21 April 2011

Chiligati, Nape chupuchupu kuangukiwa jukwaa

Na Eliasa Ally, Iringa

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Mpinduzi (CCM), Bw. John Chiligati na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye wameponea chupuchupu kuangukia na
jukwaa walilokuwa wanatumia kwenye mkutano wao katika Kata ya Mgama mjini Iringa jana.

Mbali na viongozi hao walioko kwenye ziara ya kutambulisha Sekretarieti mpya ya chama hicho, viongozi wengine wa chama hicho  Wilaya ya Iringa Vijijini, akiwamo Mkuu wa Wilaya, Bw. Asseri Msangi walifunikwa na jukwaa hilo.

Wengine waliofunikwa na jukwaa hilo, Katibu CCM wilaya ya Iringa Vijijini Ahamed Mkiri, Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini Bi.
Delfina Mtavilalo; Mwenyekiti wa UWT mkoa, Bi. Zainabu Mwamwindi; Mwenyekiti wa CCM Iringa Mjini, Bw. Abeid Kiponza na mbunge wa Mimbo la Kalenga, Dkt. William Mgimwa.

Jukwaa hilo lilianguka muda mfupi tu ya baada ya Nape na Chiligati kuteremka kwenda kugawa kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho.

Tukio hilo lilitokea jana saa 6:00 mchana, muda mfupi baada ya viongozi hao kuwasili eneo hilo wakitokea Chuo cha CCM cha Ihemi na kuwahutubia wananchi, na kisha kuwapokea wanachama 80 wapya  ambao walidai kuwa wamehama kutoka upinzani.

DC Msangi alisema kuwa tangu awali aliona jukwaa hilo linayumba na aliwaambia  viongozi wa CCM kuwa jukwaa ni bovu kabla ya kuangua wakajibu kuwa haliwezi kuanguka.

Mkutano huo ulitawaliwa na vohoja, kwani awali, Diwani wa Kata ya Mgama, Bw. Disima Lupalla (CCM) alimgomea Bw. Chiligati alipoitwa kutambulishwa kwa wananchi, akisema hatambui ujio wa Chiligati na na wenzake kwenye kata hiyo kwa kuwa hawakumpa taarifa, jambo ambalo alidai ni dharau kubwa.

"Mimi kama kiongozi niliyechaguliwa na wananchi hususani wanachama wa CCM mmekuja kwenye kata yangu bila kunitaarifu, hizo ni dharau mmenidhalilisha mimi, wewe (Chiligati) sikutambui, sikuelewi na ujio wako kwenye kata yangu mimi nauona ni batili," alisema Bw. Lupalla kwa msisitizo hali iliyoshangazwa viongozi hao na wananchi.

Bw. Chiligati alimwacha diwani huyo ili kuwarudisha wananchi ambao walikuwa wanaendelea kushangazwa na tukio la kuanguka kwa jukwaa.

Katibu wa CCM kata ya Ulanda Bw. Gervas Ngakonda na diwani wa Viti Maalumu Kata ya Kiponzero, Bi. Laura Kilyenyi walilaani vikali  ujenzi mbovu wa jukwaa hilo kwa kuwa Dkt. Mgimwa alitoa sh. 500,000 kwa ajili ya shughuli hiyo na limejengwa vibaya hadi kuhatarisha maisha ya viongozi hao.

26 comments:

  1. Ufisadi wa CCM hadi kwenye ujenzi wa majukwaa ya viongozi wao!

    Hawa wananshangazakweli, kama kuna mtu aligharamia jukwaa halafu fedha zikaliwa ni ujumbe tosha kuwa ufisadi umeenea hadi kwenye ngazi ya kata.

    Nape Nnauye, majukumu uliyopewa ni maji marefu kaka. Labda uanze na JK na mwanaye Ridhwan

    ReplyDelete
  2. Toa maoni kuhusu habari iliyoandikwa,CCM wameamua kujikosha kwa wananchi na wanachama, hao waliochaguliwa wameonekana
    wataweza sasa wewe inakuhusu nini eti kusema ni maji marefu kama umeliona hilo nenda kamsaidie wewe na uanze utakavyo!! mimi naona andaa maandamnno kupinga uteuzi wao

    ReplyDelete
  3. Laana ya ccm ndio maana inasababisha hadi majukwaa yanataka kuwangukia mi nawambia ipo siku mtajutia nyie watoto wa Mafisadi kama Nape na Ridhiwan

    ReplyDelete
  4. Nape utakufa mapema sana. nakuhurumia kaka

    ReplyDelete
  5. Mtoa maoni wa 10:38, toa maoni yako acha kumshamnulia mtoa maoni mwingine. Wewe kama umeumia CCM kuitwa mafisadi, wasaidie wewe kujinasua huko. Maoni yatoatolewa sana kuhusu utendaji kazi wa Nape. Katika majukumu aliyopewa amepwaya - tena ametolewa kama mbuzi wa kafara. Kama umeumia sana, jitose wewe kumsaidia.

