11 April 2011

Udini wapenyezwa madai ya katiba

Na Heckton Chuwa, Moshi

SIKU chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) kutangaza maandamano ya nchi nzima kupinga mchakato unaoendelea wa muswada wa
katiba nchini, kundi moja la wasilamu limeonya uamuzi huo usifanyike Dar es Salaam kwa madai ya kwamba una agenda ya kumng’oa Rais Jakaya Kikwete ikulu.

Onyo hilo limetolewa na Amir wa Vijana wa Kiislamu, Shekhe Shaban Mapeyo, wakati akihutubia kongamano la waislamu lililofanyika mjini Moshi, mkoani
Kilimanjaro, jana.

“CHADEMA wamekuja na agenda mbalimbali wakidai ni za kisiasa na wengi tumeamini hivyo, ukweli ni kwamba wana agenda ya siri wao na maajenti wao tangu mwanzo kwa
njia mbaalimbali kama vile Dowans na sasa wameikomalia hii ya katiba mpya, hili waislamu tusilikubali wakija huko mikoani wakataeni.

"Sisi Dar es Salaam tunawasubiri watakutana na nguvu za wenye historia ya Tanzania,” alisema Shekhe Mapeyo huku akishangiliwa na umati wa waliohudhuria kongamano hilo.

Alisema agenda ya katiba inayotumiwa na CHADEMA kwa madai ya kutumia nguvu za umma ni danganya toto, lengo halisi ni kumng’o Rais Kikwete ikulu na kwamba waislamu watapambana kwa hali na mali kuzuia uovu huo kwa niaba ya Watanzania wote.

Shekhe Mapeyo alisema kuwa waislamu wamekuwa wakinyamaza kwa kila jambo wakati ajenda zikiibuliwa na vyama mbalimbali vya siasa lakini kwa sasa wameamua kusimama
kidete baada ya kuona CHADEMA wamekuja na ajenda ya kutaka 'kuhatarisha amani ya nchi'.

Sheikh Mapeyo alisema, “Meseji zimesambazwa zinazohamasisha watu wajiandae kumng’oa Mujahidina Ikulu na sisi tunajiuliza Rais Kikwete ni Mujahidina tangu lini? Maana sisi tunachojua ni kiongozi wa wananchi wa Tanzania anayefanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa,” alisema Sheikh Mapeyo.

Kuhusu madai ya CHADEMA kuwa wanahangaikia katiba mpya kwa niaba ya Watanzania wote, Sheikh Mapeyo alisema kuwa huo ni uzushi kutokana na jinsi viongozi wa chama hicho
wanavyotaka katiba hiyo ipatikane kwa haraka tena ndani ya miezi sita tu.

“Jamani mchakato wa kutafuta katiba mpya si mwepesi na wa haraka tena kwa miezi sita tu kama wanavyotaka wenzetu hawa, nia yao hii ni hatari kutokana na umuhimu wa katiba ya nchi; katiba inayopatikana kwa muda wa miezi sita ni ya nchi ya watu waliochanganyikiwa, kunahitajika umakini wa hali ya juu kwenye swala kama hili,” alisema.

Kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi ya CHADEMA iliyonadiwa na mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa mwaka jana, chama hicho kilipanga kuanzisha mchakato wa kuandaa katiba mpya ndani ya siku 100 (siku 100).

29 comments:

