Na Said Njuki, Arusha
TUKIO la hivi karibuni la kulipukiwa na baruti kwa Mlinzi wa Kampuni ya Madini ya TanzaniteOne ya Afrika ya Kusini katika mchimbo ya Mererani wilayani Simanjiro, Manyara, Bw. Raphael
Aswela limezidi kuwachanganya wadau wa madini hayo baada ya kudaiwa matukio hayo yanatokana na 'dili' za kupora madini ya kampuni hiyo.
Imedaiwa kuwa baadhi ya walinzi wasio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na wachimbaji wadogo kuingia katika migodi ya kampuni hiyo, na kwa kuwa walinzi hao wanaifahamu vizuri wanatumia nafasi hiyo kuwaonesha madini wachimbaji wadogo na kulipua baruti ambazo wakati mwingine husababisha maafa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa na baadhi ya wadau wa madini hayo kwa nyakati tofauti umebaini hali ya ulipuaji wa baruti ulioambatana na fitina na baina ya wachimbaji wadogo na chuki dhidi ya kampuni hiyo ya kigeni umekuwa hatari kwa maisha ya wachimbaji hao.
Bw. Aswela alijaruhiwa vibaya Machi 25 mwaka huu na kilichodaiwa bomu lililotengenezwa kienyeji, licha ya wadau wengine kudai halikuwa bomu bali ni baruti iliyotegwa kulipua sehemu ya mgodi wa TanzaniteOne kwa
lengo la kupora madini hayo.
Wadau hao wamedai siku ya tukio mlinzi huyo akishirikiana na baadhi ya wachimbaji wadogo wa mgodi wa jirani (mmiliki tunamhifadhi) walitega baruti mbili katika mgodi wa kampuni hiyo na ilipolipua baruti ya kwanza mlinzi huyo alikimbilia kuagalia kilichopatikana, ndipo alipokutana na mlipuko wa pili uliomjeruhi vibaya.
Habari zaidi zilidai kuwa mmoja wa wachimbaji wadogo hao (jina tunalo) ambaye mgodi wake unapakana na mgodi wa kampuni ya TanzaniteOne alidai ulipuaji wa baruti katika migodi ya kampuni hiyo kinyemela ni 'dili' ya muda mrefu na hufanyika kwa ushirikiano na walinzi.
Alidai kuwa yeye ni mmoja wa watu waliompandisha mlinzi huyo baada ya kujeruhiwa na baruti hiyo.
"Nikiwa ni moja waliosaidia kumpadisha mlinzi aliyejeruhiwa nakuhakikishia kuwa kazi za migodi hiyo sasa ni dili tupu kwani madini hayo kwa sasa yapo katika kitalu kinachomilikiwa na Tanzanite One tu...na ili kuyapata huna budi kushirikiana na walinzi ambao ndio wanaojua njia za madini na ndivyo ilivyokuwa siku hiyo," alisema mchimbaji huyo.
Aliongeza kuwa iwapo mlinzi huyo angesita kukimbilia madini baada ya mlipuko wa kwanza asingepata ajali ile lakini kutokana na uchu wa kupata, ndio sababu ya kukimbilia na kuhatarisha maisha yake.
Ofisa Madini Kanda ya Kaskazini, Bw. dhamini Mkonyoka alisema uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea na watatoa taarifa rasmi baada ya kukamilika.
unaju katika nilivyo soma nivigumu sana m2 alie panga dili kwenda bila kugundua kua milipuko nilio tega ni zaidi ya mmoja hivyo mi naona nikama propa ganda za kufukia matukio ila ku weka sifa zakampuni la hasha ukweli ana ujua ni marehem ila nimuhimu kufanya uchunguzi wa kina
ReplyDelete