    Ninamwuunga mkono mtoa maoni, Nape si cho chote si lo lote. Amewekwa kulipiza kisasi kwa Lowassa. Sasa hili nalo unasemaje?

    ReplyDelete
  6. Uko sahihi ndugu yangu wa 12:54. Watu wengine wanakereka na uimara wa CHADEMA kwa hiyo wananfikiri kila anayetoa maoni hapa against CCM ni mwanaCHADEMA. Wawe wavumilivu!

    ReplyDelete
  7. mmenifurahisha sana mlivyompa ukweli huyo mwanaccm. kwakweli kifo cha kisiasa kwa nape kipo karibu sana. anachofanya anaropoka sana na hata hajui anachokiongea impact yake ITAKUWA NI nini kwa baadae. KIUFUPI CHEO ALICHOPATA SASA NDIYO KINAMUUA KISIASA.

    ReplyDelete
  8. Cheo kinamuua si kisiasa tu bali hata kijamii. Nape amelewa madaraka mapema mno. Inaelekea ana ajenda ya siri anayotaka kuitekeleza kwa hao waliotajwa kuwa mafisadi. Ningemshauri kuwa makini sana kwani anadeal na marafiki wa karibu na wa muda mrefu sana na JK - hili liko wazi kabisa.

    ReplyDelete
  9. nashukuru kwamaoni yenu,ccm sasa ni kama imevua gamba na kuwavalisha familia na hiki ndicho kifo cha ccm.tizama Nape amelelewa na mzee makamba akiwa singida so ni mwanae na kaka yake ni january makamba.Mimi c CDM ni mtz ninaye ganga njaa kutokana na mafisadi hao.Watanzania tuwe macho haka ni kamchezo cha kurishishana madaraka.

    ReplyDelete
  10. Watoa maoni hapo juu ni mmoja kajifanya anajiunga mkono uozo wake wewe unamuonea gere kupewa jukumu kubwa wakati ni kijana damu changa inaonyesha nyie mna njama ya kumuua mapema ili ionekane hao kina Lowasa ndio wamemuua,maana kuhusu Lowasa na Nape habari yao ilkwisha zamaaani ktk vikao acheni fitina zenu CDM ni wafa maji hawaachi kutapatapa CCM chama kubwa 2015 sio mbali mtasaga meno tuu,tunajuwa kuna mamluki wanaopewa jukumu la kuandika maoni kila kukicha hata kama ni utumbo! ikifika 2015 mtarudi mtangaze dini muitwe wachungaji wastaafu

    ReplyDelete
  11. MAADIL YA KITANZANIA YAMEPOROMOKA WATU WAMEKUWA WAGUMU KUFIKIRI NA KUTOA MAONO YAO
    NA KUSHAURI NJIA ZILIZOMBADALA NA KUELIMISHANA ILA SASA NI KULUMBANA NA KUKEBEHIYANA NA KILA MMOJA KUJIONA NI MBORA KULIKO MWENZAKE,TUNADHARAULIANA IWEJE WATU TUNAGOMBEA FITO WAKATI NYUMBA TUIJENGAYO NI MOJA?LEO CCM WAMEONA WAVUE GAMBA LA MAOVU LAKINI BADALA YA KUWAPONGEZA LABDA KELELE ZIMEWAAMSHA BADO TUNAWAKEBEHI, NI WANGAPI WALIKUWA WALEVI NA SASA WAMEACHA? WANGAPI WALIKUWA WAZINZI LEO WAMEOKOKA? SI AJABU MTU NI YULEYULE LAKINI KAJIVUA GAMBA LA MAOVU ANAOKOKA TUWAPE NAFASI TUWAONE NI KWELI?LEO VIJANA AMBAO NI JUZIJUZI MLIKUWA MNAWASIFIA BAADA YA KUWAUMBUWA VIGOGO WALIOKUWA WANAKULA MALI ZA UVCCM,LEO MNAWAONA HAWAJAKOMAA,ETI NAO WAMO KTK UFISADI NA KUWAKEBEHI KUWA HAYO MAJI MAREFU KWAO.HIVI UKWELI UKO WAPI?
    WEWE MTOA MAONI 12.54 UNAMWAMBIA MWENZAKO ATOE MAONI ASIMSHAMBULIE MWENZAKE WEWE UNAFANYA NINI MBONA NA WEWE UMEMSHAMBULIA WAKATI ALICHOKISEMA PIA NI MCHANGO WAKE KINA MANTIKI ZUNGUMZA LAKO.CCM IMEONA MBALI
    NA NINAKUBALIANA NA HUYO HAPO JUU KUWA KUNA WENGINE NI MAMLUKI WA KUANDIKA UOZO ILIMRADI WAPINGE TUU HATA MEMA!!

