiwa na kupoteza maisha kutokana na kipigo hicho kikali na alifia njiani kupelekwa Hospitali ya Tumbi kwa matibabu.

Katika tukio hilo pia walimjeruhi kifuani Koplo Jumanne na mwenyekiti wa Kijiji cha Lugoba Bw. Shaban Onera alijeruhiwa kichwani pia waliharibu kioo cha gari la polisi Namba STJ 9719 aina ya ya Land Cruiser.

No comments:

Post a Comment