Na Agnes Mwaijega
MKAZI wa Ubungo Maziwa Bw. Feto Philemon amekutwa akiwa amekufa chooni, nyumbani kwake.Tukio hilo lilitokea Dar es Salaam jana majira ya saa 7 mchana.Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Bw. Charles Kenyela alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mke wa marehemu, Bi. Jesca Andrew (33), inawezekana marehemu alikunya sumu au vidonge kutokana na ugomvi uliyokuwepo kati yao.
Alisema ugomvi huo ulitokea baada ya marehemu kukopa shilingi laki nne na kizutumia katika starehe zake.
Mwili wa mrehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala na upelelezi kuhusu tukio hilo unaendelea.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi linawashikiria watu sita kwa tuhuma za kukutwa na lita 20 za gongo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala alisema watu hao walikamatwa Dar es Salaam juzi katika maeneo ya Karakata Bondeni.
Aliwataja watu hao kuwa ni Ester Victor (43), Bakari Juma (25), Tony Yakobo (32), James Kirabi (28), Dongwe Zanta (25) na Ally Said (24)
No comments:
Post a Comment