    ReplyDelete
  12. wewe uliyetoa maoni hapo juu haujui kitu ni bendera fuata upepo,ngugu zako wanakufa njaa, matibabu shida ,shule za kata watoo 600 walimu wawili mtoto yupi wa JK anasoma shule za kata kama sio wa walala hoi tu.Fikiri kwanza kabla ya kuchangi acha habari za ushabiki wa kisiasa tuangalie uhalisia wa hali halisi ya mtz .Tunahaja ya kubadilika vinginevyo tatabakia na mfumo wa kifisadi tu.Watz amkeni tumechoka elime itusaidie kufikiria chama kimekubali kina mafisadi wewe unataka nini zaidi KUMBUKA CCM INAWENYEWE

    ReplyDelete
  13. Yeees, hapo pataaamu maana jamaa wamezoea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi, wao ilimadi domo kaya na mzee wao wa kulipuka lipuka!!Poleeeeeni eti kapwaya mtaishia kula kwa maaachoooo!!baada ya miezi 6 atafiti tuu,umemuona na shangishangi lake VX?Mtakufa nacho kijiba cha roohhho

    ReplyDelete
  14. Shangingi ni lake si la kwako. Mama na dada zako wameahidiwa bajaj tena za kuwapeleka hospitali kujifungua watoto ambao ni viumbe wa Mungu na ni Taifa linalotarajiwa.

    Ama kweli, akili ni nywele - unashabikia shangingi la Nape? Wewe kwako tushabikie nini? Au mkokoteni?

    ReplyDelete
  15. hapo juu umesema kweli mwambie huyu jamaa ndugu zake wanatumia bajaji kwenda kujifungua wakati wengine wanatumia shangingi na hospitali zaq ni nje.Unashangilia utadhani mtoto mdogo bwana hivi kweli bajaji ni ya kubeba mama mjamzito kweli kama si dharau ni nini? hebu tujifunze kufikiri na si kushabikia tu c ajbu hat chai haujanywa na haujui utakula nini? kazi kuzalishwa mifulana na kupiga makkofi hata kama ni upuuzi.Tizama maisha ya ndg zet huko kijijin halafu ushangilie sio unabweka tu bila kufikiria.Akili za kuambiwa changanya na zako mbayuwayu we!

    ReplyDelete
  16. Mwambie huyo labda atakuelewa. Ni uzumbukuku unamsumbua. Sisi tunataka maendeleo kwa kila mmoja wetu,na siyo kushabikia shangingi la mtoto wa kigogo aliyezaliwa kwenye raha za pepo na bado wanaendelea kumpa pepo kwa gharama za maisha yetu. Wengi wa wananchi wanaishi maisha ya shida na dhiki halafu sisi hao hao tunaona walio nacho wakiendelea kulundukiwa, halafu sisi tunashangilia!

    ReplyDelete
  17. BILA KUIONDOA CCM, TANZANIA UMASKINI HAUTAISHA. WASHABIKIENI TU ILA ITAKULA KWENU. CCM NI CHAMA CHA WENYEWE SI KWA AJILI YA WANANCHI, KAMWE MATUNDA HAYATAKUWEPO KWA WANANCHI ZAIDI YA MATUMBO YAO NA WATOTO WAO+WAJUKUU.

    ReplyDelete
  18. ...kwa maoni hayo, hukutunakoenda tunawakaribia LIBYA,ngoja tuwakaribishe hao NATO waje kuchukua madini na wanyama pori....

    ReplyDelete
  19. HAAA JUKWAA LILIJENGWA KWA ELFU 50 TU, PESA ZANGINE UNAJUWA ZILIENDA WAPI!

