Na Mwali Ibrahim
SHIRIKISO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limesema uhaba wa vifaa vya mchezo huo, umekuwa kikwazo kikubwa kwa mabondia kujipima uwezo wao.Akizungumza
Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa BFT, Eckland Mwafisi, alisema shirikisho lao limekumbwa na uhaba wa vifaa ambao unawafanya mabondia washindwe kupima uwezo wao.
Mwaffisi alisema kuwa, vifaa wanavyotumia mabondai wao, vyote vimechakaa, hivyo havifai kufanyiwa mazoezi.
Alisema mbali na vifaa, pia mabondia hao hawana sare, jambo linaloweza kuwafanya wakakosa medali katika mashindano ya Afrika All African Games yatakayofanyika Msumbiji na mashindano ya Community Championship nchini Uganda.
"Mazoezi ya vitendo, ndiyo yanayowajenga mabondia, bila vifaa, hawawezi kujipima vizuri uweo wao," alisema Mwaffisi.
Msemaji huyo ameiomba serikali na wadau wa michezo, kuwasidia vifaa vya mchezo huo ili mabondia waweze kufanya mazoezi katika hali nzuri.
No comments:
Post a Comment