  1. UZUSHI WA MWANDISHI. JE HUJAMUONA IMAMU WA ZANZIBAR AKIICHANA RASIMU YA KATIBA? WAISLAMU TUNATAKA KATIBA MPYA NA ITAYOANDIKWA NA WANANCHI NA SI WANASIASA. CCM NA CHADEMA HAWANA TOFAUTI WANAGOMBEA UONGOZI KUWEZA KUNUFAISHA BIASHARA ZAO IKULU. WAANDISHI KAMA NYIE MLIOEGEMEA UPANDE MMOJA NDIO HATARI KWA NCHI NA SIO WAISLAMU. MTAYARISHAJI WA RASIMU YA KATIBA NI MWANASHERIA MKUU AMBAYE NI WEREMA AKISHIRIKIANA NA WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA KOMBANI WOTE HAWA NI WAKIRISTO. WEWE MUANDISHI USILETE MAMBO YA KIJINGA HAPA,WAACHENI MASHEIKH,MAPADRI,MAASKOFU NA MADHEHEBU MENGINE WASEME,HICHI NDICHO TUNACHOKATAA KWENYE RASIMU YA KATIBA KUPANGIWA YA KUSEMA.HIYO KATIBA NDANI YA SIKU MIA NI YA WANANCHI AU YA MBOWE,SLAA,NDESA NA MTEI? HATUTAKI WANASIASA WATUTUNGIE KATIBA. TAYARI NYUSO ZAO ZIMEISHAONDOKANA NA UBINAADAMU KUTOKANA NA TAMAA YA MADARAKA NA UTAJIRI NDANI YA SIASA. TUNAPENDA MTU MUADILIFU,MCHA MUNGU NA ANAYEISHI MAISHA YA KAWAIDA SANA NA FAMILIA YAKE KAMA ILIVYOKUWA ENZI ZA KINA NYERERE. AHSANTE SANA MBATIA NA NCCR MAGEUZI KWA KULITAKA BUNGE LIBADILISHE KIPENGERE CHA KUANDIKWA KATIBA ILI KATIBA ITUNGWE NJE YA CHOMBO HICHO ILI TUWEZE KUWADHIBITI.

    ReplyDelete
  2. Hawa CDM wao wanajifanya kila jambo wanalivalia njuga, na kulifahamu fika na kujifanya wana uchungu sana na nchi hii lakini hizi ni sera maalumu za kuwarubuni watu na ni waongo na wazandiki. Ninakubaliana na maneno ya Ngawaia wkt wa NCCR akiwa na Mrema kuwa hata wao walikutana na huo mtandao wa kufanya vurugu ili wananchi waichukie Serikali iliyo madarakani na wanalipwa hela nyingi sana maana hao ni wenye pesa chafu hazina kazi wao starehe yao ni kuona watu wakipigana wenyewe kwa wenyewe na kukuuana, Sera zao inakuwa maandamano na kupinga hata likiwa jema ndio kazi yao tuwe makini na tuamke hawa ni wanafiki na hawafiki mbali.Angalieni Tunisia,Somalia,Egypy Yemen,Syria na hata huko Libya ni haohao kuuondoa uongozi halali uliopo madarakani,na hapa utaona leo wamedai katiba,inataka kuanza mchakato wanaandamana,ikiteuliwa hiyo kamati pia wataipinga na kuandamana ikija kujadiliwa pia wataandamana na ikicheleweshwa kupitishwa pia wataandamana na mwisho lengo lao litimie TUWE MAKINI NA HAWA WENYE UCHU NA TAMAA YA MBWA MWITU

    ReplyDelete
  3. Kama hali ndiyo hii ya dini kuingia kwenye siasa tanzania tunakwenda wapi? waislam kama huyu sheik wao wametuchosha sana na hawafai katika jamii ya usasa, tunajua kuwa wanatumiwa na CCM ili kumlinda mwislam mwenzao ambaye amedhihirisha wazi kuwa hana uwezo wa kuongoza nchi. Labda hili hawalijui, Hapa hatuna Rais bali tuna Mkaazi wa IKULU TU.

    ReplyDelete
  4. Kwan wanayoyalalamikia chadema uongo?sasa ule muswada gan acha uchanwe..kuhusu kupewa pesa na wamerekan ni bora waongezewe kabisa hata wangepewa na shetan ilimradi wanayoyapigia kelele ni mazur kwa wananch its okey..ccm wasipopelekwa puta wanajisahau sana na kutuona watz wasenge.hata sio ishu ya kikwete hapa ni ccm hao waislam nao siwaamin watakuwa ccm na sio waislam..mana 2po waislam lkn ha2na wawazo hayo..kwanza watanzania ADUI YETU MKUBWA SI DINI FULANI WALA KABILA FULAN BALI ADUI YETU NI UFISADI. Saa ya ukomboz ni sasa 2sikubali kugawanywa.

