LONDON,England
KOCHA wa timu ya Arsenal,Arsene Wenger amesema kuwa anahitaji kukifanyia marekebisho kikosi chake ikiwa ni wa mara ya kwanza kwa kocha huyo kukiri udhaifu
wa timu yake.
Wenger aliyasema hayo juzi baada ya kocha Sir Alex Ferguson kusema kuwa klabu yake ya Manchester united ina hofu na Chelsea iliyopiga hatua kuliko Arsenal.
Wenger alisema kuwa klabu ya Arsenal ina msimamo mzuri kifedha na ikibidi wanaweza kufanya mabadiliko makubwa.
Aliongezea kuwa, katika ulimwengu huu kila mmoja analia hana fedha, lakini mtu asiyetumia pesa atakuwa ni mjinga.
Wenger alisema kuwa nia yao ilikuwa kujenga uwanja mpya bila kupoteza nafasi kileleni mwa Ligi kuu ingawaje walifahamu kuwa watakuwa na kipindi kigumu cha muda wa miaka minne hadi mitano.
"Tulichukua uamuzi wa jinsi ya kusalia miongoni mwa timu bora tukitegemea mapato duni yaliyopo.Tumejitahidi, lakini sasa hivi, bila shaka watu wamechoka. Ninaelewa vyema kwa sababu hata mimi nimechoshwa pia," alisema Wenger.
"Ukitizama msimu wetu utaona kuwa hatuhitaji mabadiliko makubwa. Hapo tutakosea tukifanya hivyo.Ukiwa na biashara ya gazeti lililo katika nafasi ya pili bora kwa mauzo, hufungi biashara yako,"aliongeza.
Alisema kuwa lazima wazingatie dunia ya sasa ambapo ukimaliza wa pili kwa tofauti ndogo, kila mmoja atakuona kama taka.
Akizungumza na wandishi wa habari baada ya mechi ya Manchester United dhidi ya Everton, Wenger aliuliza kama hisia zake zinanisukuma katika soko huku akisema kuwa anahisi daima kuna haja ya kuimarisha kikosi.
Shinikizo la kushindwa kupata ufanisi kwa msimu wa sita mfululizo lilionekana kumdhuru Arsene Wenger siku ya jumatano aliposhuhudia vijana wake wakishindwa kuzuia kuporomoka kwa uongozi wa mabao matatu kwa moja.
Tumekuchoka wenger ondoka zako nenda zako ukapumzike,sisi si washindani ikiwa wewe utaendelea kuwapo hapo, bora ondoka aje mwingine alete ushindani.kila mwaka cc ni wasindikizaji tu,chenga twawala kufungwa twafungwa nini maana yake,tumechoka ondoka hatukutaki nenda kwenu paris ukapumzike,tena tunakuambia kwa roho safi ondoka,asernal sio mali yako achia ngazi wapishe na wengine waje hapo,kila siku cc tumekuwa jamvi la wageni,tukifunga hatuwezi zuia goal,tumechoka nw, please take u a time mr wenger.tumekosa FA CUP tumekosa UEFA CUP na sasa tunakosa PREMIER CUP nenda zako mr wenger.
ReplyDelete