    ReplyDelete
  20. UMEONA JEURI YA MHEHE AU CHIF MKWAWA AJAPEWA TAARIFA KWA HIYO ANAONA UMEMDHARAU MIMI NI MHEHE NINAWAJUA NDUGU ZANGU NDIO MAANA HAWAPEWAGI VYEO SABABU WANAPENDA HAKI WATU WA IRINGA .UNAFIKILI MKOA MWINGINE MTU ANGEMWAMBIA MKUU WAO WA CCM TAIFA NDUGU ZANGU UO NDIO UZEMBE WA KUTOKUTOA TAARIFA NA HAO WAHEHE BWANA WANGEWATOA ROHO ZAO HAWO VIONGOZI WA CCM TAIFA.USIWACHEZEE WAZEE WA IRINGA KUMBUKA DR KRELUU ALIYEKUWA MKUU WA MKOA IRINGA ALIYEUAWA NKWA KUPIGWA RISASI NA MHEHE MWAKA 1972

    ReplyDelete
  21. kujivua gamba bado sumu ya nyoka ni ile ile

    ReplyDelete
  22. Wakati wenzetu wanapanga namna ya kukuza na kuimarisha uchumi wao kwa kuuza bidhaa nje, sie watanzania tumebaki kujadili ufisadi na gamba. Ufisadi hutakwisha kamwe....kwa kuwa hakuna mwenye ubavu wa kujitoa mhanga kupambana nao. Sie wa-tz tumekwisha...Sasa twapondwa (left, right,centre) kiuchumi na wageni. Tayari wazungu wameshateka nchi- mabenki, migodi, viwanda vya bia, viwanda vya cement na sukari. Pole pole wameanza kuteka ardhi...Kenya nao wameanza kutuponda...angalia Kenye Commercial Bank inavyoteka nchi, viwanda vyake kadhaa..n.k.Bado Rwanda na Uganda wajipanga kutushukia...

    Ushauri wangu kwa vijana. Stop kuzaa, maana watoto wenu watakuwa watumwa kwenye nchi yao. Hakuna mgeni anayejenga nchi vijana wangu........

    ReplyDelete
  23. Uko sahihi kabisa mtu wangu. Kenya walituponda zaidi tulipoomba "lift" kwenye Kenya Airways kuwachukua watu wetu kule Libya. Kwani ndege zetu zile tulizojivunia sana na tukaweka picha ya Twiga zilikwenda wapi wajameni?

    ReplyDelete
  24. KILA NIKISOMA HOJA ZINAZOTOLEWA NA WATU, KWA ASILIMIA KUBWA WATU HUANDIKA BUMBA TU ,KWANI WENGI WAO HAWANA AKILI ZA KUSOMA VIZURI NA KUTAFAKARI WANACHOANDIKA. INASIKITISHA SANA KUONA KUWA SERIKALI INALAUMIWA KWA KILA KITU HUSUSA MASUALA YA MAENDELEO. KWA NINI WATU HAWALAUMU WANANCHI WANAOKAA KIJIWENI SIKU NZIMA AU WALE WANAOLIMA NUSU HEKA WAKITEGEMEA KUWA MAPATO YA MAZAO YATATOSHA KWA CHAKULA NA ZIADA KUUZWA ILI KUTOSHELEZA MAHITAJI YA FAMILIA ZAO,KWA NINI WATU HAWAKEMEI UFISADI AMBAO UMETAWALA DAMU YA KILA MTANZANIA ,WATU WANAONA HOUSE GIRL/BOY ,WAHUDUMU OFISINI ,WALANGUZI,nK KUWA WAO PIA NI MAFISADI. WATANZANIA INABIDI TUBADILIKE KIMAWAZO ,TUPUNGUZE KULALAMIKA KUSIKO NA MAANA ,TUPUNGUNZE KUTEGEMEA SERIKALI KUFANYA KILA KITU. MNYALU- BOSTON,USA

    ReplyDelete
  25. Mnyalu wa USA,umesema pia umeshauri vizuri,ndugu zangu wa-tanzania lazima tuzingate ELIMU,ni kweli maisha ni magumu hivyo tusibweteke kwa kudhania hata tukiongozwa na Chama mbadala ya CCM kutakuwa na nafuu wa maisha au ajira bure kwa kwa elimu zetu za FORM SEVEN,tuwe wabunifu.

    ReplyDelete
  26. MH JAMAN SASA HII TOO MUCH WATU WENGINE WANAINGIA KWENYE SAF HII KUZOMEA BILA KUJENGA HOJA ZA MISINGI AMBAZO ZINAWEZA KULETA MABADILIKO YOYOTE KWA KINACHOJADILIWA TUJIFUNZE KUTUMIA UTASHI ZAIDI KULIKO NGUVU

    ReplyDelete