    ReplyDelete
  5. Mwenye macho haambiwi tazama na ukiwa ndio unaamka basi hujachelewa osha uso wako kuwa tayari kwa chai,hii hali ni mpango maalumu wa kutaka kumng`oa kikwete kwa njia ya maandamano,kinachosubiriwa hapo ni kupitishwa katiba haraka haraka ili aweze kushtakiwa,ikiwa mmeamka basi hongereni la ikiwa bado mpo katika ndoto oh poleni sana.hapo yoyote yule mwenye jina la kiswahili basi ni adui tu ila akikaa mwenye jina la kizungu huyo ni mzuri hata afanye baya kiasi gani!hebu tazameni mfano hai kwa rais mstaafu wa awamu ya pili au mmesahau nyie wadanganyika!amkeni sasa sio kulala tu na kulalamika.Mungu tuepushe na vyama vyenye mtazamo wa UDINI kama hivi vya chaga na vingine.

    ReplyDelete
  6. Lakini kwanini hawa jamaa wanakurupuka siku zote? Au hawana vichwa? Mbona inaonesha uwezo wao wa kuchambua mambo ni mdogo? Wao siku zote ni kuchanganya mada tu.Nawashauri wawe wanasoma na vitabu vingine vya kuwasaidia kubrashi bongo zao siyo kun'gan'gana na kile kitabu kimoja tu,hakiwajengi.Hasa wale wanopendelea kutoa mawazo yao hadharani.

    ReplyDelete
  7. oh!!! poleni sana watanzania wenzangu kwani binafsi nimeona bora niseme kwa sababu naona hali si nzuri kwa nini tunapenda kuamini kila kitu bila kukifanyia uchunguzi kama hili suala la UDINI hili suala lilikuja tena kupitia viongozi wetu wa juu serikalini bila uchunguzi wowote kwamba ni kweli au si kweli tumeanza kukurupuka nalo oh dini oh mara kabila tunakwenda wapi bila hata aibu vijana nao wamejikita wakisema kile ambacho mkuu wa nchi alisema jamani vijana hapa tukisema tuende kidini itakuwa hatari maana tukisema upande wa shule kuna shule za wakristo nyingi hata waislamu wanasoma upande wa hosipitali hivyhivyo kwa hiyo hapa vijana wenzangu cha msingi nikuangalia jinsi ya kujitoa ktk huu umaskini ulio ikumba nchi yetu na si malumbano ya UDINI

    ReplyDelete
  8. Kuna watu wanauchafua Uislam. Wanautumia kama Idara ya CCM. Wameangukia kwenye propoganda ya CCM dhidi ya CHADEMA. Wanadanganywa kuwa mtu hawezi kuwa dhaifu ila kwa sababu ya dini yake. Tuseme basi hata Makamba anaandamwa kwa sababu ya Uislamu wake? au Lowasa alijiuzulu kwa ajili ya kuandamwa na waislamu? Tuache kufanywa wajinga, tufikiri kwa vichwa vyetu na tusihusishe dini zetu na propaganda za CCM

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli mwelekeo wa taifa letu juu ya propaganda za udini sio nzuri. Watanzania tumekubali kugawanywa na kuchochewa kuaanza kutazamana kwa misingi ya udini. Hebu fungua na sikiliza link hii hapa chini uone mwenyewe:

    http://www.wavuti.com/4/post/2011/04/muungano-bassaleh.html

    ReplyDelete
  10. Ndugu yangu uliyenitangulia hapo juu acha lugha chafu kuwaita wengine washenzi! Dini gani ile inajiona inafaa machoni pa Mungu? acha hayo, fuata dini yako kama unataka kwenda mbinguni/peponi! Tatizo lako nahisi una shida ya elimu kwani aliyesoma anapinga hoja si kutoa matusi na kuwaita wengine washenzi! Nenda shule kwanza!

    ReplyDelete
  11. Mshenz ww usiyejitambua..umeusoma mswada kwanza nna uhakika ujauelewa sasa watu wakipinga madudu yale mnasema wadin..sa wa2 wasikemee maovu mnaanza ooh mnamsema kikwete kwa sababu ya din yake..viongoz wa din hawajaanza leo kukemea..mshenz ww unaye2mia din kuficha ufisad wenu na walaaniwe wote wanaotumia udin kuficha uovu..mkapa na kikwete walewale,wapinzan wkt wanamshadadia mkapa kikwete c alimtetea eti aachwe.. Sasa ndo ujiulize wale din moja kwanza din zenyewe za wakolon..na mtakoma mwaka huu mafisad ha2danganyik..

