Na John Gagarini, Kibaha
WATU wanne wamekufa na wengi 30 kujeruhiwa baada ya mabasi mawili waliyokuwa wakisafiria kugongana eneo la Kisemvule wilayani Mkuranga mkoani
Pwani.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Bw. Absalom Mwakyoma alisema ajali hiyo ilitokea Aprili 11 majira ya saa 12:30 jioni barabara ya Kilwa na kulihusisha basi la kampuni ya Sumry lenye namba za usajili T 686 ARZ aina ya Nissan Diesel lililokuwa likitokea Mtwara kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Bw. Patrick
Leonard (35) mkazi wa Tabata.
“Basi la Sumry liligongana na basi dogo aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 256 AVH mali ya kampuni ya Asifu likitoka Dar es Salaam kwenda Ikwiriri wilayani Rufiji likiendeshwa na Bw. Omary Mohamed (50) mkazi wa Mbagala,” alisema Bw Mwakyoma.
Chanzo cha ajili hiyo ni ni gari lenye namb za usajili T 374 BJE aina ya Toyota Land Cruiser iliyokuwa ikiendeshwa na Bw. Deogratius Bundala (42) mkazi wa Mtwara kuegesha vibaya gari lake pembeni mwa barabara na mwendo wa kasi wa basi la Sumry na Coaster.
Kamanda huyo alisema madereva wa magari ya Land Cruiser na Sumry wamekamatwa na dereva wa Coaster amevunjika miguu yote, ambapo majeruhi sita wamelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wanne katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga huku 19 wakiwa wamelazwa Hospitali ya Manispaa ya Temeke. Majina ya marehemu bado hayajafahamika.
No comments:
Post a Comment