Na John Daniel
SEKRETARIET mpya ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema kimebaini mbinu chafu za mafisadi waliopewa siku 90 kujiondoa ndani ya Halmashauri Kuu
(NEC), kuanza kujihami kwa kukihujumu chama hicho na kumhujumu Rais Jakaya Kikwete.
Wamesema wamebaini mbinu hiyo inayolenga kuvuruga hoja ya kuwaondoa ili waonekane kuwa hawana hatia kwa kuwapakazia watu wengine akiwemo Rais Kikwete na familia yake vitendo vya kifisadi kwa lengo la kuondoka na kundi kubwa au kufuta hoja ya kuwaondoa.
Akihutubia mkutano wa hadhara ya kuwatambulisha kwa wana CCM katika uwanja wa Manzeshe maarufu kama Bakhresa jana, Katibu wa NEC Ikitikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye, alisema wamebaini watuhumiwa hao kuwatumia baadhi ya vyama vya siasa na viongozi wa dini kufanikisha azma yao.
"Tumebaini kuwa baada ya kuchukua uamuzi wa kuwaondoa mafisadi kwenye NEC kule Dodoma, wameanza kutumia baadhi ya vyama vya siasa kuhujumu chama, kibaya zaidi wanaelekeza hujuma zao kwa mwenyekiti wetu na familia yake.
"Licha ya kutumia viongozi wa baadhi ya vyama pia wanatumia hata baadhi ya viongozi wa dini kutaka kuhalalisha hoja yao, kudanganya Watanzaia na kutaka kufuta dhambi zao mbele ya jamii ili ionekane chama chote hakifai na si wao,"alisema Bw. Nape na kuongeza.
"Nataka niwaonye kuwa wasianzishe vita vya mawe wakati wanaishi kwenye nyumba ya vioo, tulipoanzisha vita vya ufisadi hatutanii, sababu tunayo, nia tunayo na uwezo tunao,"alisisitiza Bw. Nnauye.
Alisema uamuzi wa kuwapa nafasi ya kutumia busara zao kujiondoa wenyewe ilikuwa ya makusudi hivyo wasithubutu kukihujumu chama hicho na Mwenyekiti wake Rais Kikwete kama walivyoanza.
Alisema CCM haina ugomvi na vyama vya siasa kwa kuwa inapenda kukuza demokrasia nchini ndio maana hata wakisema maneno ya kashfa na uchochezi haiwachukulii hatua japo ina uweo wa kufanya hivyo.
"Sisi tunasema hatutaki malumbano na vyama vingine kutokana na hujuma za mafisadi tunaotaka waondoke kwenye NEC. Tunawashauri waondoke salama wasituchokoze hivyo,"alisema.
Alisema tayari watu hao wameanza kutuma watu wao kwenda kwa viongozi wa vyama vya siasa na dini kupika uongo wa kusema jukwaani na kwenye madhabahu jambo ambalo ni hatari kwa taifa.
"Hawa watu wameanza kusemwa kwa muda mrefu na wanajua hilo hata wao wenyewe kuwa si wasafi. Iweje leo waambiwe waondoke kwa ustaarabu kisha waanze kutumia baadhi ya vyombo vya habari na vyama vya siasa kumchafu Mwenyekiti wetu na familia yake.
"Nataka nisisitize tena kuwa watashindana na sisi lakini hawatashinda,tutapigana hadi tuwashinde kwa kuwa tuna uhakika na kile tunachofanya,tumedhamiria,"alisisitiza Bw. Nnauye.
NAPE MWONGO KABISA, CCM SIKU ZOTE IMEKATAA KATAKATA KWAMBA HAKUNA UFISADI WAPINZANI NI WAONGO,NA MWENYEKITI WA CCM KIKWETE ALIKUWA AKIWASIMAMISHA WATUHUMIWA WA UFISADI KUWA NI WATU WAZURI WAKATI WA KAMPENI,IWEJE LEO ASEME KUNA UFISADI? KIKWETE NI MNAFIKI ANAKULA KOTE,HAKUNA DAWA CCM ITAPASUKA TU.NJIA WALIOTUMIA SIYO SAHIHI ILIHITAJIKA HEKIMA ZAIDI.WAMEMWAGA PETROLI KWENYE MOTO..KIKWETE HAWEZI KUPONA KWENYE KASFA ZA UFISADI YUMO KAMA ASINGEKUWEMO ANGESHAWAKAMATA WOTE..YUMO HUMO KWENYE UFISADI WALA HASINGIZIWI YUMO NDANI.
ReplyDeletesasa nyie wabongo misioni kama mnafanya kazi kwa kweli kila kukicha kikwete au slaa nn sasa na ss tusiokuwa na vyama inakuwaje?kwakweli wengine inatukwaza
ReplyDelete