    ReplyDelete
  12. nyie wote mnanjaa nendeni mkale kwa mboe na slaa ndio muongee hamna maana hata kidogo hamjui mlifanyalo misioni sababu ya kuzozana hapa simuandamane tu tatizo lipo wapi?ingieni tu mtaani iwe historia kwenu nyie ndio vijana mliosoma na mnauchungu na hiyo nchi wengine hawana wengine hatutaki hata kuongozwa na mtu mtatuweka kundi gani?kama hujasoma unategemea utaletewa chakula mdomoni mwako na kusoma kwenyewe uangalie sio unasoma kozi za midomo kuchonga utamaliza viatu kutafuta kazi mbona wenye fani zenye akili hatuwasikii kukosa kazi?tatizo la vijana wengi mmesoma na kuhudhuria kozi za fani yenu

    ReplyDelete
  13. Ukitukanwa na wewe ukarudishia ma2c inamaanisha yamekuingia hayo ma2c, Mie ni mkristo ila nilifurahi kuona Waiclam wa Zanzibar wamekataa mswada wa katiba mpyaa kwani wao maoni yao wameona umeegemea upande mmoja tu wa Tanganyika na wala si udini kama mnavyotukanana sasa, pia bungeni kuna mbunge leo asubuhi alikua anatoa maoni baadhi ya vipengele viondolewe hasa vya kumuwekea kinga rais asishitakiwe afanyapo makosa, sasa naomba mtambue tatizo ni kikwete anataka kuharakisha hiyo katiba atakayoisimamia hadi ikamilike ila ki2 muhimu kwake aweke vipengele vitakavyomlinda atakapotoka madarakani nyie hamuoni hilo tatizo? kumbukeni ameshirikiana na mafisadi wengi wakiwamo wakristo tena ndio wengi sasa mmepandikizwa chuki mmekubali kununuliwa, Chadema wanaongelea watz na co wakristo je Zitto kaondolewa na wanachama wote ambao ni waiclam ndani ya Chadema ili tuamini ni chama cha Kidini? Think Twice Guy's msikulupuke kuanza kunununiana kisa udini kumbukeni wote ni watanzania.

    ReplyDelete
  14. Inashangaza kuona kiongozi wa dini anatumia nafasi yake ya uongozi kutoa matamshi ya kutishia jamii kua watatumia wafusi wa dhehebu lao kulinda maslahi ya kiongozi wa serikali tuliwahi kusikia eti kiongozi wa serekali atapewa ulinzi wa majini hapa kuna agenda isiojulikana lakini wa Tanzania wanatakiwa kua makini siku zote wajinga hutumiwa wakajikuta wana ua hata ndugu zao kutokana na ujinga wao, Ni nani asie jua kua utawala ni mbovu? Anaepinga ni kwa sababu anafaidika na utawala huo kwa namna fulani na hao ndio tusio wataka hivyo mabadiliko ya kweli ni ya lazma kwani wanao teseka ni wengi.

    ReplyDelete
  15. Eti suala la DOWANS na Katiba ni agenda ya siri ya CHADEMA? Nina mashaka na uelewa wa Waislamu hawa. Katiba imeanza kudaiwa toka enzi za Mwalimu, Suala la Dowans hadi Waziri mkuu kaziuzuru halafu eti ni janja ya kumuondoa JK madarakani? Uislamu sasa kama alivyosema Makamba unakuwa kama chama cha siasa.

    Ebu angalia kila mwaka wanaandamana wakihamasishana Ijumaa siku ya Swala.Eti wanapinga GADAFI kuondolewa madarakani. Mbona hawaandamani kupinga Ufaransa kumsaidia Quatara kumg'oa Laurent GABO? Ujinga huu watauacha lini?

