14 April 2011

Tanzania yapanda viwango FIFA

GENEVA, Uswiss

TANZANIA imepanda kwa ubora wa soka duniani baada ya kuchupa kutoka nafasi ya 121 iliyokuwepo hadi nafasi ya 112.Kwa mujibu wa taarifa za
viwango vya soka vinavyolewa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA, Tanzania itakuwa imechupa kwa nafasi 9 kutoka mahali ilipokuwa baada ya kujikusanyia pointi 267.

Kwa upande wa Afrika Ghana imeendelea kuongoza ikiwa inashika nafasi ya 15 ikifuatiwa na Ivory Coast ambayo inashika nafasi ya 21 wakati Misri ipo nafasi ya 36 baada ya kiporomoka kutoka nafasi ya 35 iliyokuwa ikiishikilia kwa mwezi Machi mwaka huu.

Nigeria wao wanashikia nafasi ya 38 wakiwa wamepiga hatua moja kutoka nafasi ya 39 waliyokuwepo  mwezi Machi wakifuatiwa na nchi za Afrika Kusini, Algeria na Burkina  Faso ambazo zinashika nafasi ya 39, 40 na 42 huku Cameroon ikiwa imerudi nyuma kwa nafasi 6 ikiwa katika nafasi ya 48.

Kwa upande wa Afrika Mashariki,Uganda ndiyo inashikilia usukani wa ukanda huo ikiwa nafasi ya 84 ikifuatiwa na Tanzania(112),Rwanda(123), Kenya(124) na Burundi(148).

Kwa Ulaya Hispania bado imeendelea kuongoza ukanda huo ikiwa nafasiya kwanza ikifuatiwa na Uholanzi na Brazil ambazo zinashika nafasi ya pili ya  tatu Ujerumani na Argentina zikiwa zimerudi nyuma  nyuma nafasi moja.

Zinazofuatia katika msimao huo ni England (5),Uruguy(7),Ureno(8),Italia (9) na Croatia ambayo inashika nafasi 10.

No comments:

Post a Comment