12 April 2011

Benayoun awataka wenzake kuwa makini Old Trafford

LONDON, Uingereza

KIUNGO wa Chelsea Yossi Benayoun, amesema mechi kati yao na Manchester United kila mchezaji anatakiwa kujua kwamba ni msimu wa timu yao kuwa
umekufa kama watafungwa katika mechi ya marudiano itakayochezwa Old Trafford leo.

Blues itaifuata Manchester United kucheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hatua ya robo fainali huku timu yao ikiwa imepoteza mechi ya kwanza.

Kwa kifupi kama Chelsea itafungwa leo, itapoteza nafasi yake ya kutwaa kombe msimu huu.

Lakini kiungo Benayoun, anatabiri ushindi utasafisha njia kwa ajili ya nema nyingine.

Mchezaji huyo kutoka Israel alisema: "Kila mtu anajua kuwa sisi tutacheza kuokoa msimu wetu. Kila mtu anajua ni mchezo muhimu zaidi wa msimu huu.

"Tunatakiwa kuokoa msimu wetu na kujaribu kufuzu nusu fainali.

"Kuna uwezekano kutoka hapa sisi kumaliza katika nafasi tatu za juu au nne katika Ligi Kuu na kuwa kwenye Ligi ya Mabingwa tena msimu ujao.

"Hivyo kitu pekee kiolichobakia ni kujaribu kutwaa kombe na kombe pekee tunaloweza kutwaa ni Ligi ya Mabingwa.

"Ndiyo maana tunatakiwa kufanya kila kitu na kwa uwezo wetu wote. Kwa sababu kama tutashinda mchezo huu tutabadilisha kila kitu.

"Nina hakika kwamba, kama tutawafunga United tutafika hadi mwisho na kutwaa ubingwa kwa hiyo fainali yetu itakuwa Jumanne (leo).

"Ni wazi tunajua haitakuwa rahisi kwa sababu United ni timu nzuri sana. "Lakini Chelsea imeonesha ubora katika kipindi cha miaka michache iliyopita wanaweza kushinda wakiwa Old Trafford."

Alisema kama Chelsea itacheza kwa kujituma kwa asilimia 100 inaweza kuibuka na ushindi.

Nyota huyo alisema watu wanafikiri kuwa United ina faida ya kushinda ugenini bao 1-0, lakini si kigezo kwa kuwa Chelsea ilishaonesha uwezo kwa kushinda katika Uwanja wa Old Trafford .

No comments:

Post a Comment