    ReplyDelete
  16. Unajua ni kitu cha kushangaza mtu anaposema eti watz ha2fanyi kaz ndomana ni masikin nasema hapana kaz 2nafanya lkn hatul mafisad wanakula jasho le2..afu naudhika nnapoona eti viongoz wa din wanapotetea viongoz dhaifu eti tu kwa sababu ya din zao utafikir wao sio watz na hawapat shda kama wenzao..narudia tena adui ya mtanzania ni FISADI NA WALA SI DINI NYINGINE WALA KABILA LINGINE. Ful stop

    ReplyDelete
  17. Mapadri na maaskofu hawajawah kuchagua chama iwe ccm,cjui chadema wala cuf. Kawaida yao kukemea maovu likikugusa haya,afu unachekesha umasikn wa nch hii umeletwa na ccm coz ndo waliotutawala kwa miaka 50 sasa hapo wakristu wanaingiaje?au ndo kusema ccm ni chama cha wakristu we kwel mavi,eti chadema cha wakristo haya cha waislam kip?cuf au?acha kukuwadia mafisad ulipo hapo unadhik hadi matakon afu unawashadadia mafisad..unalo hlo kizaz kpya hik hatudanganyik ng'o

    ReplyDelete
  18. Kweli kunamatatizo makubwa sana mpaka tutakapofanikiwa kupata uongozi bora kwani naona kunawatu wanaotumiwa kutoa sababu za uongo katika uongozi tulionao kwa kupitia njia ya udini.Huu udini unatokea wapi katika viongozi ambao wako madarakani na hawatekelezi majukumu yao ipasavyo?Kweli bado tunasafari ndefu sana kwa staili hii maana hata vyama naona vimeshagawaywa hiki ni cha wakristo na kile ni cha waislam.Kuna watu ambao njaa zao zinawasumbua na ndio hao waoingiza udini katika siasa

    ReplyDelete
  19. Hapa Waheshimiwa tatizo ni elimu tu basi. Maana mtu anadanganywa kwenye mihadhara, si mtafiti, hasomi na kuchambua mambo. Mtu anasema udini unaletwa na viongozi wa kikristo anapshika muislamu madaraka. Kivipi?Upumbavu ulioje huu! Hivi JK yuko pekee madarakani? Au ni jambo gani wanalofaidi waislamu kwa JK kuwa madarakani ambali watu wengine hawafaidi?

    Udini ni sifa ya Mjinga na maskini wa mawazo. Watu hawa hupenda saana kufadhiliwa bila kufanya kazi. Ni rahisi kutumiwa na mafisadi sababu ya njaa zao.

    ReplyDelete
  20. haya ndugu zangu wengine tukisema twaitwa wadini,ila shida ya hawa jamaa ni upeo mdogom katika kuchambua mambo,wamezama mno katika quran,kila kitu wanakiangalia kupitia miwani ya quran,huwezi kuangalia mambo uhalisia wake kwa mtaji huu.badilikeni waislam japo si wote wenye tatizo hili.

    ReplyDelete
  21. PROPAGANDA HII YA UDINI HUPENYEZWA NA CCM KILA MARA. WAKIONA KUNA CHAMA CHA UPINZANI KINA NGUVU WANAIBUA PROPAGANDA HII. WALIANZA NA CUF WAKATI KILIKUWA NA NGUVU NCHI NZIMA WAKAENEZA KUWA NI CHAMA CHA KIISLAM SA NI CHADEMA KWAMBA KINA UKRISTU NA UKABILA, NA WATANZANIA KWA KUWA HATUJISUMBUI KUFIKIRIA TUNATEKWA NA PROPAGANDA HIZI HATARI. SASA NI MATUSI NA KILA AINA YA LUGHA CHAFU KATI YA WAISLAM NA WAKRISTO. HEBU ANGALIENI UHALISIA WA MAMBO NA MJENGE HOJA SI USHABIKI USIO KUWA NA TIJA.

    ReplyDelete
  22. Mpumbavu utamjua tu. Hivi hamkumbuki Mkapa kashtakiwa mahakamani kwa keshi ya rushwa ya M 900? Hamkumbuki jinsi alivyopingwa sana kwenye kasfa za RADA na Ndege ya Rais?

