12 April 2011

Patrick Phiri amwaga visingizo

Na Zahoro Mlanzi

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Phiri amesema kushindwa kutwaa ubingwa wa msimu wa 2010/2011 kumetokana na timu yake kucheza michezo mingi
ndani ya muda mfupi, hivyo wachezaji wake kukosa muda wa kutosha wa kupumzika.

Simba ilishindwa kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, licha ya kuifunga Majimaji ya Songea mabao 4-1 huku Yanga wao wakiichapa Toto African mabao 3-0, hivyo kuwa bingwa tofauti ya bao moja.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa juzi uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Phiri alisema ilikuwa ni siku yao ya huzuni kwani kushindwa kutwaa ubingwa kwa utofauti wa mabao si jambo la kawaida.

"Tumecheza michezo miwili mfululizo dhidi ya Kagera Sugar na TP Mazembe ndani ya siku sita, wachezaji walikuwa bado hawajapumzika na tukacheza na JKT Ruvu, sasa ukiangalia hayo yote utaona hatukupata muda wa kupumzika," alisema Phiri.

Alisema pamoja na kushindwa kutwaa ubingwa, lakini anaipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa na kwamba sasa anachoangalia ni kujipanga kwa ajili ya msimu unaokuja.

Phiri alisema katika hilo atakaa chini na Kamati ya Utendaji na kutoa tathmini yake ya msimu mzima, nini kifanyike au ni wachezaji gani wanapaswa kuondolewa na kuongeza wapya.

Akizungumzia mchezo huo kwa ujumla, Phiri alisema walitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini wachezaji wake hawakuwa makini kukwamisha mpira wavuni.

Alisema kutokana na hali hiyo aliamua kumtoa Ali Ahmed 'Shiboli', ambaye alionekana hayupo mchezoni na mabadiliko mengine ili kihakikisha timu yake inafunga mabao meingi zaidi.

2 comments:

  1. I fee that Patric Phiri has no reason to excuse the team by the reason of playing many games within a week.He should remember that Yanga had to trvel from Ethiopia, spend one night to Dar and go to BUKOBA, YET win the game and now they are champions. I will always advise Phiri that, he has to invest more in PSYCHOLOGICAL problems. After that deafeat from TP Mazembe it was clear that plyayers were affected.

    ReplyDelete
  2. Tatizo la simba ni kwamba wachezaji,viongozi pamoja na kocha walishajiamini kupita kiasi na kuanza kucheza mpira katika magazeti bila ya kukumbuka ya kuwa mpira unachezwa uwanjani tena kwa bidii na sio kuweka dharau mbele kwa timu wanazocheza nazo.Hili litakuwa ni fundisho tosha kwa msimu ujao.
    Mechi na TP Mazembe ilikuwa inachezwa kwenye magazeti kwa kujipa moyo ya kuwa TP Mazembe wanafungika,Je wanafungika bila ya maandalizi ya kutosha?Twalib Hilal alishawaambia ya kuwa maandalizi yenu hayalingani na timu mnayocheza nayo lakini hakuna tahadhari iliyochukuliwa.

    ReplyDelete