Na Elizabeth Mayemba
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeipa unafuu, Simba katika mechi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Wyadad de Casablanca Morocco kwa kuipeleka
mbele kwa siku kumi kuanzia jana.
Mechi hiyo ambayo Simba, inacheza na Wyadad, baada ya Mabingwa wa Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kuenguliwa na CAF kwa kumchzesha Janvier Besala Bokungu aliyekuwa na mkataba na timu ya Esperance ya Tunisia, itachezwa kati ya Mei 27, 28 na 29 mwaka huu katika uwanja huru.
Taarifa hiyo ya CAF iliyotumwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuchezwa tarehe hizo inaonekana kuwa ahueni kwa Simba kwani kwa sasa itakuwa na muda wa kujiandaa vyema, tofauti na taarifa za awali ambazo zilidai mechi hiyo ingechezwa wiki hii wakati wawakilishi hao wa Tanzania wakiwa hawajakaa sawa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alieleza kuwa Simba na Wydad de Casablanca ya Morocco ndizo zitakazopambana katika mechi hiyo ya mkondo mmoja.
Alisema Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), linatarajia kutaja katika muda mfupi ujao nchi ambayo mechi hiyo itachezwa.
Wambura alisema timu itakayoshinda mechi hiyo itaingia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, ikiwa kundi B pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, Esperence ya Tunisia na Moloudia Club d’Algerya Algeria.
Aliongeza kwamba pia timu itakayoshindwa katika mechi hiyo, itaingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi ya kwanza nyumbani na Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na 12 mwaka huu.
mbona kwenye ratiba ya Caf inanonyesha timu itakayoshindwa mechi hiyo itacheza na DC mapembe 27, 28, 29 May 2011 na kurudiana june 10,11 na 12?TFF fuatilieni hili muwe na uhakika wa ratiba
ReplyDeleteCONFEDERATION AFRICAINE DE FOOTBALL
8th Edition of the Orange Confederation Cup CC 2011 / 8ème Edition de l’Orange Coupe de la Confédération CC 2011
Draw of the 2nd 1/8th final / Tirage du 2ème 1/8ème de finale
Teams disqualified from 1/8th final, CL
Equipes disqualifiées du 1/8ème de la final, CL
Teams qualified from 1/8th final, CC
Equipes qualifiées du 1/8ème de la final, CC
E.S.Sétif (Algeria) JSK (Algeria)
Interclube (Angola) 1o Agosto (Angola)
Asec Mimosas (Côte d’Ivoire) Sofapaka (Kenya)
Ittihad (Libya) MAS (Morocco)
WAC (Morocco) / Simba (Tanzania) DHJ (Morocco)
ASC Jaraaf (Senegal) Kaduna Utd (Nigeria)
Club Africain (Tunisia) Sunshine Stars (Nigeria)
Zesco Utd (Zambia) DCMP (RD Congo)
No Match
89 E.S.Sétif (Algeria) v Kaduna Utd (Nigeria)
90 Kaduna Utd (Nigeria) v E.S.Sétif (Algeria)
91 ASC Jaraaf (Senegal) v JSK (Algeria)
92 JSK (Algeria) v ASC Jaraaf (Senegal)
93 Club Africain (Tunisia) v Sofapaka (Kenya)
94 Sofapaka (Kenya) v Club Africain (Tunisia)
95 Ittihad (Libya) v Sunshine Stars (Nigeria)
96 Sunshine Stars (Nigeria) v Ittihad (Libya)
97 Zesco Utd (Zambia) v MAS (Morocco)
98 MAS (Morocco) v Zesco Utd (Zambia)
99 WAC (Morocco) / Simba (Tanzania) v DCMP (RD Congo)
100 DCMP (RD Congo) v WAC (Morocco) / Simba (Tanzania)
101 Asec Mimosas (Côte d’Ivoire) v 1o Agosto (Angola)
102 1o Agosto (Angola) v Asec Mimosas (Côte d’Ivoire)
103 Interclube (Angola) v DHJ (Morocco)
104 DHJ (Morocco) v Interclube (Angola)
N.B.: The 8 winners of the Confederation cup, plays the 2nd leg at home
Dates : Match aller / 1st leg 27, 28, 29 Mai 2011
Match retour / 2nd leg 10, 11, 12 Juin 2011