    Hakuna mkristo anayeweza kumtetea mtu sababu ya dini yake, hii iko kwa maamuma wa kiislamu. Wakristo wanaangalia mtu anayejali maslahi ya wanyonge, mzalendo halisi, mtu asiyeogopa kuchukua hatua za dhati bila woga.

    Sasa ukimgusa kikwete Wajinga wanasema huyu ni wa dini yetu, ni UPUMBAVU.

    Mafisadi waliotajwa kina Chenge, Lowasa n.k ni dini gani? Hivi mwenye akili anaweza kusema mapambano ya ufisadi yanayofanywa na Chadema yana udini ndani yake.

    Kweli elimu ni ufunguo wa maisha, mwenye elimu hasikilizi maneno ya mabarazani, ni mchunguzi na mtafiti. NENDENI SHULE KUFUTA UJINGA JAMANI!!!

    ReplyDelete
  23. kujibu swali la huyu Bwana "AKISEMA SHEIKH NI UDINI AKISEMA ASKOFU ANA HAKI YA KUSEMA"
    ni kuwa, mwenye busara haangalii eti kasema NANI bali KASEMA NINI? Hii ndio tofauti kati yetu na nyie, Mnaangalia kateuliwa dini gani sisi tunaangalia CV ya mtu. Ndio maana japo shida za taifa ni moja hatuna malalamiko ya kijinga kama nyie.

    ReplyDelete
  24. Duh. kweli ccm imefanikiwa kudumaza watu. kikwete oyee! malecela oyee! muhidini michuzi oyee!

    oyeeee!

    ReplyDelete
  25. Kwani nini mnamgawa Kikwete? Tokea lini amekuwa ni rais wa Waislamu tu? Ninavyofahamu ni rais wa Tanzania. Ni rais wangu na nina haki ya kumkosoa hata kumfukuza kazi.Think first, usiongee tu kama umekunywa maji ya chooni.

    ReplyDelete
  26. Mimi nimefutilia mjadala huu kwa makini. Kinachokosekana ni BUSARA katika kuzunguzia HOJA. Matusi yametawala mjadala kwa kukosekana UKATIKATI/NEUTRALITY badala ya MAWAZO YA UBINAFSI yanatawala hisia za wachangia mada. JK ni Rais wa Watanzania wote, tunampenda-hatuangalii wala kujadili DINI. Kiongozi wa kikundi cha kidini fulani kupanda jukwaani na KUPENYEZA hisia zake ili apate WAFUASI/SUPPORTORS ni HATARI kutumia mgomgo wa dini. Wakati umefika kwa wafuasi wa dini yo yote ile nchini KUMKANYA KWA AJENDA CHONGANISHI yenye mwelekeo wa kuvunja UMOJA WA KITAIFA. Wafuasi/supportors wa kingozi wa kikundi cha kidini kama huyu wanapaswa kutambua ishara za nyakati na KUMWACHA MWENYEWE JUKWAANI ANAKO-PANDA MBEGU za chuki.

    ReplyDelete
  27. na bado,mtatukanana sana,mkichoka mpigane

    ReplyDelete
  28. Watanzania kuweni na hekima hakuna chama chochote chenye udini hizi ni propaganda za CCM kuwagawa watanzania UFISADI umefanywa na watu wa dini zote tangu enzi za Mwinyi,Mkapa na sasa Kikwete,Kinachofanyika ni viongozi wa dini pamoja na vyombo vya habari kununuliwa kuchomeka ishu za udini ili kuwahamisha watu kutoka mada husika,kumbukeni maaskofu ndio waliosema KIKWETE ni chaguo la Mungu na baadhi kama Lwakatare bado wanapigia kampeni CCM hivyo basi Walewote wanaingiza masuala ya udini katika hoja za msingi za taifa tuwapuuzie,UKWELI ni kwamba CHADEMA kama taasisi huru inachokipigania ni sahihi na kina manufaa kwa kila mwananchi kama kikikaa kimya kisha Sheria mbovu ikapitishwa wakristo waislamu watakaoumia bila kujali imani zao.

    ReplyDelete
  29. Jamani COMMENT hapo juu ni hitimisho tosha. Someni na muishie hapahapo maana. Ukweli Tuwapuuzie wanazoingiza udini katiaka mambo ya msingi.
    ...END....

    ReplyDelete